kwakweli binafsi kibuti ambacho sitakisahau nilipewa juzi juzi tu hapa yaan miaka kama miwili iliyo pita, inshort nilikuwa na mpnzi ambaye tulikuwa pamoja kwa kipindi cha miaka mitatu mfulilizo. mwaka wa tatu karibu na anniversary yetu ndipo alipoanza kubadilika maana tulikuwa wote ni madent wa chuo lakin tukiwa vyuo mbalimbali, kitu kilichofanya nihsi mabadiliko yake ilikuwa ni kukosa kwa hamasa juu ya siku hii ambayo miaka ya nyuma ilikuwa na hamasa sana kwake. mpaka anniversary inaisha kwakweli hali haikuwa nzuri lakin kijana nilijaribu kumvumilia tu nikiamin may b n just misukosuko ya mapenzi ya kawaida kama wapenzi wengine. lakini siku moja nikiwa nasubiri kuingia lecture simu ngeni ilipiga na nilipopokea sauti moja ya kiume ilisikika na alichosema kijana huyu ni kwamba niache kumsumbua girl friend wake na anaomba niachane naye kwani muda wangu wa kuwa naye umefika ukomo. nilijikaza nikaongea na huyu dogo mpaka mwisho, nikasema siwezi gombana na mwanaume mwenzagu kisa demu, nikasema itabidi nimwulize mhusika ili anijuze vizuri. basi baada ya lecture nilimpigia huyu mpenzi wangu na nilipomuuliza kwanza alikataa na nilipombana alikili kuwa na uhusiano na mtu huyu. nilimmind na kukata simu. siku ya pili alipiga na nilipomwuliza kwann alifanya hivyo na nn msimamo wake. alinjb kuwa ilikuwa bahati mbaya lakin asingeweza kuachana na huyo bwana kwan angemwumiza sana na hakupenda kufanya hivyo na hivyo indirect alitangaza kuachana na mimi rasmi. hk ndo kibuti ambacho sitakisahau.