Darmian,
Akili inakuaje sharp? Hivi unadhani kucalculate 3444.22323^2 / 8483.2233344 * 32.333 inafanya akili iwe sharp au inapoteza muda kwa mambo yasiyo ya msingi ambayo hakuna anayefanya kwa ubongo siku hizi?
Form four wanajua vizuri hesabu basic hizi kujumlisha na kutoa, hakuna sababu yoyote ya wao kufanyia kichwa tena namba ndefu ambazo hakuna mtu anatumia kichwa kucalculate, ubongo sharp inamaana dunia nzima wanakosea bongo tu ndo mnajua kukuza ubongo wa watu uwe sharp? miaka ya nyuma ambapo walikuwa hawatumii calculator na ubongo wao sharp wamefanya nini hadi leo?
Wanaotumia calculator wamekuletea computer, simu, wamefika mwezini, leo wanatengeneza rocket kuruka kwenda mars, sisi ambao miaka yote tulikua hatutumii huo ubongo sharp umetuletea nini? tumetengeneza hata jembe la kulima kweli? au hata majembe tuna-weld kwa kutumia machine walizotutengenezea watumia calculator?
Nimejua kwa nini elimu ya bongo haibadiliki, sababu ni wengi hampendi mabadiliko mmekariri ila hamkusoma mkajua challenges zilizopo Tanzania, tunapoteza muda kwenye mambo ya kijinga badala ya kufocus kwenye uelewa ambacho ndio kitu cha muhimu.
Unavyojifunza kutengeneza daraja litakaloweza kusimama urefu flani na kupitisha magari ya tani kadhaa, huendi kujifunza kujumlisha na kutoa, hayo yote utatumia calculator, unaenda kujifunza utumie material ipi, uliweke daraja katika angle ipi, utahandle vipi upepo, pressure ya maji etc. Hivyo ndio vya muhimu vya kujifunza 99.99999%. hiyo 0.00001% ya calculation inafanywa kwa computer siku hizi kwa kua binadamu kawaida hua tunafanya makosa kucalculate namba ndogo.
Embu jaribu kukubali mabadiliko sio mmekaa na njia zenu za kizamani ambazo hazijawafikisha popote pale.