Kichaa cha mbwa hakitibiwi kwa jadi

JanguKamaJangu

JF-Expert Member
Feb 7, 2022
2,308
5,460
IMG-20220928-WA0090.jpg
JAMII imeaswa kwenda kupata huduma za tiba ya kichaa cha mbwa kwenye vituo vya kutolea huduma za Afya badala ya kwenda kwa waganga wa jadi, hali inayoweza kusababisha vifo visivyokuwa vya lazima.

Hayo yamebainishwa na Ofisa mifugo kata ya Sofu,Grory Amos,wakati akitoa elimu ya umuhimu wa chanjo ya mbwa kwa wakazi wa kata hiyo,huku akiwaonya kutokimbilia kwa waganga wa jadi kupata tiba ya kichaa cha mbwa.

Amedai kuwa kichaa cha mbwa hakina tiba na kwamba wanachokifanya ni kutoa chanjo ili kuwakinga na virusi vinavyosababisha ugonjwa huo hatari kwa jamii.

Sambamba na hilo amedai kwamba mtu anapoambukizwa ugonjwa wa kichaa cha mbwa hupaswa kupata tiba sahihi kwa kipindi cha miezi mitatu mfululizo.

"Ninapenda kuiasa jamii kutambua kuwa kichaa cha mbwa hakitibiwi kwa waganga wa jadi...ili mtu aliyeambukizwa aweze kupona anapaswa kuwahi kwenye Zahanati,kituo cha afya au hospitali zinazotambuliwa na serikali"amesema Amos.

Kwa upande wake Ofisa mtendaji wa mtaa wa sofu,Debora John,amesema ili kukabiliana na ugonjwa wa kichaa cha mbwa,jamii inapaswa kuendelea kupata elimu sahihi ya ufugaji wa mbwa badala ya kuendelea kufuga kwa mazoea.

Aidha amewataka wananchi kutoa taarifa haraka kwa viongozi wa mitaa na kata iwapo wataona mbwa mwenye dalili za ugonjwa wa kichaa cha mbwa kwa lengo la kunusuru jamii kukumbwa na maradhi hayo.

Naye Ofisa maendeleo ya jamii kata hiyo,Lilian Wilfred,ametumia fursa hiyo kuwaonya wananchi wote wanaofuga mbwa pasipo kuzingatia sheria,taratibu na kanuni za ufugaji na kwamba iwapo ikithibitika mbwa mwenye ugonjwa huo kusababisha madhara kwa jamii hatua za kisheria zitachukuliwa dhidi yake.

Septemba 28, 2022 ikiwa ni maadhimisho ya siku ya kichaa cha mbwa duniani, halmashauri ya Mji Kibaha yenye Mitaa 73 na Kata 14 inakadiriwa kuwa na Mbwa 3114 na Paka 930.

Chanzo: Torchmedia




=====================

UGOJWA WA KICHAA CHA MBWA NI NINI?

Ugonjwa hatari unaoenea toka kwa wanyama kwenda kwa binadamu (zoonotic disease)

husababishwa na virusi aina ya RNA kundi la Lyssavirus, familia ya Rhabdoviridae.

Kifo ni 100% kama mtu aliyeumwa na mbwa hatapatiwa tiba kinga


JINSI UGONJWA WA KICHAA CHA MBWA UNAVYOENEA

KWA TANZANIA MBWA NDIYE MWENEZAJI MKUU WA UGONJWA HUU KWA BINADAMU NA KWA WANYAMA WENGINE KAMA NG’OMBE NK

JINSI UGONJWA WA KICHAA CHA MBWA UNAVYOENEA

KATIKA MATUKIO MACHACHE KICHAA CHA MBWA HUWEZA KUENEA KWA:

Njia ya hewa (Aerosolized virus)

Kwa njia ya kupandikizwa kiungo cha mwili (Transplantation of tissue) kama figo toka kwa mtu mwenye maambukizi ya ugojwa wa kichaa cha mbwa

(TANZANIA HAIJAWAHI KUTOLEWA TAARIFA)

MUDA WA DALILI KUJITOKEZA(INCUBATION PERIOD)
Siku 10 mpaka mwaka mmoja( Wastani ni mwezi 1 hadi 2.

Hii hutegemeana na:

Idadi ya virusi vilivyoingizwa mwilini

Ukubwa wa eneo la mwili lililotafunwa

Kinga binafsi ya mtu mwilini

Aina ya kirusi kilichoingizwa mwilini

Umbali wa jereha kutoka kwenye mfumo wa fahamu

DALILI ZA UGONJWA WA KICHA CHA MBWA

UGONJWA WA KICHAA CHA MBWA HUJITOKEZA KWA NAMNA MBILI ZIFUATAZO:

Kupooza mwili (Paralytic rabies)

2.Kichaa moto (Furious rabies)



Hatua zote hizi mbili hutanguliwa na dalili zifuatazo:

Homa,kuumwa kichwa,mwili kuchoka,

kichefuchefu,kutapika, kuwashwa sehemu mtu alipoumwa na mbwa,

kuwashwa na koo na kuwa

kikohozi kisichotoa makohozi baada ya tukio la kutafunwa na mbwa

KICHAA BARIDI( PARALYITC RABIES)

DALILI ZAKE:
Kuuma kwa misuli ya mwili

Kupumua kwa tabu

Kupooza kwa misuli ya mwili hususani miguu na mikono

Kifo



KICHAA MOTO(FURIOUS RABIES)

DALILI ZAKE:

Kukakamaa misuli

Kushituka shituka

Kuhema kwa tabu

Kuogopa maji, upepo na mwangaza

Kuchanganyikiwa au kurukwa akili

Kifo

NAMNA 3 ZA MTU KUPATA MAAMBUKIZI YA KICHAA CHA MBWA (TYPE OF CONTACT EXPOSURE)

Kuguswa au kulabwa kwenye ngozi isiyokuwa na michubuko (Touching or feeding of animals/licks on intact skin)

Jeraha lisilotoa damu (Minor scratches or abrasions without bleeding)

Jeraha linalotoa damu (single or multiple transdermal bites


HUDUMA YA KWANZA KWA MTU ALIYEUMWA NA MBWA

Osha jeraha kwa maji mengi yanayotiririka na sabuni

Osha kwa maziwa au kimiminika chochote kama maji hayapatikani

Safisha jeraha kutumia antiseptic (k.m. dettol, spirit n.k)

Wahi kituo cha Afya kupewa TT na tiba kinga(chanjo) ya kichaa cha mbwa


TIBA KINGA (CHANJO) YA KICHAA CHA MBWA

Hutolewa kwa njia kuu mbili (2)

Njia ya misuli (Intra-muscular, IM)

Njia ya ngozi(intra-dermal, ID

Njia ya ngozi(ID) inapendekezwa itumike badala ya njia ya misuli(IM) kwa sababu:

Humpunguzia mwathirika muda wa kuhudhuria kituo cha tiba kupata chanjo

Gharama yake ni ndogo (chupa 1 vs 5)

Humjengea mtu kinga ndani ya siku (7) saba

UTOAJI WA KINGA(CHANJO) YA KICHAA CHA MBWA KWA BINADAMU

Njia ya misuli(IM) haipendekezwi kwa sababu zifuatazo

Ni njia ya gharama sana

Mteja hupaswa kuhudhuria kituo cha tiba mara tano

Humjengea mtu kinga baada ya siku 14


UTARATIBU WA UTOAJI WA CHANJO YA KICHAA CHA MBWA

NJIA YA MISULI(IM) 1mlx5=5vials SIKU 0, 3, 7, 14 na 28

NJIA YA NGOZI(ID) 0.2mlx4=0.8ml SIKU 0, 3 , 7 na 28

NB: Serum(RIG) hutolewa siku 0(40IU per Kg body-weight kwa jeraha linalotoa damu tu.

Mtu aliyepata chanjo mwaka mmoja nyuma na akaumwa tena na mbwa, apewe SIKU 0 na 3
KINGA KWA MTU ALIYEUMWA NA MBWA ANAYEHISIWA KUWA NA KICHAA



JERAHA LA MTU ALIYEUMWA NA MBWA ANAYEHISIWA KUWA NA KICHAA HALISHONWI, kama kushona ni lazima ifanyike baada ya muathirika kupatiwa serum(RIG)

Muathirika apatiwe Antibiotic na sindano ya Pepopunda (T.T) kumkinga na pepopunda na magonjwa nyemelezi


CHANJO KWA MAKUNDI MAALAMU
Wataalamu wa mifugo wanaoshiriki kampeni ya uchanjaji wa mbwa

Waokotaji wa mizoga ya mbwa waliogongwa na magari

Wataalamu wa maabara wanaofanya uchunguzi wa wanyama wanaohisiwa kuwa na kichaa SIKU 0, 7 na siku ya 21 au 28


MBINU ZA KUDHIBITI KICHAA CHA MBWA
Kuchanja mbwa na paka kila mwaka kwa zaidi ya asilimia 70 katika kila eneo lenye mbwa/paka

Kudhibiti idadi ya mbwa kwenye kaya kulingana na uwezo wa kuwahudumia

Kudhibiti mbwa wazururaji

UFUATILIAJI WA UGONJWA WA KICHAA CHA MBWA/ KUNG’ATWA NA MBWA
Ufuatiliaji wa wagojwa waliong’atwa na mbwa anaesadikiwa kuwa na kicha hutolewa taarifa kila wiki & mwezi kwa mfumo wa IDSR (IDWE, Monthly) Ngazi ya Wizara ya Afya, Maendereo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto
 
Back
Top Bottom