Kibiti: Polisi yaua watu wanne(4) wanaodhaniwa kujihusisha na mauaji wilayani humo

Mtu akimbilie kichakani alafu wewe umfuate kichakani/ubaki barabarani alafu wewe ndio umue kwa risasi mtu aliejificha kichakani tena bila wewe kudhurika huku ikiwa ni mida usiku!!!!

Au waliwau wakati wanakimbilia kichakani?Inawezekana kweli katika mazingira ya giza?!

kama waliwau wakati wanakimbilia kichakani,ndio kuwe na mapambano ya muda wa zaidi ya nusa saa?

Kama ni kweli, basi hao labda ni vibaka lakini sio hawa jamaa wanaouwaa kwa style hii tunayoisikia.
Nimeshangaa polisi kubaki barabarani ila wakafanikiwa kuwauwa walioko vichakani bila ya wao kudhulika tena usiku itakuwa hao wanaozaniwa nimajambazi walikuwa wamevaa refrecta au kama sivyo labada izo wanazo ita SMG zinawaka usiku au walikuwa na tochi. bado nashangaa hao majambazi naoskiaga kwa umahili wakulenga, kuuwawa kiboya kiasi hicho.
 
Polisi na baadhi ya watu waliouwawa, baadhi yao picha zilionyeshwa. Kwa nini polisi wasituonyeshe picha za hao majsmbazi wanne ambao wanewaua?
 
Kama habari hii ni kweli lipo tatizo

Kudhania tu hakumfanyi mtu kuwa na hatia na adhabu!
Mkuu kama walikuwa na silaha na walivyoona gari la polisi wakakimbia kichakani na kuanza kuwarushia polisi risasi mpaka hapo inaonesha hawakuwa RAIA wema hata kama hakuna uthibitisho kama wao ni miongoni mwa wanaoendesha mauaji ya kibiti hivyo polisi walichukua uamuzi sahihi wa kujibu mapigo
 
Kama habari hii ni kweli lipo tatizo

Kudhania tu hakumfanyi mtu kuwa na hatia na adhabu!
Wadhaniwa acheni wauawe na wanaodhani kwani inaonekana kudhani na kuua ndio njia pekee ya kukomesha mauaji ya kinyama yanayofanyika Pwani. Inatutosha kujua kusoma na kuandika si weledi katika shughuli zetu.
 
Kama walikua wanarusha risasi ulitegemea wawakamateje
labda angekuwa yeye angewaambia ninyi ninyi acheni basi kurusha risasi. Na polisi hawawezi kusema moja kwa moja kuwa hao ni wauaji, ni lazima uchunguzi ufanyike (they have to prove beyond reasonable doubt)
 
najitahidi kuwa positive na hii habari, isijekuwa wameua watu sio na kuadress ndio ili wasionekane wamewashindwa
kama ni kweli inaleta tumaini kwamba adui anawezekana nilihisi hata wanatumia nguvu za giza
ila muhimu tujue watu hao waliouliwa ni kina nani, wenyeji wa wapi, umri etc inaweza kutupa picha kamili ya adui ni nani
Very true. Hiyo pia itaondoa sintofahamu kwamba walikuwa raia wa kawaida au la!
 
Kuna siku hao mapolisi watakuja wauwane wao kwa wao huku kila mmoja akiwa ana mdhania mwenzake ni jambazi
 
Hizo porojo na ni mapicha kama ya kova..kuna jambazi anayetembea mchana.mxxxx ..sabas anaongea huku anatetemeka maana anajua ni uongo mtupu anaufanya
 
Nimeshangaa polisi kubaki barabarani ila wakafanikiwa kuwauwa walioko vichakani bila ya wao kudhulika tena usiku itakuwa hao wanaozaniwa nimajambazi walikuwa wamevaa refrecta au kama sivyo labada izo wanazo ita SMG zinawaka usiku au walikuwa na tochi. bado nashangaa hao majambazi naoskiaga kwa umahili wakulenga, kuuwawa kiboya kiasi hicho.
Mkuu ujue polisi wa Tanzania ndiyo wanaongoza kwa maigizo Duniani yaani wamekamata watu wamewapeleka Vichakani wakiwa hai badala ya kuwahoji wameamua kuwaua ili kuwahadaa watanzania wawaone kuwa wanafanya kazi kubwa, ni Aibu kubwa kuua pasipo kumdaka jambazi akiwa hai waache kuwadharau watanzania kwa kuwaona ni wajinga hawajui kutafakari tukio.
 
Siku akitandikwa baba au mama yako risasi ya kichwa na kupasuliwa ubongo ndio utajua ni wahalifu u majambazi na ndio utaamini
Mambo ya baba na mama yameingiaje huku,..tuheshimiane mkuu..when your parents are mentioned in such kind of mess what will be your reaction??never downgrade people who you only see in social media...
 
labda angekuwa yeye angewaambia ninyi ninyi acheni basi kurusha risasi. Na polisi hawawezi kusema moja kwa moja kuwa hao ni wauaji, ni lazima uchunguzi ufanyike (they have to prove beyond reasonable doubt)
Nni kweli lazima uchaguzi wa kiina ufanyike ndipo Ukweli ujulikane
 
  • Thanks
Reactions: cdc
Wana uhakika? Isije ikiwa ni raia wema. Vinginevyo Good work
watu sita wakakimbilia porini walipoona gari la polisi, majibizano ya risasi na hao watu yamedumu kwa takribani nusu saa, sasa hao watakuwa raia wema kweli?
 
Kwan polisi hawana smg? wametoa ofisin wakawaonesha kwamba wamekamata.. Tanua uwezo wa kufikiri nje ya box ndugu
Kwa iyo we umetanua uwezo wa kufikir umeishia hapo, ulikwepo wakat wanafany ivo!?
Mmmh! "Kikundi cha watu sita wote kwa pamoja kushambulia polisi alafu wa 4 wakauwawa lakini silaha zilizo kutwa ni 2!!!!!!!!!!!!!!!!!!!

Jeshi la Polisi nchini limefanikiwa kuwaua wahalifu wanne wanaosadikiwa kuwa miongoni mwa wahalifu wanaoendesha mauaji katika wilaya za Mkuranga, Kibiti na Rufiji katika mapambano yaliyodumu kwa zaidi ya nusu saa katika kijiji cha Pagae wilayani Kibiti mkoani Pwani.

Akielezea tukio hilo Mkuu wa Oparesheni Maalumu za Jeshi la Polisi, Naibu Kamishna wa Polisi Liberatus Sabas alisema tukio hilo lilitokea siku ya Alhamisi juni 29 majira ya saa tatu usiku kwenye barabara ya vumbi itokayo Pagae kuelekea Nyambunda ambapo Askari Polisi wakiwa doria walikutana na kikundi cha watu kinachokadiriwa kuwa na watu sita ambapo wahalifu hao baada ya kuona gari la Polisi walikimbilia vichakani na kuanza kuwarushia risasi Polisi.

Sabas alisema baada ya hali hiyo kutokea Askari nao kwa ujasiri walijibu na mapambano hayo yalidumu kwa zaidi ya nusu saa ambapo Polisi walifanikiwa kuwajeruhi wahalifu wanne kwa risasi ambao baadaye walifariki dunia wakiwa wanapelekwa hospitali.

"Katika tukio hilo tumefanikiwa kupata silaha mbili aina ya SMG na magazine mbili pamoja na risasi 17 zilizokuwa zinatumiwa na wahalifu hao na hii ni dalili kuwa tunaendelea vizuri na oparesheni yetu ambayo inashirikisha vyombo vingine vya ulinzi na Usalama katika wilaya hizi tatu za Mkuranga, Kibiti, na Rufiji" Alisema Sabas.

Aidha Sabas ametoa wito kwa wahalifu wengine kuacha mara moja kufanya vitendo hivyo kwa kuwa vyombo vya ulinzi na usalama vinaendelea kufanya jitihada zote za kuhakikisha kuwa maeneo hayo yanakuwa salama na wananchi wanaishi katika hali ya amani na usalama.

Vilevile amewataka wananchi kutoa taarifa zitakazowezesha kupatikana wahalifu wengine ili kuhakikisha kuwa kila mmoja anaishi kwa usalama ambapo kwa ambaye atakayetoa taarifa zitakazowezesha kupatikana kwa wahalifu hao kiasi cha shilingi milioni kumi kitatolewa na Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Simon Sirro.


Chanzo: ITV
 
Back
Top Bottom