Kifaa kutoka angani chaanguka Mynmar

Donatila

JF-Expert Member
Oct 23, 2014
7,561
21,538
_92395971_14992004_655381534623658_2142885126795475518_n.jpg


Kifaa kikubwa cha chuma kimeanguka kutoka angani katika eneo la migodi Kaskazini mwa Myanmar

Kifaa hicho cha muundo wa mviringo, kilichopatikana siku ya Ijumaa katika jimbo la Kachin, kina urefu wa mita 4.5 na upana wa mita 1.2.

kifaa kingine cha chuma chenye maandishi ya kichina kilitoboa paa la nyumba iliyo karibu wakati mmoja lakini hakuna mtu aliyejeruhiwa.

Inakisiwa kuwa kisa hicho huenda kinahusiana na satellite ya China iliyorushwa angani.

Wakaazi walisema kuwa walisikia sauti kubwa kabla ya kifaa hicho kuanguka

Maafisa kutoka kwa idara moja ya ulinzi iliyo karibu, wanasema kuwa kifaa hicho kilipingirika umbali wa mita 50 kabla ya kutua eneo moja lenye matope .

"Tulishikwa na hofu kwa sababu ya mlipuko huo," mwanakijiji Ko Maung aliliambia gazeti la Myanmar Times.

Vifa hivyo vinaaminiwa kuwa vya satellite au sehemu za injini ya nge au kombora.

Chanzo: BBC
 
itakua debris za satelite huko anga za juu kuna takataka nyingi sana imefikia wakati NASA wanataka kupeleka mtambo wa kusafisha anga wanaogopa zinaweza ku hit international space station
 
wahakikishe hzo rocket zao zinaburn vizur na sio vipande vkubwa km hvyo vinarud dunian halaf mbaya zaid vinaenda angukia kwe nchi ambazo hata hazijawah peleka makokoro huko juu...hawa wa china juz ndo wamerusha dude lao huko juu hebu waende markan na urusi wakapige chabo kdg kwann wenzao hawadondosh michuma namna hio
 
mungu turehemu maana sasa hawa wataalam washazid rusha rusha mambo yao yaajabu na naona hapo palikuwa na explosion kabla ya hii kitu kudondoka
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom