Mwalimu enzi hizo aliwahi kusema kama Kawawa na Jamal(waziri wa fedha) wa muda mrefu ) siyo waaminfu basi Tanzania hakukuwa n mwaminifu. Pia Sokoine alipotaka kuwachunguza mawaziri kwa ufisadi alimwambia sokoine, nitawalinda wateule wangu na sokoine akanywea. Uadilifu na uchapakazi wa sokoine hauwezi kutiliwa mashaka na MTU yoyote , na ni MTU pekee aliweza kutofautiana na Mwalimu na bado Mwalimu akamvumilia. Ndiye alianza daladala za binafsi baada ya magari ya serikali ya UDA kushindwa kuhudumia umma wa Dar akaona unateseka. Sokoine alikuwa wa aina ya pekee lakini ukiacha mihemuko ya muda mfupi yenye nia njema, huwezi kumlinganisha na Mwalimu aliyeongoza taifa kwa miaka 23 kwa usalama hadi akaacha madaraka kwa hiari yake. Pia uteuzi wa waziri mkuu sokoine alikuwa pendekezo la mzee Kawawa sababu sokoine alitoka waziri wa nchi ofisi ya waziri mkuu wakati huo ni Kawawa akapewa uwaziri Mkuu. Kama walikuja kukosana baadae , sasa haina Rafiki wa kudumu. Tatizo LA nchi changa democracy zetu ni dhaifu hiyo Sokoine alikuwa ahead of time hadi kufikiria kuwakamata mawaziri. Hivi alisahau naye ni mtele wa RAIA. Pale Karimjee Mwalimu alibanwa kuwa kawaachia wahujumu uchumi waliokamatwa. Mwalimu nakumbuka alisema Mimi nimemwachia mmoja tu (nadhani Barongo kama sijashau) lakini nyie mumeachia wengi ,sasa aliposema nyie alimaanisha watu mpaka nashindwa kuelewa hiyo kauli .Akamalizia kusema uteuzi wa viongozi ni sawa na kuchota Maji kisimani, . ukichota Maji kisimani ukakuta Maji ni machafu basi ujue Maji yote kisimani ni machafu. Nadhani alikuwa kila anayemteua anamuona ana element za ufisadi sasa tuliarajia alete watu kutoka wapi?. Ukitaka kujua unafiki wa binadamu jukwaani tunalaani mafisadi lakini watu kwenye vyeo vya kuweza kufisadi tunaishi nao na tunajua maendeleo (ukwasi wao) unavyozidi kipato chao halali lakini nani amewahi kwenda tume ya maadili kulalamikia hilo? labda wezi wa kuku ndio tunawachoma moto. Yatosha kusema Mwalimu na Sokoine will remain our great heroes , each in his capacity. Na mnakumbuka kuna watu baadae walishitaki serikali kuhusu kuonewa kwenye mambo ya uhujumu uchumi walishinda na walifidiwa baadaye .Hapo ndio utajua Mwalimu alikuwa visionary mno ndio maana hakushabikia watu wateswe kwa hisia za MTU na nchi anaongoza yeye. Nia njema
aliiona lakini approach tena ndani yake unvunjaji wa katiba hakuafiki lakini wasioona mbali tunaishia kushangilia Fulani kafilisiwa na roho zetu zinafarijika bila kujiuliza je hiyo hela alyonyang'anywa inakuja kwangu .MIHEMUKO KWA KISINGIZIO CHA UZALENDO MWALIMU WAS ABOVE THAT WEAKNESS. NA NCHI HUWA HAIBAKI SALAMA HATA SIKU MOJA .Mfano mzuri ni Venezuela Leo nchi yenye akiba ya mafuta kuliko zote duniani lakini Leo wanatambaa kiuchumi. kuna mwanafalsafa mmoja mhindi alisema (YOU CAN NOT LIFT THE WAGE EARNER BY TEARING DOWN THE WAGE PAYER.) Mwenyezi MUNGU hajakosea wema na waovu amewaacha duniani tunaishi sambamba .Wajibu wetu ni kukemeana MTU anpokwenda kinyume na maadili .