Shobi
JF-Expert Member
- May 31, 2015
- 3,401
- 4,371
Ni taarifa ya kushtusha sana ya msiba wa mwanasiasa chipukizi na jasiri, Deo Filikonjombe kutokana na ajali ya Helikopta jana jioni maeneo ya mbuga ya Selous mkoani Morogoro. Ni pigo lingine kubwa ambalo katika kipindi kifupi Taifa limepata, huku bado likiwa na kidonda cha kuondokewa na wana siasa wengine mahiri, Marehemu Celina Kombani, Dr Abdallah Kigoda na Dr Emanuel Makaidi aliyefariki jana.
Filikonjombe alikuwa Mbunge mahiri aliyesimama imara kutetea maslahi ya wananchi wa jimbo lake la Ludewa na watanzania kwa ujumla. Alikuwa mwiba kwa serikali ya Chama chake CCM kutetea maslahi ya nchi, mfano ni katika kashfa ya Escrow ambapo alikuwa Makamu Mwenyekiti wa kamati iliyochunguza kashfa hiyo.
Mwenyezi Mungu awape moyo wa subira, familia, jamaa, marafiki na wananchi wa Ludewa, katika kipindi hiki kigumu cha kuondokewa na mpendwa wao
.BWANA AMETOA, BWANA AMETWAA JINA LAKE LIHIMIDIWE.
Edward N. Lowassa