Kibatala: Waliokamatwa kwa maagizo ya Gambo wafungue case ya Unlawful Imprisonment

OKW BOBAN SUNZU

Platinum Member
Aug 24, 2011
52,013
114,357
"Mstahiki Mayor wa Arusha, Kalisti Lazaro, Madiwani, Viongozi wa Dini, Waandishi wa habari, wazazi mliokamatwa na Polisi (ambao kama walinukuliwa sahihi basi waliagizwa na ndugu Mkuu wa Mkoa Arusha);

NITAWASHANGAA SANA kama hamtafungua na kufuatilia case ya Unlawful Imprisonment dhidi ya kukamatwa kwenu (na kupewa lift bila hiari) na kudai fidia.

Mbona Arusha mna Wakili wengi tu?"

Haya ni maneno ya wakili msomi Peter Kibatala
Kibatala ametaja mawakili wasomi wanaoweza kusaidia hili
John Mallya, Sheck Mfinanga, Faraji Mangula
 
Gambo atamfungia kibatara asikanyage Arusha kwa kufanya uchochezi kati ya waandishi wa habar na polisi
 
Namuunga mkono Wakili Kibatala asilimia mia kwa mia. Hii tabia ya viongozi kuamua kutumia mabavu kuwadhalilisha watu kwa masuala yasyohusiana na uvunjifu wa sheria yanatakiwa yakomeshwe. Njia kuu ni kutumia sheria ili ujinga huu usiendelee.
 
da hebu waanze kupunguzwa wendawazim mtu unateuliwa unakuwa mungu na kile kijamaa tulikichaguwa wenyewe kwa kutubembeleza leo kiburiiiiiii :(
 
Niko tayari kuchangia pesa taslimu ili kusaidia kuharakisha mchakato huo , hii kesi itasaidia kuweka mwongozo wa namna hawa viongozi wadogowadogo wa kuteuliwa baada ya kuhurumiwa , kuiheshimu katiba ya nchi .

Napendekeza kesi ifunguliwe Jumatatu saa 2 asubuhi .
 
si nasikia mkuu wa mkoa uwezo kisheria wa kukuweka ndani masaa 48 bila maelezo yyte au ilishafutwa hii

Sio bila maelezo yoyote, bali tu pale inaposadikika kwamba usalama wako, au usalama wa raia wengine unaweza kuwa mashakani. Watanzania tunahitaji sana kujua Katiba yetu hasa haki za msingi za raia
 
"Mstahiki Mayor wa Arusha, Kalisti Lazaro, Madiwani, Viongozi wa Dini, Waandishi wa habari, wazazi mliokamatwa na Polisi (ambao kama walinukuliwa sahihi basi waliagizwa na ndugu Mkuu wa Mkoa Arusha);

NITAWASHANGAA SANA kama hamtafungua na kufuatilia case ya Unlawful Imprisonment dhidi ya kukamatwa kwenu (na kupewa lift bila hiari) na kudai fidia.

Mbona Arusha mna Wakili wengi tu?"

Haya ni maneno ya wakili msomi Peter Kibatala
Kibatala ametaja mawakili wasomi wanaoweza kusaidia hili
John Mallya, Sheck Mfinanga, Faraji Mangula
Kweli cdm tuna wanachama wanaojielewa sana
 
Tatizo hapo atashitakiwa kama RC na wakisihinda faini italipwa na ofisi ya mkuu wa mkoa.

Hii ni moja ya sababu iliyowahi kunifanya nilete mada hii hapa chini ambayo nadhani haikueleweka.

Tubadili sheria anaetumia madaraka vibaya na kusabibisha serikali kudaiwa fidia awajibeke kulipa
Acha washtakiwe tu, kama hukumu itatoka kuwa wameshinda ina maana sana kwa nchi bila kujali kama fedha zinalipwa na ofisi ya RC/ hawa watu wakiachwa wajifanyie kama wanavyofanya nchi hii itazama, na kila kitu kitavurugika. Nchi imekuwa ya amani kwa miaka yote leo wanaibuka watu wanataka kuiporomosha huku wakijidai wanatunza amani!
 
"Mstahiki Mayor wa Arusha, Kalisti Lazaro, Madiwani, Viongozi wa Dini, Waandishi wa habari, wazazi mliokamatwa na Polisi (ambao kama walinukuliwa sahihi basi waliagizwa na ndugu Mkuu wa Mkoa Arusha);

NITAWASHANGAA SANA kama hamtafungua na kufuatilia case ya Unlawful Imprisonment dhidi ya kukamatwa kwenu (na kupewa lift bila hiari) na kudai fidia.

Mbona Arusha mna Wakili wengi tu?"

Haya ni maneno ya wakili msomi Peter Kibatala
Kibatala ametaja mawakili wasomi wanaoweza kusaidia hili
John Mallya, Sheck Mfinanga, Faraji Mangula
amezoea kula ruzuku ya chadema kirahisi anafikiri hela ya serikali ya jpm ni bwerere.
 
kila nnapomtazama gambo kwa jicho la tatu naonaga kama kuna kitu kimepunguka kwenye upstair yake. cjui ninyi wengine lakini hebu fanyeni utafitu..kila mnapomuona jaribun kumchek kwa jicho la kiutafit bila shaka mtagundua kitu ambacho sio normal
 
Back
Top Bottom