Ni kawaida kwa mwanaume aliyekamilika kula vibuti. Vibuti vina staili tofauti, kuna kumwagwa na kumiminwa. Kibuti sitakaa nikisahau, kwani nilipopewa haya maneno, sikuwa na moyo wa kuendelea, licha ya kumfatilia kwa miaka 5, namnukuu "unajua dunia hii unaweza ukampenda sana mtu kama mpenzi, naye akakupenda kama rafiki? Tindikali kaa ukijua kuna watu waliwapenda sana, wakafiwa na wake zao, lakini walikuja kuoa tena na maisha yakaendelea, sembuse mimi usiyejua matamu na machungu yangu? Na isitoshe dini itakusumbu, naomba tubaki tu kama marafiki.....", nilimpenda sana huyu binti na bado nampenda, lakini cha kusikitisha alinipenda kama rafiki. Je wewe una uzoefu gani na vibuti?