DIDAS TUMAINI
JF-Expert Member
- Nov 11, 2014
- 242
- 680
Serikali DHALIMU ya mwendazake ilimshtaki ndugu yangu mmoja kwa kesi ya uhujumu uchumi. Akakamatwa, biashara zake zikafungwa, na fedha zilizokua kwenye akaunti zake zikachukuliwa. Akakaa rumande zaidi ya mwaka mmoja bila dhamana.
Akaacha mtoto wa miezi mitatu nyumbani. Mtoto akadhulumiwa haki yake ya malezi ya baba. Yeye anadai hakufanya jinai isipokua aliadhibiwa kwa sababu za kisiasa. Askari upelelezi wa kesi yake siku moja alimuapia kuwa UTAFIA JELA.
Tulipoenda kumtembelea magereza akatuambia kwamba ameambiwa na mpelelezi wa kesi yake kwamba atafia jela. Tukatafuta namba ya simu ya huyo mpelelezi kumuuliza kama ni kweli alitamka maneno hayo. Akaishia kutukana matusi mazito.
Mtoto akaendelea kukua hadi kufikisha mwaka mmoja bila kumfahamu baba yake mzazi. Mama yake akaenda kanisani akalia kwa uchungu na kumkabidhi Mungu kesi hiyo. Wafanyabiashara wenzake wakamtaka akiri ili afanye "plea burgaining" alipe na aachiwe lakini akasema hawezi kukiri kosa ambalo hajalifanya. Akasota jela zaidi ya mwaka mmoja.
Mapema mwaka huu yule mpelelezi akakutwa amefia nyumba ya kulala wageni, akiwa uchi na madawa ya kuongeza nguvu za kiume pembeni. Inadaiwa alikua na mwanamke lakini mwaanamke huyo hakufahamika. Habari yake "ikafichwafichwa" ili kuepusha aibu kwa Jamhuri.
Miezi michache baadae (Mama akiwa tayari madarakani) ndugu huyo akafutiwa kesi yake na kuachiwa huru bila masharti yoyote. Akaunti zake zikafunguliwa na baadhi ya fedha zikarudishwa (si zote). Akaanza maisha upya. Jumapili moja tukafanya ibada ya shukrani kwa ajili ya wema ambao Mungu amemtendea, baadae tukawa na tafrija kidogo nyumbani kwake Mbweni.
Kwenye ile tafrija akasema "nimesahau kumualika rafiki yangu mmoja, askari upelelezi aliyeniapia kuwa nitafia gerezani. Ningefurahi angekua hapa kushuhudia ukuu wa Mungu kwamba sijafia gerezani" Lakini tukamwambia alishakufa. Alifia nyumba ya kulala wageni. Kifo cha aibu.
Malisa GJ