Kidogo kuhusu usalama wa atm na mabenki

Yona F. Maro

R I P
Nov 2, 2006
4,202
218
MADA HII IPO HAPA KUNA NINI NBC

NIMEAMUA NIILETE HAPA KIDOGO ILI TUWEZE KUSHIRIKI PAMOJA

Ndugu zangu nimeona mlichochangia hapo napenda kusema kwamba ni kweli kuna msako wa kutafuta wahalifu wanaoendesha mitandao hii ndani ya nchi pamoja na nchi zingine lakini moja ya tatizo kubwa ni kwa baadhi ya nchi kutoshirikisha nchi zingine katika taarifa za wahalifu unaohusiana na mitandao hili ni tatizo kubwa na la pili ni kwa watu wanaohusika na masuala ya mitandao kwenye vyombo vya dola kutokuwa na uelewa mpana kuhusu masuala haya matokeo yake ni kukuta kwa mfano askari anamtumia mtu wa IT kumtafutia taarifa Fulani kweye benki au sehemu nyingine wakati unakuta huyo huyo anashirikiana na wenye benki hizo kama mdau samweli alivyosema hapo juu , haya mengine ni masuala ya kibenki sijawahi kufanya kazi benki kwahiyo sijui sana masuala mengine nimeandika yale ambayo yako wazi .

Mfano kuna mtu mmoja aliwahi kukamatwa kwa kosa la kutumia Kadi ya ATM ya mwingine pale mlimani city kununulia vitu kwanza alinunua vitu vya kama laki 4 hivi akaondoka mara ya pili alivyorudi ( siku nyingine ) akatumia kadi hiyo hiyo lakini alikamatwa kwa kuwa ilishindwa kufanya kazi nakumbuka alipelekwa kituo cha mabatini kesi yake sijui iliishia wapi lakini mtu kama huyu angeweza kuwa msaada sana hawa ndio kati ya watu wa mwanzo kabisa kuanza kufanya uhalifu unaohusiana na ATM Hapa nchini .

Nchini Malaysia napo kuliwahi kuwa na uhalifu kutumia kadi za ATM zilizotolewa na benki moja hapa nchini kwa muda wa wiki moja rafiki yangu mmoja aliniambia pesa zilizotolewa benki hiyo haikuweza kurecover

Kuna wakati niliwahi kumwona mtu mmoja anatengeneza mashine za kutolea photocopy ndani ya benki moja jijini dsm ambaye kati ya mwaka 2000 na 2005 amewahi kutuhumiwa na makosa kadhaa nchi moja lakini kwetu anadunda .

Suala la hawa watu au kampuni zinazopewa kandarasi za kuweka mashine za ATM pamoja na shuguli zingine zinazohusiana na mashine hizo kama ubora wa mashine na vifaa vingine vya kiulinzi vinavyohusiana na mashine hizo za ATM

Pili ni suala la benki nyingi kutokuwekeza sana kwenye masuala ya Usalama kwenye vitengo vyao vya teknohama hili ni tatizo kubwa sio kwa benki tu hata kwa sekta nyingine za kiserikali nchini hata mfano wanapoamua kutumia tekinologia mpya hawaijaribu kupata taarifa za uhakika hii ipo haswa kwenye benki ndogo au sehemu ambazo benki zinafikiri kuna wateja kidogo kwahiyo wanaweka ulinzi na tekinologia za kizamani , tumeona jinsi benki ya NBC inavyofanya ukarabati wake sasa hivi naamini inaweza kuwa chachu kwa benki zingine pia .

Na ATM zinaendeshwa na windows systems na tunajua jinsi wahalifu wanavyojaribu kuvamia kwa kutumia njia kadhaa ili kuweza kupata upenyo wa kuendesha uhalifu wao , hata hivyo pamoja na jitihada zote hizi kufanyika njia rahisi zaidi zinazotumika kuendesha uhalifu huu ni kwa kutumia wafanyakazi wa ndani wa benki au taasisi hizo .

Ili kuweza kudhibiti au kupunguza uhalifu wa aina hii yapasa watu wengi zaidi washiriki katika kuhakikisha suala hili linafanikiwa hili sio suala la benki inayokupa huduma hii pekee ni suala linalohusisha wateja , wafanyakazi wa benki , vyombo vya usalama na wadau wengine mbalimbali .

Wizi na uhalifu mwingine sio tu una peleka hasara kwa benki lakini pia inapunguza uaminifu wa wateja kwenye benki husika hii inaweza kuchangia kushuka matumizi ya ATM kwenye masuala ya kifedha kwa baadhi ya wateja ingawa ni muhimu kwa benki kuhakikisha inatoa ulinzi zaidi kwenye sehemu ambazo zina usalama mdogo ambapo mashine hizo zimewekwa .
 
tatizo hawa wezi wanakimbia kitechnolojia wakati vyombo vyetu vinatambaa
 
Nitakuwa na kipindi kujadili suala hili siku ya jumatatu kuanzia saa 10 mpaka 11 kwenye kituo cha radio Morning cha jijini dar es salaam , Karibuni sikilizieni kwa maswali na masuala mengine muhimu
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom