Kifo cha Floyd na unafiki wa Waafrika

Kifo cha Floyd na unafiki wa Waafrika

MIGNON

JF-Expert Member
Joined
Nov 23, 2009
Posts
4,116
Reaction score
5,119
Mmarekani mweusi amekandamizwa shingoni kwa dakika nane na kupoteza maisha.Maandamano na ghasia vikaibuka Marekani na nchi zingine.Africa hatukubaki nyuma kulikemea jambo hili.Huu ni unafiki mkubwa kwani kwenye nchi zetu hayo yamefanyika sana na kwa uwazi lakini hatukemei.

Kwanza,kitendo hiki kimechukuliwa kuwa ni ubaguzi wa rangi,hii ni picha unayoipata kama hutataka kushughulisha akili yako.Kwa Marekani uhalifu mwingi unatendwa na watu weusi na hata magereza yao yamejaa watu weusi.Kwa nini watu weusi wawe ndio wengi wanaofanya makosa,hili ndilo la kuangalia zaidi.

Polisi mzungu ametuhumiwa kuua lakini hebu hata hapa kwetu tuangalie je Polisi akienda kumkamata mtuhumiwa wa uhalifu wa kabila la Wapare atakwenda kwa style hiyo hiyo kumkamata mtuhumiwa wa Kikurya?Miji ya Marekani isiyo salama ni miji yenye Weusi wengi.

Mikononi mwa Polisi hata hapa kwetu yametokea,kuna mtu alifungwa pingu na kuchoma kisu akiwa ndani ya gari ya Polisi,muulize Kasusura alichokipata kwa Zombe na mengi mengineyo.

America ina mengi yanayofanya weusi waingie matatani zaidi na historia ni sababu mojawapo.

Tukio la Marekani liwe fundisho kwa vyombo vyetu vya usalama katika kuboresha utendaji wao.
 
Hapa kuna watu watakuja kukupinga kisa tu wamekariri kuwa mzungu akimkosea mwafrika ni ubaguzi wa rangi.

Lkn mimi siku zote naamini ubaguzi wowote ni mbaya hata uwe wa kidini, kikabila, kisiasa, kijinsia, kirangi nk.

Kwa wengine tuliyowahi kuishi nchini Marekani tunaelewa ulichoandika. Wamarekani weusi na weupe wana viwango vya maisha vinavyotofautiana sana.

Nilipokuwa huko miaka ishirini iliyopita niliwahi kumuuliza Mmarekani mmoja mweusi kuwa, kwa nini nyie hampendi sana kufanya kazi kama wazungu wanavyofanya?

Alinijibu kuwa, "Sisi tunaamini kazi za shuruti mababu zetu walizofanyishwa enzi za utumwa na kupelekea wengi wao kupoteza maisha na kuwa msingi wa utajiri wa nchi hii inatosha kutuwezesha sisi leo kulipwa hata bila kufanya tena kazi".

Madhila waliyofanyiwa watu weusi enzi za utumwa ni makovu ambayo yamekataa kupona kwa wengi wa jamii ya wamarekani weusi hadi leo na vile vile wapo jamii ya wamarekani weupe ambao bado wanaamini kuwa mtu mweusi ni mtumwa tu siku zote.

Biashara ya utumwa ni dhambi mbaya ambayo imechangia mtu mweusi kunyanyapaliwa sana na labda kama isingekuwepo labda leo watu weusi wangekuwa na kaunafuu fulani humu duniani na cha kusikitisha zaidi ni kuwa hata kitabu cha Mungu kama Biblia haikulaani utumwa na tena ni kama iliubariki tu, (Kutoka 21:1-11).
 
Back
Top Bottom