Kibanda aliteswa na majasusi!

Nimeshangaa sana kwa gazeti la mtanzania kuandika makala km hii, na hili la kibanda liwe funzo hata kwa waandishi wengine kufichua uovu wote unaofanywa na serikali bila woga. Gazeti la mtanzania mwanzoni lilikuwa ni moja ya magazeti yaliyokuwa yanaitetea serikali na kuifichia maovu yaliyokuwa yanatendwa ila naona limeanza kubadilika baada ya mhariri wake kujeruhiwa
 
Acha kuota wewe, wapi umemsikia mwenyekiti wa madaktari akileta usumbufu baada ya kufanywa vibaya kule mabwepande? Zaidi zaidi Kibanda atakuwa na adabu ili hilo jicho lililobaki liendelee kuwepo..!
 
Unaweza kudanganya baadhi ya watu kwa muda fulani lakini sio watu wote kwa muda wote. Haya mambo ipo siku yatakuwa hadharani. Na tutashangaa sana kama ilivyokawaida yetu tutakapowaona wale tusiowahisi kumbe ndio kwenye mambo haya ya kishetani.
 
Rafiki yangu Pasco Mayala nadhani atasoma hili Uandishi wa Habari na Siasa ni hatari sana!

Bora yeye yuko na PPRA yake anangojea zake 7-7 na 8-8 anakula kama anashuka kwa sadala vile kiurainiiii! Machale yashamcheza Siasa za Bongo ni mwiba!
 
Last edited by a moderator:
Na sasa taarifa zaidi zinasema lile jicho alipigwa risasi...na maeneo yale hakukusikia mlio wowote wa risasi, ina maana jamaa walikuwa na "Sailensa" jambazi wa kawaida sio rahisi kumilikihiyo kitu!
 
Nilieleza toka mwanzo katika thread ile kua ni vigumu sana raia wa kawaida ambaye hajawa trained akawiva kwa kazi za ujasusi kufanya haya. Ni makosa makubwa kuhusisha CDM na mambo hizi. ila nokoleze kidogo, isije kua ni miongoni mwa wale maadui 11(sikumbuki vizuri namba kamili) wa Mh wa Mtama ambao jamaa aliapa kuwashughulikia, ndo kaanza nae huyo.
Tutayaona mengi sana kabla ya 2015
 
Mungu ni mwema sana Kibanda atapona na kuendelea na majukumu yake ya kila siku, tatizo ni kwamba hatuna jeshi la polisi hapa Tz, hata watuhumiwa wakijulikana pamoja na mtandao wao sijui kama kuna wakuwagusa.

Hilo limetokea, nadhani wengine wajifunze toka hapo.
 
Mi nadhani hawa wamezoeshwa na chama chao kuropoka tuu! Na hata Nape Nnauye na Mtela Mwampamba wanaweza kusaidia polisi maana waonesha wana ushahidi!
 
Last edited by a moderator:

Mkuu kwenye red umenena!
Kibanda alikuwa na ziada, alikuwa vuguvugu...ni hatari sana kwa mwandishi..leo unamuunga mkono fisadi huyu, kesho yule, kesho kutwa unamtukana matusi mpinga ufisadi wa kweli!! Namfahamu kibanda, nilishawahi kumwonya kwa tabia yake hiyo... Kwa mwandishi nivema kuwa moto au baridi fuu stop!
Alisahau kuwa fisadi ni fisadi tu!!!...
 
nijuacho,mwajiri wake wa awali hausk,yeye alishindwa kusoma alama ukutani.haiwezekan atoke t-daima aende kwa rostam azizi mdau mkubwa wa ccm na sirikali ake,nachokiona hapa alisogezwa ktk machinjio ili kuondoa shaka nyuma dhidi ya sirikali yetu mbovu,ebu fikirini kwa undani iweje apewe ajira huko wakati ana kesi mahakaman dhidi yao ya uasi eshini?pia kumbukeni ujumbe wa kamati ya kutafuta vazi la taifa alijitoa bada ya kuandamwa,na leo eti yupo kwa rostam hivi inaingia akilin kweli?hakusom alama ukutani.
 
tanzania haina raia wenye mafunzo maalum, wenye mafunzo maalum ni usalama wa taifa baadhi ya wanajeshi si wote na police kidogo sanaaaaa

lakini achilia mbali hapo kulingana na kilchomtokea ulimboka na sasa kibanda ukiunganisha na kufungiwa kwa mwanahalisi haina shaka kuwa wauaji ni state oparatives either wametumika na serikali au wanasiasa wenye uchu wa madaraka au wajeda wapuuzi ambao ni vibaraka wa wanasiasa

Tukienda mbali kidogo na kuangalia gazeti la Mtanzania ambalo linamilikiwa na Bashe ambaye ni mshirika wa Lowassa sidhan kama hii kazi itakuwa imefanywa na yeye najua hapo he is innocent lakin je huyu mwana usalama wa zamani ambaye hata familia ya mkuu inampigia chepe yeye twaweza kumuacha nyuma kwenye hili ukilinganisha kuwa yeye ni hasimu wa EL.... Hapa naweka Question mark kibao??????????????????
 
kikubwa zaidi twangalie je kuanzia ahamie huko kwa bashe je ameanddika nini cha kuwaudhi hawa jamaa
 
Na sasa taarifa zaidi zinasema lile jicho alipigwa risasi...na maeneo yale hakukusikia mlio wowote wa risasi, ina maana jamaa walikuwa na "Sailensa" jambazi wa kawaida sio rahisi kumilikihiyo kitu!

Wewe nae vipi ni risasi gani inayopiga jicho tu na bila kufumua kichwa chote? Au ndivyo silencer za kwenu zilivyo?

Halafu unakuta wanaoihusisha na Chadema issue hii ni wajinga fulani kama sijui Atongwele na pimbi wenzake ambao wanaonge pumba humu,mie nanyamaza wasije wakanisikia wakaning'oa kucha na meno yangu endeleeni tu nyie kama hamuwaogopiTISS na ccm yao
 
Enyi waandishi waganga njaa ,chagueni moja hivi leo kama mtawatumikia wananchi kwa kuwapa habari au mtaitumikia siasa,kama mtaitumikia siasa acha uandishi na kama utautumikia uandishi achana na siasa usije ukang'olewa kucha na meno na kuvunjwa taya kwa umbea wenu na njaa
 
Kwa kawaida Majasusi ni kwa ajili ya watawala, mtawala akibadilika nao huhamia kwa mtawala mpya. Mtawala mpya akisema mteseni huyu , hata kama alikuwa mtawala Majasusi hawana maswali they have intuitive thinking.
 

Mkuu soma gazeti la Tanzania daima la leo...limeripoti taarifa toka hosipitali huko Afrika kusini, na wamesema ni risasi!
Uwe unanunua magazeti bwana!! tena hilo la miatano tu!
 
Mtanzania wanajaribu kuungaunga stori...ukweli utabaki pale pale kuwa kibanda ameteswa na mwajiri wake wa zamani
 
Kwa kawaida Majasusi ni kwa ajili ya watawala, mtawala akibadilika nao huhamia kwa mtawala mpya. Mtawala mpya akisema mteseni huyu , hata kama alikuwa mtawala Majasusi hawana maswali they have intuitive thinking.
Basi kama ndivyo ilivyo basi siasa za kuuana au kulipiza kisasi hazina mashiko!! Kwa mantiki hii kazi imetumwa na walio madarakani!! Sasa wale wanaoituhumu CDM kwani iko madarakani?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…