Kidogo tuzichape na shemeji mtarajiwa

Kidogo tuzichape na shemeji mtarajiwa

Kama mtakumbuka wiki iliyopita niliomba sampuli ya barua ya ukweni, nawashukuru kwa ushirikiano wenu, nilifanikiwa kuipeleka ila kidogo iibue zahama.

Mke mtarajiwa alinihint kuwa kaka yake ni mtata, basi mtoto wa mjini nikaamua kuvunja taratibu, siku ya kupeleka na mimi nikaenda ili kupambana, tumefika fresh tu, wakatupokea, na sisi bila ajizi tukaikabidhi barua yetu.

Si mnajua mambo ya kuchomekeana, tukataka kuona mwelekeo wao, sasa kila ukiuliza kitu kaka mtu anaponda kana kwamba hataki dada yake aolewe, ikafikia pahali anatujibu kwa kutudhalilisha.

Nilipoona hali inakuwa ngumu nikamvaa shemu mtarajiwa, hali ilichafuka nikataka kumkunja shati tukaamuliwa, nikamwambia hata kama hataki dada yake nitamchukua hata bila process, asinibabaishe, maana dada yake nishmwagia sumu hawezi kusikia la mtu.

Tulitoka pale bila hata kula na mawazo sana, hivi pamoja na heshima yote ya kufata process bado kuna watu wa hovyo hivi? hivi anajua heshima anayotaka kuipata watu wanaililia?.

hii inapaswa kuwa breaking news
 
umechemka wewe hata kama utamuoa huyo dada mtu, kwanza unaonesha uende kwa shari pengine ndo maana ukaona anakuponmda hata kwenye maswali yake ya msingi tu
 
watalinywa wao, wanawake kibao wanatafuta waume nitapata shida wapi mimi.
Wewe bado hujawa tayari kuoa. Kwa atitude hii ya kuona kuwa kuoa ni kumpa favor huyo unayemuoa inabidi ukae chini ujiulize upya ni kwa nini unataka kuoa vinginevyo tarajia vurugu tu huko mbeleni kwenye ndoa yako
 
Huna uvumilivu hata kidogo halafu unakuja hapa unajisifu kha
 
Muache huyo kaka aoe dada yake maana hana adabu
 
Back
Top Bottom