Kidogo tuzichape na shemeji mtarajiwa

Kidogo tuzichape na shemeji mtarajiwa

JEKI

JF-Expert Member
Joined
Aug 16, 2013
Posts
4,845
Reaction score
2,968
Kama mtakumbuka wiki iliyopita niliomba sampuli ya barua ya ukweni, nawashukuru kwa ushirikiano wenu, nilifanikiwa kuipeleka ila kidogo iibue zahama.

Mke mtarajiwa alinihint kuwa kaka yake ni mtata, basi mtoto wa mjini nikaamua kuvunja taratibu, siku ya kupeleka na mimi nikaenda ili kupambana, tumefika fresh tu, wakatupokea, na sisi bila ajizi tukaikabidhi barua yetu.

Si mnajua mambo ya kuchomekeana, tukataka kuona mwelekeo wao, sasa kila ukiuliza kitu kaka mtu anaponda kana kwamba hataki dada yake aolewe, ikafikia pahali anatujibu kwa kutudhalilisha.

Nilipoona hali inakuwa ngumu nikamvaa shemu mtarajiwa, hali ilichafuka nikataka kumkunja shati tukaamuliwa, nikamwambia hata kama hataki dada yake nitamchukua hata bila process, asinibabaishe, maana dada yake nishmwagia sumu hawezi kusikia la mtu.

Tulitoka pale bila hata kula na mawazo sana, hivi pamoja na heshima yote ya kufata process bado kuna watu wa hovyo hivi? hivi anajua heshima anayotaka kuipata watu wanaililia?.
 
mmmmnh siku ya kwanza tu umeonyesha utovu wa nidhamu ukweni nahisi hizi ni kamba unatufunga
 
we huna self control? haya sasa umeshaonekana huna busara....
 
Ulienda umejiandaa kwa mapambano, kama ulitonywa ni mtatat mtu mwenye hekima ungejishusha mambo yakapita mwisho wa siku uyo kaka angejiona mjinga ila ulienda na defence kubwa sana na ulikuwa umempania labda hata hakuongea vibaya sana ila wewe kichwani ulikuwa umeishaweka kuwa kila kiltu chake ni ovyo. Pole sana sana umeonyesha utovu wa nidhamu wa hali ya juu.
 
hata kama ungekuwa na busara kiasi gani kwa yule jamaa lazima ungechoka, maana alikuwa ni kutukatisha tamaa tu. Nilimvumilia sana.
 
we huna self control? haya sasa umeshaonekana huna busara....

ninayo sana, ila jamaa alizidisha, nilivumilia mengi, kila kitu kina elastic limit.
 
hata kama ungekuwa na busara kiasi gani kwa yule jamaa lazima ungechoka, maana alikuwa ni kutukatisha tamaa tu. Nilimvumilia sana.

Huenda alikuwa anakupima ili kujua aina ya mtu anayetarajia kuoa Dada au Mdogo wake. Sasa kwa hayo uliyofanya, tegemea kukosa mke maana ukoo mzima hautakubali, watakuona wewe mtu wa shari. Na ushukuru Mungu kama ingekuwa baadhi ya mikoa hasa kule Kanda ya Ziwa ungepigwa marungu !!!
 
anhaaa, ulitaka nivumilie kudharauliwa? hata mke si angenidharau maana angejua hayupo salama, kitendo cha kumpigania lazima akione cha kishujaa.
 
anhaaa, ulitaka nivumilie kudharauliwa? hata mke si angenidharau maana angejua hayupo salama, kitendo cha kumpigania lazima akione cha kishujaa.

kupigana siku ya kwanza umefka ukweni tena na kaka yake ambae alishakutonya kuhusu characters zake alafu akuone shujaa? Hakikuwa kitendo kzuri kijana we ulikuwa pale kwa mda ungevumilia kwan hujawah kuvumilia kitu kingne hata kikubwa zaidi ya hicho ktk maisha yako? Pale ni ukweni kuna heshima yake. Nakuasa usirudie tena na wala usijivune kwa ulichotenda tena ikiwezekana nenda kaombe msamaha katka maisha kuna wakati inabidi ujishushe mambo yaende
 
anhaaa, ulitaka nivumilie kudharauliwa? hata mke si angenidharau maana angejua hayupo salama, kitendo cha kumpigania lazima akione cha kishujaa.

Sio kumpigania kwa kuwapiga ndugu zake tena kabla hujamuoa !!! Linapokuja suala la ndugu unatakiwa kutumia busara, kama usingepigana wangekuona una busara na wangekuamini zaidi. Kumbuka damu ni nzito kuliko maji, katika hali ya kawaida hata iweje huyo Dada hawezi kukupenda kuliko ndugu zake, kinachokusumbua wewe ni mhemko tu kwa huyo Dada. Kitendo cha wewe kumpiga Kaka mtu kitatafusiriwa kuwa utakuwa unampiga dada mtu. Kumbuka katika maisha ugomvi hauamuliwi kwa ugomvi bali ugomvi huamuliwa na upole. Ugomvi ukiamuliwa kwa ugomvi huienga chuki. Hivi mtu akikudaharau anakupunguzia nini katika mwili wako ?
 
kwani alikuambia nini mpaka ukaudhika namna hiyo? ulipaswa uvumilie tu
 
Back
Top Bottom