Kifo cha Sumari: JK atuma salamu za rambirambi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kifo cha Sumari: JK atuma salamu za rambirambi

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by bibikuku, Jan 19, 2012.

 1. bibikuku

  bibikuku JF-Expert Member

  #1
  Jan 19, 2012
  Joined: Feb 16, 2011
  Messages: 828
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 35
  Salamu za Rambirambi toka kwa Rais JK

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete amemtumia salamu za rambirambi Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Anne Semamba Makinda (Mb.,) kutokana na kifo cha Mhe. Jeremia Solomon Sumari, aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Arumeru Mashariki kwa tiketi ya CCM na Naibu Waziri wa Fedha na Uchumi, kilichotokea usiku wa kuamkia leo tarehe 19 Januari, 2012 katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili alikokuwa amelazwa kwa matibabu.
  “Nimeshtushwa, nimesikitishwa na kuhuzunishwa sana kutokana na taarifa za kifo cha Mheshimiwa Jeremia Solomon Sumari kwani alikuwa kiongozi aliyewatumikia vema wananchi wa Jimbo lake la Uchaguzi la Arumeru Mashariki na Taifa kwa ujumla katika wadhfa wake wa Waziri kwa umahiri na uhodari mkubwa”, amesema Rais Kikwete katika salamu zake. Rais Kikwete amesema kutokana na kifo chake, wananchi wa Arumeru Mashariki wamepoteza kiongozi wa kutegemewa sana huku Taifa likiachwa na pengo kubwa ambalo si rahisi kuzibika ikizingatiwa kwamba alikuwa kiongozi katika Wizara ambayo ni mhimili muhimu kwa maendeleo ya nchi yetu. “Kwa dhati ya moyo wangu, natuma salamu za rambirambi na pole nyingi kwa familia ya Marehemu Jeremia Sumari kwa kumpoteza kiongozi na mhimili madhubuti wa familia. Ninawahakikishia kwamba nipo pamoja nanyi katika kuomboleza msiba huu mkubwa, na namuomba Mwenyezi Mungu, mwingi wa Rehema aipumzishe roho ya Marehemu Jeremia Solomon Sumari mahali pema peponi, Amina”, ameongeza kusema Rais Kikwete. Ameiomba familia ya Marehemu kuwa na moyo wa uvumilivu na subira katika kipindi hiki kigumu cha maombolezo ya mpendwa wao kwa kutambua kuwa yote ni mapenzi yake mola.

  Imetolewa na IKULU
  19 Jan 2012
   
 2. andrewk

  andrewk JF-Expert Member

  #2
  Jan 19, 2012
  Joined: Apr 13, 2010
  Messages: 3,103
  Likes Received: 55
  Trophy Points: 145
  sasa anatuma salam za pole kwa spika, mbona nasikia alikuwa bado hajala kiapo?
   
 3. jino kwa jino

  jino kwa jino JF-Expert Member

  #3
  Jan 19, 2012
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 769
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  wamechanganyikiwa hawajui hata watume kwa nani salamu za rambirambi
   
 4. m

  mtengwa JF-Expert Member

  #4
  Jan 19, 2012
  Joined: Aug 20, 2011
  Messages: 1,745
  Likes Received: 225
  Trophy Points: 160
  Kazi kweli kweli
   
 5. Graph Theory

  Graph Theory JF-Expert Member

  #5
  Jan 19, 2012
  Joined: Jul 2, 2011
  Messages: 3,803
  Likes Received: 1,116
  Trophy Points: 280
  Kazi ipo
   
 6. Vmark.

  Vmark. JF-Expert Member

  #6
  Jan 19, 2012
  Joined: Aug 2, 2011
  Messages: 1,361
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 0
  Na atatuma xana....wengi bado wanafuata with me inclusive!!
   
 7. Kigogo

  Kigogo JF-Expert Member

  #7
  Jan 19, 2012
  Joined: Dec 14, 2007
  Messages: 20,498
  Likes Received: 1,453
  Trophy Points: 280
  Yaaani hizi angejitumia yeye mwenyewe kama mwenyekiti wa chama...ndo tabu hii watu wagonjwa bado tu mnatiamajitiamaji kuwasimamisha wagombee..haya sana mnaleta uchaguzi usio hata wa lazima..muwe mnapima wagombea afya kama wanavofanya timu za mpira ulaya..
   
 8. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #8
  Jan 19, 2012
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 308
  Trophy Points: 180
  Salamu sawa atume!
  Lakini kubwa kuliko yote mwambieni anasubiriwa na wana Arusha aje kuzika!
   
 9. ndetichia

  ndetichia JF-Expert Member

  #9
  Jan 19, 2012
  Joined: Mar 18, 2011
  Messages: 27,641
  Likes Received: 236
  Trophy Points: 160
  na sasa hv lazima ccm kitapigwa chni vibaya kwani kibubu chake kimeshaishia ndo maana hawapendi kuona mb anafukuzwa ama kufariki...

  Poleni sana wana arumeru east kwa msiba wa mbunge mteuliwa wa jimbo lenu..
   
 10. Mzito Kabwela

  Mzito Kabwela JF-Expert Member

  #10
  Jan 19, 2012
  Joined: Nov 28, 2009
  Messages: 17,520
  Likes Received: 1,691
  Trophy Points: 280
  Job true true
   
 11. Pelle mza

  Pelle mza JF-Expert Member

  #11
  Jan 19, 2012
  Joined: May 15, 2008
  Messages: 749
  Likes Received: 71
  Trophy Points: 45
  Pole sana Mwenyezi Mungu ailaze roho ya marehemu mahali pema peponi. AMINA
   
 12. Daffi

  Daffi JF-Expert Member

  #12
  Jan 19, 2012
  Joined: Jun 25, 2011
  Messages: 3,803
  Likes Received: 178
  Trophy Points: 160
  Nafikiri ataambulia matusi na mabango ya kumkejeli.
   
 13. Fekifeki

  Fekifeki JF-Expert Member

  #13
  Jan 19, 2012
  Joined: Nov 18, 2011
  Messages: 1,163
  Likes Received: 164
  Trophy Points: 160
  Ni kweli, wagombea wote wapimwe afya kabla ya kugombea ili kuepusha gharama zinazoepukika! CHADEMA Twaja huko,
   
 14. Mwanajamii

  Mwanajamii JF-Expert Member

  #14
  Jan 19, 2012
  Joined: Mar 5, 2008
  Messages: 7,080
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 0
  hizi comment za kitoto zinajulikana ni watu gani na wa upande gani.mnataka na wenzenu waanze kuyasema makosa ya marehemu wa juzi?hebu wekeni itikadi zenu pembeni,suala la kifo ni la kila mtu bila kujali we chadema au mama yake na nani.acheni ushamba...................................rest in peace sumari.tulikupenda sana lakini mungu amekupenda zaidi.
   
 15. Mwanajamii

  Mwanajamii JF-Expert Member

  #15
  Jan 19, 2012
  Joined: Mar 5, 2008
  Messages: 7,080
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 0
  sawa kabisa,madereva wote nao wapimwe ulemavu wao kabla hawajapewa magari ili kuepusha uzembe barabarani.
   
 16. Mungi

  Mungi JF Gold Member

  #16
  Jan 19, 2012
  Joined: Sep 23, 2010
  Messages: 16,985
  Likes Received: 441
  Trophy Points: 180
  Hivi ushemeji wa Sumari na Lowassa ukoje?
  Je, ni nani anamkanyagia mwenzake?
  Hawa mabepari wana siri sana
   
 17. Mwanajamii

  Mwanajamii JF-Expert Member

  #17
  Jan 19, 2012
  Joined: Mar 5, 2008
  Messages: 7,080
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 0
  wee ndo umechoka kweli.ivi kwa nini marehemu alikuwa anaendesha gari kwa mwendo mkali wakati ni mlemavu na hana leseni?
   
 18. Mwanajamii

  Mwanajamii JF-Expert Member

  #18
  Jan 19, 2012
  Joined: Mar 5, 2008
  Messages: 7,080
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 0
  mbowe anamkanyagia mtei
   
 19. Mungi

  Mungi JF Gold Member

  #19
  Jan 19, 2012
  Joined: Sep 23, 2010
  Messages: 16,985
  Likes Received: 441
  Trophy Points: 180
  hili swali halihitaji kuwauliza Great Thinkers, hata mama yako anaweza kukupa jibu nzuri tu!
   
 20. Mungi

  Mungi JF Gold Member

  #20
  Jan 19, 2012
  Joined: Sep 23, 2010
  Messages: 16,985
  Likes Received: 441
  Trophy Points: 180
  sawa, niambie Lowassa na Sumari nani anamkanyagia mwenzake? ni hilo tu
   
Loading...