Kaka Kibanda kwanza nikupongeze kwa ujasiri wako ambao umekuwa ukiuonesha kwa muda mrefu kwenye fani hii ya Uandishi wa ahabari hapa nchini,ingawa kuna watu ambao hawapendi kukubaliana na wewe katika hoja zako,hili si tatizo kwa sababu huwezi kumlzimisha kila mmoja awe mshabiki wako ama akubaliane na wewe!
Pili kwenye fani ya Uandishi wa habari hauko kwa ajiili ya kumfurahisha kila mtu ama kumuudhi kila mtu,bali uko kwa ajili ya kueleza ukweli kwa jamii na kuufikisha ujumbe kama uivyo bila kuubadilisha ama kuukatakata vipande,na hii ni moja ya mambo ambayo watu hawapendi hasa kusikia,watanzania wamefika mahali pabaya sana na hasa hawa wanaojiita 'wanabadiliko'!
Hawa watu wanashangaza kweli,wnadhani mtusi na kejeli na kushibikia kila hoja inayomsifia mpizani ama kiongozi fulani wa upinzani ndio mabadiliko yenyewe,inasikitisha sana!!!,ni atu ambao hawataki kukuubali ukweli wal kuambiwa ukweli,ikifika hapo ni lazima watakuporomoshea matusi ya nguoni bila kujali wewe ni nani na umetoka wapi?!
Na ndiyo maana mimi nimekuwa nikisema kwamba bado CCM itaendelea kuongoza nchi hii pamoja na matatizo yake chungu mzima,kwa sababu watu hawataki kujifunza na kuujua ukweli wa mambo namna ulivyo na nini kifanyike,watu wamekuwa washabiki wa mambo bila kufanya utafiti na kujua ukweli,nasem hii haisaidii hata kidogo katika kufanya mabdiliko am mpinduzi!!.
Ni lazima watu wajifunze kuukubali ukeli na kua watfiti wa mambo na ha yale ya msingi yanayolihusu Taifa na watu wake,watu wajifunze kuwa wavumilibu wa kusikia na y upande a pili,watu ajifunze kusikia hata yale ambyo hawapendi kuyasikia,yale yanyowachoma moyo,ni vyema ukakubali kunywa Klorokwini pamoja na kamba ni chungu ili uweze kupona mlri,kuliko kunywa Panadol na kuituliza,mwisho wa siku Malria itandelea kukutafuna na mwisho wa iku ni kifo.
Hapa ndipo walipofika watanzania ambo mimi naamini kwamba hawaipendi nchi yao bali wanapenda kushabikia watu fulanifulani,nataka nikiri na kuamini kwamba Mahali ambapo CCM imewafikisha watanzani si pazuri,lakini kam kweli tunahitaji kufanya mabadiliko ya keli na kupata uongozin ulio imara ndani ya CCM ama nje ya CCM ni vyema tukawa wavumilivu na wapembuzi a mambo,tuachane na huu uhuni wa kushabikia mambo ili mrai tu jambo lililosemwa ni la kufagilia Dk.Slaa,Mbowe,Zitto............!!!
Hapa hakika tutakua bado hatuwasaidia watu hawa,hakuna mtu mkamilifu Duniani,wote wameghfilika,kikubwa hpa ni kujaribu kushauriana hata kama mtu amekwenda kinyume aambiwe ajue ili arudi kenye mtari na hatimaye tukamilishe ule mpango etu wa kufanya mabadiliko,vinginevyo tutakuja kuendelea kupiga makelele mara ohhhh tumeibiwa,mara ohhh tumefaniwa kile,kumbe hatukufanya maandalizi.
Ni ukeli kamba mtu aliyewahi kung'ata na nyoka hata akiguswa na jani tu anastuka,CCM kuna kitu imekiona kenye uchaguzi wa mwaka 2010,kwa hiyo kwa vyovyote vile kwa asa inajaribu kufanya kila linalowezekana ili kujisafisha,na kibaya zaidi wapinani wamekuwa wakitumia tu yale madhaifu ya CCM kujieleza ama kujoambanua kwa wananchi,sasa swali la msingi hapa kama CCM ikirekebisha hayo ambayo yanapigiwa kelele na wapizani si ni wazi kwamba itakapofika uchaguzi watu watasema si tayari wamerekebisha hili na hili ambayo bdiyo yalikuwa yakitusumbua,kwa hiyo maan yake ni kwamba wataipatia kura za kuiweka tena madrakani.
Ni vyema tukawa wawazi katika kuwashauri hawa viongozi wetu wa Upinzani kwamba kama kweli wanataka kuchukua nchi na kuingoza ni vyema wakawa na mikakati ya muda mfupi na muda mrefu ili kuendana na wakati na si kufanya mambo ambayo kesho na keshokutwa yakipatiwa ufumbuzi watu wanakosa hoja!!
Najua kuna watu watakuja na matusi yao hapa lakini mimi sijali kwa ababu huu ndio ukweli wenyewe,Kibanda hongera sana niko p[amoja na wewe,hebu tuendelee kuueleza ukweli na hasa kwa hawa wanaojifanya wapinzani kumbe ni mchwa waliojipenyeza kwa ajili ya kutafuna na kuusambaratisha upinzani,karibuni kwa matusi.Naamini wenye akili timamu watakuja na hoja lakini wale wasiokuwa na akili timamu wataanza kuporomosha matusi kwa Kibanda na kwangu tena kwa maneno mawili,matatu manne au maneno kumi tu!