mcTobby
JF-Expert Member
- Feb 16, 2018
- 6,499
- 18,170
Japan miaka yake ikiwa kwenye peak, ilikuwa ni moja ya nchi tishio barani Asia kama tu Ujerumani ilivyokuwa tishio barani ulaya enzi zile za vita kuu ya pili ya dunia.
Sasa ndani ya jeshi la Japan kulikuwa na kitengo cha kitabibu kulichokuwa mahsusi katika kufanya tafiti za kisayansi za kiutabibu kikichojulikana kama Unit.731.
Kitengo hiki kilijulikana kwa ukatili wa hali ya juu katika kuwafanyia majaribio ya kitabibu wafungwa wakiwa hai. Kwa mfano watu walikuwa wakigandishwa kwenye friji, watoto wakifanyiwa upasuaji pasipo kuwekwa nusu kaputi(anesthesia), na la zaidi kutumia mabomu yenye vimelea vya magonjwa kwenye maeneo ya makazi ya watu. Lengo la haya yote ni kufanya utafiti wa kitabibu katika kutengeneza silaha za kibayolojia na za kikemikali kwa ajili ya kutumiwa na jeshi la japan kwenye uwanja wa vita.
Katika haya yote mtu katili kabisa katika historia ya vita kuu ya pili ya dunia aliyekuwa akisimamia kitengo hiki cha unit 731, alikuwa daktari mmoja wa kijapani aliyeitwa Shirō Ishii.
Huyu bwana Shirō Ishii kwanza kihistoria alizaliwa kwenye familia ya kishua(wealthy japannoblefamily)mwaka 1892.
Huyu bwana shirō baada ya kutunikiwa PhD kwenye kitivo cha sayansi ya Microbiology alijikuta akipanda vyeo kwa haraka sana ndani ya jeshi la Japan's Imperial Army medical corps. Huyu bwana kiufupi hakuwa na interest sana na maswala ya udaktari bali alikuwa na uchu tu wa madaraka.
Baada ya azimio la Geneva la mwaka 1925, kupiga marufuku kupiga vita matumizi ya silaha za sumu za kibayolojia, huyu bwana Ishii aliamua kuunda kitengo no.731 ndani ya jeshi la japan kwa ajili kufanya tafiti za kitabibu kwa wafungwa kwa siri sana.
Kitengo hiki kilitengeneza facility kwa ajili ya tafiti hizi zilizopigwa marufuku kwenye eneo la hurbin ndani ya jimbo la Manchuria la china lililokuwa likitawaliwa na Japan. Ikatengenezwa maabara ya kawaida ikiaminika ilikuwa ikifanya shughuli zake za utafiti wa tiba, kumbe ndani yake ilikuwa ni kama bucha ya kuwachinja watu wakiwa wazima wazima. Hii ilikuwa ni moja kati ya kiwanda cha kifo /death factory kuwahi kutengenezwa enzi ya vita kuu ya pili ya Dunia. Walioshia ndani ya hii maabara walikuwa wafungwa wa kivita ikiwemo wamarekani,wachina , wakorea na wamongolia pamoja na akina mama na watoto.
Unyama uliokuwa ukifanyika ndani ya maabara ya Unit.731 ilikuwa kama ifuatavyo;
Hizo ndizo zìlikuwa tafiti chache kati ta nyingi zilizokuwa zikifanywa na daktari huyu. Na hakika watu walikufa haswa.
Sasa baada ya Japan kujisalimisha baada ya kupigwa na mabomu ya nagasaki na Hiroshima mwaka 1945 na U.s, huyu daktari Shirō Ishii aliamua kuiharibu maabara hii iliyokuwa ikisimamiwa na unit731 . Lengo haswa ilikuwa kupoteza ushahidi wowo ambao ungemtia hatiani kama ambavyo Wanazi wa Ujerumani walikuwa wamepelekwa kwenye mahakama ya Nuremberg katika kuhusika kwao katika uhalifu dhidi ya ubinadamu. Hivyo aliamua kufuta kila aina ya ushai na hata wafungwa waliokuwa kwe3 hii maabara kwa ajili ya utafiti waliuliwa wote waliobaki ili kuficha ushahidi.
Umoja wa usoviet wakati huo ulitaka huyu daktari afikishwe mahakamani kujibu kesi zilizokuwa zinamkabili kuhusiana na kile alichokuwa akikifanya, lakini Marekani waliamua kucheza Deal na huyu daktari. Deal gani hilo?
Marekani walivutiwa na tafiti zake hizo ,hivyo wakamtaka huyu daktari awakabidhi nyaraka zote zinazohusihana na tafiti za kitabibu alizokuwa akifanya kisha apewe KINGA ya kutoshtakiwa . Na kweli serikali ya marekani ikaamua kuficha ushahidi wowote kuhusiana na huyu daktari na hakuwahi kupelekwa jela na akapewa makazi na kila kitu na serikali ya marekani mpaka alipokuja kufa mwenyewe mwaka 1959 kwa saratani. Miaka ya Baadaye sana madaktari na wanasayansi watafiti waliokuwa chini ya kitengo hiki cha Unit.731 ndio hao hao waliokuja kuimarisha sekta afya na tiba ya japan hadi leo hii.
Credit😱nline magazine articles.

- Vivisection without Anesthesia. Huu ulikuwa utaratibu kitabibu ambapo ndani ya maabara za Unit.731 wafungw walikuwa wakifanyiwa upasuaji wa kitabibu pasipo kuchomwa zile sindano za ganzi au nusu kaputi (anesthesia). Baada ya kufanyiwa upasuaji mtu akiwa mzima , viungo vya ndani kama figo, moyo, mapafu na maini , vilikuwa vinachomwa vimelea vya magonjwa vya syphilis, anthrax au hata plague, hivyo madaktari wangeweza kubaini athari za vimelea vya magonjwa kwenye viungo vya ndani ya mwili wa mtu kwa garaka zaidi. Kwa mfano ikatokea labda maini yangeathirika na vimelea hivyo, madaktari walikuwa wanayaondoa kwa kuyakata haraka ilihali mtu huyu akiwa mzimamzima kabisa. baada ya hapo baada ya kukamilisha utafiti wa kitabibu, mtu huyo angeuliwa kabisa kisha kuzikwa au kuchomwa moto au pengine angetumiwa baadhi ya viungo vyake kwenye utafiti mwingine baadaye .
- Frostbite experiment. Huu ulikuwa utafiti maalumu ambao ulilenga kuwasaidia jeshi la japan watakapokuwa wanapigana kwen mazingira yenye changamoto ya baridi kali. Hivyo maabara hii ya Unit.731 ilikuwa ikiwatumia wafungwa katika utafiti huu ambapo wafungwa mikono yao ilikuwa inawekwa kwenye eneo la baridi kali hadi pale ngozi itakapobadilika na kuwa nyeusi. Lengo la daktari ishii katika utafiti huu ni kuweza kubaini ni kwa namna gani mwili wa mwanadamu unaweza ku survive kwa muda mrefu kwenye mazingira yenye baridikali.
- Weaponizing the plague. Huu ulikuwa ni utafiti mwingine uliofanywa na daktari huyu, lengo haswa lilikuwa kutumia virusi vya tauni kama silaha ya maangamizi. Kwa mfano utafiti huu ulitumia ndege vita kumwaga wadudu kama chawa waliowekwa virusi hivi vya tauni kisha kunyunyizwa kwenye vijiji vya wachina. Pia maji na vyakula vilivyowekwq vimelea vya ugonjwa wa tauni vilisambazwa kwa watu wa maeneo ya china ili kuweza kubaini ni kwa kiwango gani na kwa kasi ipi ugonjwa wa tauni unaweza kusambaa kwenye population ya watu. Pia panya waliochomwa vimelea vya tauni walisambazwa maeneo ya mijini katika kuharakisha usambaaji wa tauni. Inakdiriwa watu zaidi ya laki 5 walikufa na tauni kutokana na huu utafiti wa wajapan.
- Disease-Infected Prostitution Rings. Huu nao ulikuwa ni utafiti wa aina yale uliofanywa na daktari huyu bwana Ishii wa Unit.731 ili kubaini ni kwa namna gani magonjwa ya kuambukiza ya ngono yanasambaa in real time. Katika utafiti huu bwana ishii alikuwa akiwatumia makahaba kwa kuwalazimisha kufanya ngono na wanaume ambao walikuwa wameambukizwa tayari magonjwa ya zinaa ili kubaini inachukua muda gani mtu kuambukizwa ugonjwa wa zinaa kutoka kwa mtumwingine. Pia wanawake wajawazito walibakwa mara kwa mara ili kuweza kubaini namna mimba zinavyoathirika na magonjwa haya ya zinaa.