Hatuiombei kifo CCM lakini tunasema miaka 50 inatosha, hali ni mbaya kiasi kwamba haivumiliki zaidi ya kuiondoa CCM madarakani, mfano:Kanali wa JWTZ wa bandia kakamatwa. polisi wa usalama barabarani wa bandia kakamatwa,daktari wa bandia kakamtwa Muhimbili, dawa za mamilioni ya shilingi za bandia zimekamatwa,kituo cha afya cha bandia kimefungwa, dawa za kupunguza makali ya ugonjwa wa ukimwi za bandia zimekamatwa,mbolea ya ruzuku ya bandia imekamatwa, madawa ya mifugo ya bandia yamekamatwa, dawa za kuua wadudu za bandia zimekamatwa, barabara kuanzia Chalinze hadi Mlandizi ya bandia, barabara kati ya Dar es Salaam na Mtwara halijakamilika tangu miaka ya 90, askari magereza wamekamatwa na nyama ya twiga!? askari wa kituo cha Oysterbay wamekamatwa na pembe za ndovu huko Kisarawe, askari wa kituo cha Dumila wamekamatwa na kifuu cha binadamu kwenye mfuko wa rambo, askari wa Arusha wamekamatwa na magunia 18 ya bangi, walimu wanaidai serikali zaidi ya sh bilioni 30, matokeo yake asilimia 94 ya wanafunzi waliofanya mtihani wa kidato cha nne mwaka jana wamefeli, mafuta ya treni zinazoenda bara kuliko kusafirishwa na treni yanasafirishwa na maroli ya kukodi (badala ya mafuta kusafirishwa na treni zenyewe wenzetu hawa wanakodi malori),Mzungu mmoja huko bandarini ameweka bomba lake linalochota mafuta kutoka kwenye bomba la serikali, majambazi wamevamia kituo cha polisi cha kati Mwanza, fimbo ya dhahabu ya IGP imeibwa, wazee zaidi ya miaka 60 wameahidiwa matibabu bure kutoka hospitali yeyote ya umma lakini dawa hakuna, Watanzania hawaaminiki tena popote duniani kwa sababu ya kujihusisha na madawa ya kulevya, Dar es Salaam kwa sasa inaaminika kuwa ndiyo njia kuu ya kupitisha madawa ya kulevya Afrika Mashariki, wananchi wanaendelea kuumizwa na tindikali, hakuna mahali unapoweza kupata huduma ya kuridhisha bila kutoa rushwa.Listi ni ndefu, sasa katika hali kama hii chama kile kile, serikali ile ile, viongozi wale wale, tutatokaje hapa, hapana tunahitaji mabadiliko. Naomba kutoa hoja.