Tabora: Mwanamke auawa, chanzo wivu wa mapenzi

Muuza Kangala

JF-Expert Member
Jul 21, 2021
1,238
4,807
Jeshi la Polisi linamshikilia mwanamume kwa tuhuma za kumuua kwa kumnyonga mkazi wa Mtaa wa Maselele, Kata ya Cheyo B Manispaa ya Tabora, Juliana Mbogo (40) kisha mwili wake kuuficha uvunguni mwa kitanda, chanzo kikidaiwa ni wivu wa mapenzi.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tabora, Richard Abwao amesema hayo leo Jumatato, Agosti 14, 2024 na kuongeza kuwa, mtuhumiwa huyo ambaye jina lake limehifadhiwa alitenda tukio hilo nyumbani kwa mwanamke huyo.

"Ni kweli tunamshikilia mtu mmoja kwa tuhuma za kumuua kwa kumnyonga Juliana Mbogo, imeelezwa alimnyonga kwa kamba ya filimbi kisha mwili wake kuuweka chini ya uvungu wa kitanda alichokuwa akilala," amesema.

"Mtuhumiwa alikuwa na uhusiano na Juliana lakini baadaye ukayumba, ndipo akaamua kuja nyumbani kwa Juliana na kumlaghai mtoto wake wa miaka 10 akalale sebuleni, baada ya mtoto kwenda kulala ndipo mtuhumiwa akatekeleza unyama huo.”

Amesema uchunguzi wa kisayansi unaendelea na ukikamilika mtuhumiwa atafikishwa mahakamani kwa tuhuma zinazomkabili za mauaji.

Soma Pia:
Jirani wa marehemu, Elisha Kumbangwa amesema taarifa za kifo cha Juliana alizipata kutoka kwa mtoto wa kwanza wa marehemu mwenye miaka 10.

“Mtoto wa marehemu ametuambia Jumamosi jioni alikuja mtu nyumbani kwao akiwa na mkoba mweusi akajitambulisha kwake kuwa ni mjomba, baada ya hapo mama yake alimkaribisha ndani na ulipofika muda wa kulala, mtoto huyo akaenda kulala akamwacha mama yake na huyo uncle wamekaa sebuleni," amesema Kumbangwa.

Hata hivyo, amesema mtoto huyo aliwaambia ilipofika asubuhi, aliingia chumbani kwa mama yake kuchukua nguo za kuvaa aende kanisani, na alipoingia hakumuona, akaanza kumuita lakini ghafla akatokea mtu akiwa amejifunga kitambaa usoni.
Snapinsta.app_455195413_1545026136095534_1617639928301498066_n_1080.jpg
 
Hakuna kiumbe chenye ndevu kikaitwa mrembo duniani,huyo hana tofauti na mwanaume na mwanaume asili yake inamkataza kuitwa mrembo.

Kama mwanamke ana ndevu ni sharti muda wote azinyoe zisionekane unless atakuwa mchafu
hakuna matibabu ya kuondoa ndevu zisirudi? maana ni suala la kihomonia..najiuliza madaktari hawatibu likapotea mazima
 
Back
Top Bottom