Kichere: TRA imeshindwa kufikia lengo la ukusanyaji kodi kwa miaka minne

Return Of Undertaker

JF-Expert Member
Jun 12, 2012
4,572
26,868
Kichere: TRA imeshindwa kufikia lengo la ukusanyaji kodi kwa miaka minne

====
Wakati Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) ikipitia mabadiliko makubwa ndani ya miaka mitano, Mdhibiti na Mkaguzi wa Hesabu za Serikali (CAG) amesema imeshindwa kufikia malengo ya ukusanyaji mapato kwa kipindi hicho.

Tangu Rais John Magufuli alipoingia madarakani mwishoni mwa mwaka 2015 ameshafanya mabadiliko ya makamishna wanne katika mamlaka hiyo ilia kuboresha ukusanyaji wa mapato

Alianza kwa kumwondoa aliyekuwa Kamishna Rished Bade na kumteua Dk Philip Mpango ambaye kwa sasa ni waziri wa Fedha na Mipango.

Alipomwondoa Mpango alimteua Alfayo Kidata ambaye pia alimwondoa na kumteua Charles Kichere ambaye kwa sasa ndiye CAG na nafasi yake imechukuliwa na Dk Edwin Mhede.

Licha ya mabadiliko hayo na ya maofisa wengine wa ngazi tofauti, ripoti ya CAG ya hesabu zinazoishia Juni 30, 2019 imesema mwaka 2015/16 pekee ndiyo TRA ilipita makadirio kwa asilimia 0.13.

“Kwa ujumla, mwelekeo wa makusanyo ya mapato kwa kipindi cha miaka mitano iliyopita ulikuwa chini ya makadirio yaliyoidhinishwa, isipokuwa mwaka wa fedha 2015/16 ambapo makusanyo halisi yalikuwa juu ya makadirio kwa asilimia 0.13,” imesema ripoti hiyo.

Hata hivyo, alipoulizwa juu ya suala hilo, Mkurugenzi wa Huduma na Elimu kwa mlipa kodi, Richard Kayombo alisema hawezi kuongelea suala hilo kwa sasa kutokana na ripoti kuwa imewasilishwa bungeni.

Ripoti hiyo imesema kwa mwaka wa fedha wa 2018/19 Mamlaka ya Mapato ilikusanya zaidi ya Sh15.74 trilioni dhidi ya malengo yaliyowekwa ya zaidi ya Sh18.29 trilioni.

“Hii inaonyesha makusanyo yalikuwa pungufu kwa Sh2.55 trilioni sawa na asilimia 14 ya malengo,” imesema ripoti hiyo.
Imesema jumla ya makusanyo hayo haihusishi Sh20.05 bilioni za vocha za misamaha ya kodi na fedha za marejesho ya kodi kutoka Hazina.

Kuhusu ufanisi katika ukusanyaji kodi kwa mwaka huo wa fedha, ripoti hiyo inasema haukuwa mzuri, kwani uwiano wa makusanyo ya kodi dhidi ya pato la ndani la taifa ulipungua mpaka kufikia asilimia 11.4 ikilinganishwa na asilimia 12.8 kwa mwaka 2017/18.

“Nashauri Serikali iongeze jitihada katika ukusanyaji wa mapato ili kuongeza ufanisi wa makusanyo ya kodi,” alisema CAG.

Ripoti hiyo imechanganua ukusanyaji wa kodi kwa kuangalia idara tatu zikiongozwa na idara ya Forodha na Ushuru wa bidhaa iliyoongoza kwa kukusanya asilimia 40.2 ya mapato yote; ikifuatiwa na Idara ya Walipakodi wakubwa iliyokusanya asilimia 39.8 na Idara ya Kodi za Ndani iliyokusanya asilimia 20.

“Kwa ujumla, idara zote tatu za mapato zilishindwa kufikia malengo kwa mwaka huu wa fedha 2018/19,” imeeleza ripoti.
Ripoti hiyo imetaja sababu za kutoongezeka kwa mapato kuwa pamoja na kuwapo kwa kesi za kodi za muda mrefu katika Bodi ya Rufaa za Kodi (TRAB), Baraza la Rufaa za Kodi (TRAT) na Mahakama ya Rufaa (CAT).

“Nilibaini kesi za kodi zenye jumla ya Sh 366.03 trilioni zilizokwama kwa muda mrefu katika Bodi ya Rufaa za Kodi (TRAB), Baraza la Rufaa za Kodi (TRAT) na Mahakama ya Rufaa (CAT).

Alisema miongoni mwa sababu zilizosababisha kuchelewa kumalizwa kwa kesi hizi ni pamoja na ufinyu wa bajeti unaoathiri utendaji na uendeshaji wa taasisi hizo.

Alitaja pia madeni ya kodi akisema amebaini ufuatiliaji usioridhisha wa madeni ya kodi, hivyo kusababisha kurundikana kwa madeni ya kodi kwa muda mrefu.

“Nimetathmini ufanisi na jitihada za Mamlaka katika kutatua mapingamizi ya kodi na kubaini uchelewaji katika kuyashughulikia na kuyatatua.

“Uchelewaji huu una madhara katika ukusanyaji wa mapato, kwani kodi za Serikali zinashikiliwa katika mapingamizi hayo kwa muda mrefu,” imesema ripoti hiyo.

Pia CAG ametaja upungufu wa rasilimali na wakaguzi wa kodi wenye weledi akisema kumesababisha kuahirishwa kwa baadhi ya kaguzi za kikodi kulikosababishwa na ugumu wa miamala katika taarifa za walipakodi husika, hasa katika makampuni ya kimataifa na ya mafuta.

Sababu nyingine ni udhibiti usioridhisha katika kushughulikia mizigo iliyoingia nchini kwa ajili ya matumizi ya ndani ya nchi na kwa ajili ya kusafirishwa kwenda nchi nyingine.
 
Ni kwa sababu the bar was raised higher lakini haimaanishi makusanyo hayakuongezeka ukilinganisha na miaka ya 2015 na kwenda chini.

Suala ni tungeweza kufanya bora zaidi? Jawabu ni ndio. Tungeweza kufanya mzaingira ya ukusanyaji kodi rafiki zaidi na kuengeza invesments na biashara ndogo ndogo kukuwa na kuweza kukusanya kidogo kidogo lakini kwa idadi kubwa ya walipa kodi.

Mizigo inayoingia nchini ingeongezeka na wageni kutoka nchi jirani wangeongezeka na kuinuwa uchumi na kutoa ajira katika sectors za hospitality na logistic industries.
 
Wakati huo yeye ndiye alikuwa mtendaji mkuu( commissioner general) wa TRA.
 
"Nilibaini kesi za kodi zenye jumla ya Sh 366.03 trilioni zilizokwama kwa muda mrefu katika Bodi ya Rufaa za Kodi (TRAB), Baraza la Rufaa za Kodi (TRAT) na Mahakama ya Rufaa (CAT)."

Sawa na wastani wa 18T, miaka 20 mbele hii ikoje wakuu, ama zimo na zile za Acacia?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwanini hawataji kupungua kwa TAX BASE? Biashara zikifungwa lazima kodi zipungue. Mwaka 2015/2016 nadhani ilikuwa ukusanyaji wa madeni ya nyuma ndio ilipelekea kuvuka lengo na kuanza kutumika kwa Sheria ya Usimamizi wa Kodi ya mwaka 2015 hususani kipengele cha 78 ya hiyo kodi.
 
Huyu jamaa atakuwa ametumwa na beberu kuidharirisha awamu ya malaika
 
Namba hazijawi danganya, mafail yapo hata nikipewa Mimi ofsi naweza kuiendesha, mawaziri Hawa sijui wanajificha wapi, @hkigwangala, Mpango, maana wote wametajwa sana
 
"Nilibaini kesi za kodi zenye jumla ya Sh 366.03 trilioni zilizokwama kwa muda mrefu katika Bodi ya Rufaa za Kodi (TRAB), Baraza la Rufaa za Kodi (TRAT) na Mahakama ya Rufaa (CAT)."

Sawa na wastani wa 18T, miaka 20 mbele hii ikoje wakuu, ama zimo na zile za Acacia?

Sent using Jamii Forums mobile app
Hiyo ni moja wapo ya njia ya wafanyabiashara kubuy time, anafungua kesi , anaipaki mahakamani.
 
BUSINESS DEVELOPMENT UNIT (BDU) NDANI YA TRA

KUUNGWA MKONO
Pongezi nyingi sana kwa serikali kwa mambo makubwa yanayoendelea kufanyika nchini. Hayahitaji hata kutangazwa kila mtu anaona na kusikia hata kuyagusa kwa mikono. Viva Rais John Magufuli kwa uongozi thabiti na wenye malengo. Kuna umuhimu wa watendaji kuwajibika zaidi kwa kutimiza wajibu maana tuna Rais ambaye anaweza kusikiliza, kushauri, kutoa maamuzi haraka na kusimamia mambo yakafanyika.

KUANZISHWE BUSINESS DEVELOPMENT UNIT NDANI YA TRA
Mapato ya serikali yanategemea vyanzo vile vile vya siku zote na vingine vimepungua kwasababu ya kukosekana kwa ‘dili’, upigaji haupo tena au sababu nyinginezo. Kupanua wigo wa walipa kodi (Broadening tax base) na kurefusha kina cha walipa kodi (deepening tax base) ndio njia kongwe zinakubalika katika kuongeza ukusanyasaji wa kodi. BDU kitatumia njia zote mbili ingawa kwa kiasi kubwa zote zimekuwa saturated mpaka uwe na jicho la tai.

KUTANUA WIGO WA WALIPA KODI (BROADENING TAX BASE)

Kundi la kwanza
Ni watu wanaofanya shughuli endelevu zinazoingizia mapato ya uhakika lakini hawajasajiliwa kuwa walipa kodi. Kuna kundi la kwanza ni kundi la kisekta. Kuna sekta ambazo zinafanya biashara kubwa sana lakini kwa vile traditionally zimekuwa hazilipi kodi, mambo yamekuwa yakiendelea hivyo. Hatua ya kwanza ni kuziingiza hizo sekta kwenye mfumo wa kodi. Kuna sekta kama tano hivi ambazo haziguswi kabisa na kodi lakini zina mapato kuliko hizi biashara za kawaida tulizozizoea.

Pia kuna sekta au kada maalumu hazijasajiliwa kulipa kodi . Hao watasajiliwa rasmi na TRA, zaidi ya hayo BDU itawasiliana na mamlaka husika zinazosimamia hizo kada ili waweze kupatiwa utambulisho wa kipekee (exclusive rights) kufanya shughuli hizo. Mchakato wote huo utafanywa na BDU, mteja atapatiwa vyote hivyo katika dirisha la BDU (one stop center). Hakuna gharama zaidi ya kusajiliwa na TRA ambayo ni bure, kazi yake msajiliwa itakuwa kulipa kodi tu.

Kundi la pili
Kuna watu wanaofanya biashara ambazo ni endelevu (sustainable) na zinafanya vizuri kimapato lakini kulingana na mfumo wa utendaji wa TRA ni vigumu mno kuwasajili watu hao kama walipa kodi, yaani ni ngumu kwa TRA kuwafikia. BDU itazifikia hizi biashara popote zilizopo. BDU itatoa elimu ya kodi, elimu ya kutunza kumbumbuku za biashara, umuhimu wa kulipa kodi, kisha itawasajili rasmi na kuwaingiza kwenye mfumo maalumu wa usajili. Kwa zile biashara mpya, kivutio kuingia katika mpango huu ni kuwa ukisajiliwa chini ya huu mpango, hulipi leseni ya biashara wala vikorokoro vingine vyote kwa muda wa mwaka mmoja.

Kundi la Tatu
Kusambaza vitambulisho vya ujasiliamali kila mwaka kwa wajasiliamali wapya wanaoingia katika sekta. Kila mwaka kuna fursa mpya za ujasiliamali, pia kuna wanafunzi wanaohitimu katika shule na vyuo mbalimbali. Hivyo, zoezi la utoaji wa vitambulisho litakuwa endelevu.

Kundi la Nne
BDU itahusika na mpango wa kuwa transition hawa wajasiliamali kutoka hatua ya vitambulisho vya ujasiliamali kuingia kwenye wigo wa kuanza kulipa kodi. Vitambulisho vya ujasiliamali ni daraja la kuwavusha kuingia hatua nyingine ya kutambulika rasmi. Rais alishatoa dira ni muhimu kuwe na mwendelezo wa maono ya Rais kuhakikisha kila mtanzania anapata nafasi ya kufanya ujasiliamali bila kubughudhiwa. Kivutio kuingia katika mpango huu ni kuwa ukisajiliwa chini ya huu mpango, hulipi leseni ya biashara wala vikorokoro vingine vyote kwa muda wa mwaka mmoja. Tunategemea kila mwaka 90% ya waliopata vitambulisho ya ujasiliamali wataingia kwenye lile kundi la kwanza la kulipa kodi kawaida.

Kuanzisha Mfuko wa Kukopesha kuanza biashara (Start ups)
Watu wengi wanatamani kuwa wajasiliamali lakini tatizo liko kwenye mtaji wa kuanzia. Kunaweza kuanzishwa taasisin ambayo itaweza kuwakopesha vijana waliojiunga pamoja kwa ajili ya ujasiliamali. Ulipaji wa mikopo hiyo itakuwa based on cashflows za hiyo miradi. Maturity ya mikopo itategemea pia maturity ya biashara. (hili nitalieza vizuri kwa thread inayojitegemea)

KUREFUSHA KINA CHA WALIPA KODI (DEEPENING TAX BASE)
Kuna kundi kubwa la wafanyabiashara ambao wanalipa kodi isiyo stahiki (mara nyingi wanalipa chini ya kiwango). Lakini pia kuna kupishana kwa kanuni ya ulinganifu wa mlalo (The principle of horizontal equity) hii pia inahitaji kuangaliwa (sitaweza kuongea zaidi hapa kwasababu nitakuwa naongelea utendaji wa sasa wa Mamlaka).

BDU ITAKAVYOFANYA KAZI
Kitengo hiki kipya kazi yake kubwa itakuwa kusajili vyanzo vipya vya kodi, hawa watakuwa watu wa nyanjani (field) 100%. Watu walioko ofisini kazi yao kubwa itakuwa ni kuchakata na kukadiria kodi. Kwa jinsi ilivyo sasa, Afisa wa TRA akikaa ofisini kwake yuko busy kuhudumia wateja muda wote wa kazi, ni ngumu sana kupata wasaa wa kufikiria vyanzo vipya vya kodi au kwenda nyanjani kutembelea wateja ispokuwa kwa suala maalumu, muda mwingi wametingwa na paper trails kuanzia maafisa mpaka viongozi wa ngazi za juu.

Ni sawa na nurse au tabibu hana muda wa kufikiria juu ya njia mpya za kimatibabu yeye yupo busy kutibu tu. Lakini hata katika viwanda kuna vitengo vya utafiti na maendeleo (Research and Development) vinavyofikiri juu ya ubunifu wa huduma mpya.

Kitengo hiki kitafanya kazi kwa matokeo (results based). Mfano, wilaya ya Ilala yenye kata around 23 kuanzia 1st July 2020 hadi 30th June 2021 inatakiwa kusajili walipa kodi wapya 2,000 ambao kwa wastani kila mlipa kodi alipe Tsh 1,200,000 kwa mwaka, mapato yatapatikana Tsh 2.4b. Gharama za uendeshaji za juu kabisa (42%) inaweza kuwa Tsh 1,008,000,000, hivyo serikali kubakia na Tsh 1,392,000,000. Hapa inaweza kuwa kwa wafanyabiashara wale ambao tayari wanafanya kazi au kwa wale ambao wanaanza biashara (start ups).

Hapa nimetolea mfano kwa wilaya moja tu, unaweza kuona kama utaratibu huu ukifanywa kwa nchi nzima. Tunaweza kuanza kwa majaribio mikoa michache tutahitaji serikali iikopeshe BDU kwa ajili ya bajeti ya kuanzia lakini baadaye BDU itailipa serikali. Hiki kitengo kitajitegemea kwa kila kitu kwa maana ya gharama zake zote sio kutegemea ruzuku.

Serikali inahitaji watu wenye the right attitude na skills kufanya haya, watu wanaotazama mambo kwa jicho la pili. Na uzuri watu hao tupo na pacesetter (Rais John Magufuli) yupo, hakuna kinachoshindikana ni kubadilika.

tunatekeleza@gmail.com
 
Ukweli utatuweka huru jamani ivi ninyi mnaishi dunia gani? Ivi mnafikiri mnapopita mitaani flame nyingi zimefungwa mnadhani wenye nazo wamefata bidhaa? Walishafilisika wengi walienda mikoani na wa mikoani wengi walikimbilia vijijini kwahiyo mnataka TRA kodi wakusanye kwa nani?
Lazima tuangalie vizuri sharia zetu sio rafiki na wafanya na walipa kodi,lakini pia wenye mamlaka wanatisha walipakodi bad ala kuwasaidia,kuwaelekeza nk.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
hahah kumbe zile report za kuvuka malengo zilikua zinapikwa ?

Katika mwaka kuna miezi 12, na sio miezi yote hiyo TRA wanavuka malengo. Kuna miezi ya peak kwa RTD na CUSTOMS pia kwa DRD ila naona DRD bado ufanisi zi mzuri sana maana asilimia 20 tu bado waongeze nguvu biashara nyingi hasa wilaya za mikoa tofauti na miji mikubwa watu hawatumii EFD.
 
Back
Top Bottom