Nimefika kwa ndugu kama ugenini kanipokea vyema, nikaishi hapo siku za mwanzo na kawaida limoti ya tv ilikuwa ipo hapo sebuleni kwenye kabati, cha kushangaza baada ya kama wiki ile limoti ilihamishwa makao ikawa inakaa chumbani kwa kaka. Sasa sijui tatizo ni nn
Hakuna tatizo, ni kwamba unaambiwa kwa matendo kwamba umekaa vya kutosha, rudi ulikotokea! Tujikumbushe hapa:
--Mgeni siku ya kwanza mpe mchele na panza, mtilie kifuuni mkaribishe mgeni.
--Mgeni siku ya pili mpe maziwa na samli, mali yakikuzidia mzidishie mgeni
--Mgeni siku ya tatu nyumbani hamkuna kitu, kuna vibaba vitatu pika ule na mgeni.
--Mgeni siku ya nne mpe jembe akalime akirudi muagane, msindikize mgeni.
--Jazia mwenyewe...
--Hapa pia fill the blanks
--Hapa pia
--Kisha fahamu wajibu wako siku ya 8
--Mgeni siku ya kenda, enenda bwana enenda, usirudi nyuma tena; usirudi mgeni
--Mgeni siku ya kumi kwa mateke na mangumi, mfukuze mgeni.
Naona unasubiri kwanza mangumi.....hivi hufahamu kwamba bei ya umeme na mafuta soko la dunia imepanda? Kutaka kutuharibia rimoti yetu hapa!!