KIDUME CHA MBEGU BABATI;Mwalimu awapa mimba wanafunzi wake | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

KIDUME CHA MBEGU BABATI;Mwalimu awapa mimba wanafunzi wake

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Pdidy, May 27, 2009.

 1. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #1
  May 27, 2009
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,249
  Likes Received: 5,631
  Trophy Points: 280
  Mwalimu awapa mimba wanafunzi wakeAdvertisement
  [​IMG]


  Wednesday, May 27, 2009 12:00 PM
  MWALIMU wa Shule ya Msingi ya Qwam iliyopo Kata ya Kiru Wilayani Babati Mkoani Manyara ametuhumiwa kuwabaka na kuwapa mimba wanafunzi wake wawili wanaosoma darasa la saba katika shule hiyo.Imedaiwa kuwa wanafunzi hao waliopewa mimba na mwalimu huyo, mmoja ana umri wa miaka 15 na mwingine ana miaka 17 wote wakisoma darasa la saba na hali iliyowafanya wanafunzi hao kukatisha masomo kutokana na mimba hizo.

  Kaimu Kamanda Mkoani Manyara, Daudi Siasi amethibitisha kuwa mtuhumiwa huyo alikamatwa Mei 21, mwaka huu huko Arusha alikokuwa amekimbilia.

  Alisema kuwa mwalimu huyo alikuwa na uhusiano wa kimapenzi na wanafunzi hao kwa kipindi kirefu na alikuwa akiwarubuni kwa kuwapa kazi za kufanya nyumbani kwake.

  Alisema kuwa mwalimu huyo alikuwa anatumia mbinu ya kuwapa kazi nyumbani kwake na wanapofika huko ndipo alikuwa anatumia mwanya huo kutimiza adhma yake hiyo.

  Alisema wanafunzi hao waligundudulika baada yakuwa mahudhurio yao shuleni yalikuwa hayaridhishi ndipo uongozi wa shule ulipowaita kwa nyakati tofauti wanafunzi kwa ajili ya kuwahoji.

  Ndipo kila mmoja aligundulika kuwa ana mimba na alipoulizwa alimtaja mwalimu huyo kuwa alimpa mimba hiyo.

  Alisema baada ya kuzagaa kwa taarifa hiyo mwalimu alitoroka tokea Mei 4 mwaka huu na kukimbilia kwao mjini Arusha na alikamatwa Mei 21 kwa kutumia mgambo wa kijiji.

  Katika mahojiano makali na wanafunzi hao ilisemekana kuwa mwalimu huyo aliweza kumbaka mwanafunzi wa miaka 17 kati ya Septemba 17, mwaka jana na kumrudia tena Januari mwaka huu, hivyo mpaka sasa mwanafunzi huyo ana mimba yenye umri wa miezi minane.

  Na aliweza kumbaka mwanafunzi mwenye umri wa miaka 15 kati ya Novemba 15, mwaka jana na kumrudia tena Machi 23, mwaka huu na hadi sasa mwanafunzi huyo ana mimba yenye umri wa miezi mitano.

  Kamanda huyo alisema mwalimu huyo ataweza kufikishwa Mahakamani kujibu mashtaka hayo leo.
   
 2. Swahilian

  Swahilian JF-Expert Member

  #2
  May 27, 2009
  Joined: Apr 28, 2009
  Messages: 585
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  Haya ndio tusemapo kwamba maadili ya waalim na hata wafanyakazi wengine wanapopewa dhamana ya kusimamia mambo fulani, haya ona jinsi mwalimu anavyohusiana na wanafunzi kiasi hicho, ni suala ambalo sasa limekithiri tanzania, walimu wanapigana vikumbo kugombania vibinti na kuharibu maisha yao, nasikia uchungu juu ya hilo na hasa nikitazama hali halisi na ugumu wa maisha utaowakabili mabinti hao, serikali,jamii na mamlaka wajaribu kutetea hayo
   
Loading...