Kifo cha Balali ni Hekaya za Abunuasi!

Kifo cha Balali ni Hekaya za Abunuasi!

tpaul

Platinum Member
Joined
Feb 3, 2008
Posts
27,181
Reaction score
27,781
Hekaya za 'Kifo' cha aliyekuwa gavana wa BoT aliyeikimbia nchi kwa sababu ya kushiriki ufisadi wa EPA, bado zinaendelea kuvuma masikioni mwa watanzania. Na inaonekana watunzi wa HEKAYA hizi wamejipanga vizuri hadi kufikia hatua ya kugharamia utunzi mzima wa hekaya.

Hitimisho la hekaya hizi limeanza kutungwa na vyombo mbalimbali vya habari hapa nchini, ambapo mmoja wa watunzi hao amegharamiwa safari ya kwenda Marekani kupiga picha ya kaburi feki lililoandaliwa na kisha kuandikwa jina la DAUDI BALLALI na picha hizo zimekusudiwa kutumika kunogesha hadithi kwenye gazeti analoliandikia.

Ndugu zangu, watanzania wa leo sio wajinga kama watu wengi wanavyodhani. Uongo unaotungwa kwamba eti Balali hakutaka mwili wake uonekane kwa watu, ni hekaya ambazo kila mtanzania mwenye akili timamu hawezi kuzikubali. Hata mtoto wangu wa miaka 3 anayesoma chekechea atakataa uongo huo. Tukio zima la 'kifo' cha balali ni hadithi ya kusadikika. Kovu la EPA alilosababisha Balali haliwezi kufutika mioyoni mwa watanzania.
:yield:
 
Hekaya za 'Kifo' cha aliyekuwa gavana wa BoT aliyeikimbia nchi kwa sababu ya kushiriki ufisadi wa EPA, bado zinaendelea kuvuma masikioni mwa watanzania. Na inaonekana watunzi wa HEKAYA hizi wamejipanga vizuri hadi kufikia hatua ya kugharamia utunzi mzima wa hekaya.

Hitimisho la hekaya hizi limeanza kutungwa na vyombo mbalimbali vya habari hapa nchini, ambapo mmoja wa watunzi hao amegharamiwa safari ya kwenda Marekani kupiga picha ya kaburi feki lililoandaliwa na kisha kuandikwa jina la DAUDI BALLALI na picha hizo zimekusudiwa kutumika kunogesha hadithi kwenye gazeti analoliandikia.

Ndugu zangu, watanzania wa wale sio wajinga kama watu wengi wanavyodhani. Uongo unaotungwa kwamba eti Balali hakutaka mwili wake uonekane kwa watu, ni hekaya ambazo kila mtanzania mwenye akili timamu hawezi kuzikubali. Hata mtoto wangu wa miaka 3 anayesoma chekechea atakataa uongo huo. Tukio zima la 'kifo' cha balali ni hadithi ya kusadikika. Kovu la EPA alilosababisha Balali haliwezi kufutika mioyoni mwa watanzania.
:yield:

Kama kweli hajafa basi atakuwa kafanyiwa upasuaji na kumbadilisha sura, usikute yupo apa nchini anajia tu na sura bandia
 
Balali akipita humu jf nadhani hua anacheka sana kuona jinsi wananchi tunavyogeuzwa misukule na kuaminishwa eti kafariki.
 
Kama kweli hajafa basi atakuwa kafanyiwa upasuaji na kumbadilisha sura, usikute yupo apa nchini anajia tu na sura bandia

Kweli kabisa mkuu. Na iwezekana yumo humu jf anatuchora tnavyodanganywa na mafisadi na baadhi yetu kukubali uongo huo.
 
Kweli kabisa mkuu. Na iwezekana yumo humu jf anatuchora tnavyodanganywa na mafisadi na baadhi yetu kukubali uongo huo.

Kuna kipindi rais wa nchi hii aliambiwa asijidai eti kuna amani wakati anaongoza maiti, na kweli hii nchi ina maiti tupu, hakuna kuhoji, hakuna kudadisi ila ni kupamba na kulamba miguu ya watawala. Tuna taabu sana.
 
kwaiyo wewe ni maiti?
 
Nifikirie kwa kadri ya uwezo wako wa kufikiri.

labda ungesema watanzania ni waoga kuchukua hatua ingekuwa Kenya lazima wangekinukisha mfano wa maiti sio mzuri BTW, time will tell
 
labda ungesema watanzania ni waoga kuchukua hatua ingekuwa Kenya lazima wangekinukisha mfano wa maiti sio mzuri BTW, time will tell

hiyo falsafa ya 'maiti' aliitoa mzee jomo kenyatta kwa mwl nyerere, enzi zile za 'zidumu fikra za mwenyekiti', hasa kuzingatia ukweli kwamba enzi hizo nyerere & co walikuwa wakiwaongoza watanzania utadhani wanaongoza maiti---hakuna kuhoji wala ku-question jambo lolote hata kama wananchi hawafurahishwi nalo!!
 
balali mnaweza mkawa mnapishana nae kariakoo mjini au kwenye ma supermarkets na hamumjui!
 
Back
Top Bottom