....Kifo kitatuunganisha.

Naisujaki Lekangai

JF-Expert Member
Aug 19, 2012
1,343
2,000
Bwana mmoja huko Texas Marekani kwa jina Raul Hinosoja alimpata mchumba wake Yvonne Lamas mwaka 2006, na walipanga kufunga harusi ya kukumbukwa. Chochote walichokifanya kuanzia mwaka huo 2006 kilikuwa ni kwa maandalizi ya harusi yao.

Maandalizi hayo ghafla yalikumbwa na dosari pale Raul alipogundulika kuwa na ugonjwa wa saratani ya damu mwaka 2012. Maandalizi ya harusi yakageuka maandalizi ya matibabu na october 2016 Raul alilazwa hospitali. Mwanzoni mwa december 2016 madaktari walisema:"Tumejaribu yote kwa uwezo wetu, hatuwezi tena"Watu wa Raul walielewa maana ya msemo wa madaktari, na walimkaribisha kiongozi wa roho azungumze na Raul.
"Nini ombi lako la mwisho mwanangu?" Kiongozi wa dini alimwuliza Raul ambaye alijibu anataka kutunza ahadi ya kufunga ndoa na mpenzi wake Yvonne.
Harakaharaka matayarisho ya harusi yalifanywa pale hospitali na wawili hao walifunga ndoa 8/12/2016. Baada ya masaa 36 Raul alifariki dunia.
Soma zaidi hapa https://www.yahoo.com/gma/dying-man-granted-wish-marry-fianc-e-hospital-210213891--abc-news-sex.html
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom