Kidogo tuzichape na shemeji mtarajiwa

Kidogo tuzichape na shemeji mtarajiwa

Kama mtakumbuka wiki iliyopita niliomba sampuli ya barua ya ukweni, nawashukuru kwa ushirikiano wenu, nilifanikiwa kuipeleka ila kidogo iibue zahama.

Mke mtarajiwa alinihint kuwa kaka yake ni mtata, basi mtoto wa mjini nikaamua kuvunja taratibu, siku ya kupeleka na mimi nikaenda ili kupambana, tumefika fresh tu, wakatupokea, na sisi bila ajizi tukaikabidhi barua yetu.

Si mnajua mambo ya kuchomekeana, tukataka kuona mwelekeo wao, sasa kila ukiuliza kitu kaka mtu anaponda kana kwamba hataki dada yake aolewe, ikafikia pahali anatujibu kwa kutudhalilisha.

Nilipoona hali inakuwa ngumu nikamvaa shemu mtarajiwa, hali ilichafuka nikataka kumkunja shati tukaamuliwa, nikamwambia hata kama hataki dada yake nitamchukua hata bila process, asinibabaishe, maana dada yake nishmwagia sumu hawezi kusikia la mtu.

Tulitoka pale bila hata kula na mawazo sana, hivi pamoja na heshima yote ya kufata process bado kuna watu wa hovyo hivi? hivi anajua heshima anayotaka kuipata watu wanaililia?.

Kulinda hadhi issue ya kupeleka barua ungewaachia watu wengine wewe ukabaki una subiri feedback. Hivi mshenga kazi yake nini?
 
Kulinda hadhi issue ya kupeleka barua ungewaachia watu wengine wewe ukabaki una subiri feedback. Hivi mshenga kazi yake nini?

huyu jamaa anaonekana mgomvi tu. Anadai mchumba wake alimuhint kuwa kaka yake ni mtata akaamua kuvunja utaratibu ili aende kupambana. Sasa kwa kauli hii si unaonekana kabisa ulishapanga ushari toka awali?
 
Yaani wewe bwana.......ulijipanga kupambana???kwanza siku ya barua sio lazima ww kwenda,ungemtuma mshenga na wawakilishi hata 2 kwa upande wako then ungebaki kusikilizia kwako.

Ila kama story ya kijiweni hii
 
Umeenda ukweni kibangibangi. Kama ulishauriwa waliokushauri ni wavuta bangi achana nao watakuharibia maisha. Kama hukushauriwa basi nakushauri uache kuvuta bangi tena inaelekea ni bangi mbichi za kutoka mlima meru Arusha, mgeta Morogoro, Mara au Tabora zinazochanganywa kwenye mashamba ya tumbaku.
 
Mkuu neno moja ninaloweza kukuambia 'huna busara kifup ushalikoroga mtafute mshikaji kimya kimya uombe msamaha...hlf acha kuwa na kiburi kiivyo hta km dada yake anakupenda kuwa mstaarabu
 
kwani alikuambia nini mpaka ukaudhika namna hiyo? ulipaswa uvumilie tu

nikiyasema hapa uzi huu utafungwa mara moja, itoshe tu kusema ulikuwa ni udhalilishaji, yaani alituona kama tumeenda kufanya utani, watu tumeacha majukumu yetu. Pia kitendo cha yeye kutolipa thamani tukio hilo kiliniudhi sana sana.
 
mmmh sidhani kama ni kweli umpige shemu huku unataka mke... huyo bibie akikubali kuolewa na wewe ni famba huyo binti
 
...sijui hatua ya utoto ile ya kupigana aliivuka!!!
DEMBA, kingine kilichoniudhi ni pale aliposema kwetu mtu haolewi bila milioni 10, hivi hata kama ungekuwa wewe ungevumilia yote hayo?
 
Last edited by a moderator:
Mtaka cha uvunguni sharti ainame sio kuinua kitanda.
 
Yaani wewe bwana.......ulijipanga kupambana???kwanza siku ya barua sio lazima ww kwenda,ungemtuma mshenga na wawakilishi hata 2 kwa upande wako then ungebaki kusikilizia kwako.

Ila kama story ya kijiweni hii

nishasema yeyote atakayekuja mbele yangu kunikwamisha namchukulia kama katangaza vita.
 
Duh! Jarib kucontrol hisia na hasira ndugu,busara huepusha shari
 
Mtaka cha uvunguni sharti ainame sio kuinua kitanda.

mimi wala siinui kitanda, kama kitu chenyewe ni locomotive nawasha moto tu lazima kitoke.
 
mmmh sidhani kama ni kweli umpige shemu huku unataka mke... huyo bibie akikubali kuolewa na wewe ni famba huyo binti

yaan sijui kwann siku hizi humu jf watu wanatoa stor za uongo. Mtu mzma anakaa nyuma ya keyboard na kuanza kuandika uongo
 
Back
Top Bottom