Tena nahisi kwa mtu aliye makini, kibwagizo hicho ni tusi kwake! Ni tusi kwake kv mtu yeyote kupandikizwa kitu ambacho si sahii na kumtaka akiamini tafsiri yake ni kwamba umemuona juha! Kama unamshawishi mtu aamini kwamba 3x3=6 basi bila shaka ushamuona huyo mtu hajui A wala B ktk hisabati!
Wakati Kikwete akizungumzia suala zima la TUCTA (au wafanyakazi?) kutaka kima cha chini cha mshahara kiwe Shs. 350,000/= (kwa tija ipi? Yaani Walimu kama waliokuwa wamecharazwa bakora na DC Mtimuliwa, Bwana Mnaly wale wapate zaidi ya Sh. Laki 4! ) alitamka bayana kwamba kima hicho hakilipiki! Alidai kwamba makusanyo ya serikali ni kiasi cha Shilingi Trilioni 5 kwa mwaka na endapo kima cha chini cha mshahara kitakuwa Shs.350,000/= basi bajeti ya mishahara peke yake itakuwa kiasi cha Shs. Trilioni 6 kwa mwaka! Kwa maana nyingine, endapo kima hicho kitalipwa, basi shughuli zingine zote za serikali (in partcular, kutoa huduma kwa wananchi wake zisimame!) Hivyo, bila kutafuna maneno, JK akazungumza wazi kwamba kima hicho hakilipiki, na endapo hilo ndilo sharti la kupigiwa kura na wafanyakazi(au Bwana Mgaya!?) basi ni heri msinipigie! Ilikuwa ni kauli ya kijasiri, ambayo naamini inaweza kuungwa mkono hata na wanasiasa wa upinzani wasiotaka kubisha kila jambo kama alivyo Mheshimiwa Zitto! Mwanasiasa yeyote ambae anasimama kwenye ukweli bila kutishika na shinikizo za kisiasa; angesema hivyohivyo!
Kikwete anazihitaji kura za wafanyakazi, lakini kama sharti lenyewe ni kupewa kima cha chini cha Shs.350,000/= ndipo wawezwe kumpigia kura; basi yu heri kuzikosa kura hizo kuliko kuahidi kitu kisichotekelezeka! Hata Dr. Slaa mwenyewe ambae anaichukulia kauli hiyo ya Kikwete kama mtaji mpya wa kisiasa, anafahamu wazi kwamba kima hicho hakilipiki!
Hivyo basi, tuache porojo za kisiasa! Sipendi kufanywa sina akili! Chama chochote kile kinachoamini kinaweza kulipa kiasi hicho, basi naomba kiweke wazi mambo yafuatayo:
· Vyanzo vya Mapato na Thamani Zake: Msiishie tu kusema kwamba mtabuni vyanzo vingine vya mapato, bali ningependa kuorodheshewa vyanzo hivyo na bajeti ya mapato yatakayopatikana kutoka kwenye vyanzo husika. Iwe ni Scientific Budget na sio Political Budget!
· MIANYA YA UFISADI NA POSHO: Tunaambiwa kwamba serikali inashindwa kulipa kima cha Shs. 350,000/= kv serikali yenyewe imejaa ufisadi! Ndio, hilo halina mjadala kwamba ufisadi umeenea katika kila nyanja! Hivyo basi, ningependa kupatiwa mchanganuo mzima wa kiasi cha pesa kinachopotea kwenye ufisadi na posho kwa mwaka mzima ili nione endapo upotevu huo usingekuwepo basi Tatu Unusu ingelipika! Si hivyo tu, mimi ni mtu ninayeaamini kwamba Watanzania (including na waliomo kwenye uongozi wa upinzani) hatuna uaminifu kabisa! Ni Watanzania wachache sana ambao wapo honest. Hivyo basi, lazima niambiwe namna ambavyo mtazuia ufisadi huo na sio tu kusema kwamba mtakomesha ufisadi!
· MISAMAHA + MIANYA YA UKWEPAJI KODI: Hamna anayekataa kwamba bado kuna ukwepaji mkubwa wa kodi nchini. Aidha, kuna misamaha mingi ambayo haina ulazima. Hata hivyo, ningependa takwimu ili nijue ni kiasi gani kinakosekana kutokana na ukwepaji kodi. This, Must be Scientific Statistics and not Political Statistics. Aidha, niorodheshewe misamaha ambayo haikustahili kupata msamaha pamoja na thamani yake.
· MATUMIZI MABAYA YA SERIKALI: Eneo lingine linalolalamikiwa ni la matumizi mabaya ya serikali. Hapa ningependa kuorodheshewa matumizi yote yanayoonekana ni mabaya ya seriakali na thamani yake. Ni matumizi ambayo nyie mkiingia tu, mtayafuta mara moja!
NDIYO!! Nataka mambo na michanganuo lakini endapo michanganuo hiyo hamna basi mnatuongopea! Inawezekana kabisa kwamba endapo baadhi ya mambo yatafanyika basi kima hicho kinalipika. Hayo mambo ndiyo ninayoomba mtuambie at least wana wa JF! Hofu yangu ni kwamba, inawezekana kabisa kwamba pamoja na kelele za kwamba kima cha 3 unusu kinalipa kumbe hata nanyi uwezo huo hamna kv hamna vyanzo mbadala!
Hamna vyanzo mbadala kutokana na mambo yafuatayo:
· Ufisadi ndani ya nchi hii unafanywa tangu ofisi ya mtaa hadi Ikulu! Huko kote kuna wapenzi na wanachama wa vyama vya upinzani na si ajabu hata hao wanaofanya ufisadi kwenye idara na wizara za serikali wengine ni wanachama wa vyama vya upinzani! UFISADI HAUNA CHAMA WALA KABILA! This is all about inner most attitude ambayo no one political part with members with equal attitudes!
· Wataalamu ambao kwa sasa ndio wanaoibua vyanzo vya mapato wengine ni wapenzi na wanachama wa vyama vya upinzani. Kwanini basi wasiviibue sasa?! Je, ina maana vyanzo hivyo ambavyo hadi leo havipo vinasubiri upinzani kwanza uingie madarakani ndipo waviibue vyanzo hivyo?
Endapo majibu ya maswali yangu hamna mwenye nayo, basi shime kwa upinzani kutuhubiria sera zinazotekelezeka! Itakuwa ni kuwatusi Watanzania endapo mtu anayegombea Urais atasimama mbele ya wananchi na kuahidi kwamba nipeni kura nitawalipa Shs.350,000/= wakati anajua kwamba uwezo huo hana! Hatutaki porojo za akina Cheyo alipokuwa ametuahidi kutujaza mapesa watanzania wakati ameshindwa kuwajaza mapesa hata Wasukuma wenzake waliopo kwenye jimbo analoliwakilisha!