Kibanda ajitoa kamati ya Nchimbi...

Kibanda ajitoa kamati ya Nchimbi...

only83

JF-Expert Member
Joined
Oct 15, 2010
Posts
5,342
Reaction score
2,528
...Muhariri wa gazeti la Tazania Daima amejitoa kwenye kamati ya kutafuta vazi la taifa iliyokuwa imechaguliwa na waziri Imanuel Nchimbi...sababu alizotoa ni kuonyesha kutokubaliana na serikali dhidi ya unyanyasaji wa waandishi wa habari akiwamo yeye.

Source:Channel Ten

======
Update
======

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

UTANGULIZI

Itakumbukwa kwamba Desemba 15 mwaka huu, Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Dk. Emmanuel Nchimbi aliniteua kuwa mjumbe katika Kamati ya Kitaifa ya Kukamilisha Mchakato wa Kupata Vazi la Taifa.

Siku chache baada ya uteuzi huo, nilipokea wito wa kuitwa na kuhojiwa na Jeshi la Polisi kutokana na makala ambayo ilichapishwa katika gazeti la Tanzania Daima la Jumatano, Novemba 30 mwaka 2011.

Kufuatia mahojiano hayo, Desemba 21 nilifikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, ambako polisi na wanasheria wa serikali walinifungulia mashtaka ya kuwachochea askari kutoitii Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Nilipata dhamana katika kesi hiyo ambayo imeahirishwa hadi Januari 19, 2012 itakapotajwa tena.

MSIMAMO NA UAMUZI WANGU

Baada ya kutafakari kwa kina kuhusu uteuzi wa Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo sambamba na uamuzi wa serikali kunihoji na kunifungulia mashitaka, busara yangu binafsi na kwa kuzingatia ushauri nilioupata kutoka kwa wahariri wenzangu, nimefikia uamuzi wa kujitoa katika Kamati ya Kutafuta Vazi la Taifa.

Nimelazimika kufikia uamuzi huo kwa sababu zifuatazo:
1. Mosi, uamuzi wa serikali kupitia Jeshi la Polisi na Waendesha Mashitaka kunifungulia kesi ya kuchochea uasi inanifanya niamini kwa dhati kwamba, haina imani nami binafsi na ina nia ya dhati ya kuhakikisha ninaadhibiwa na hivyo kukinzana na imani ambayo Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo ameionyesha kwangu kupitia uteuzi wake.
2. Pili, nimelazimika kufikia uamuzi huo wa kujitoa katika kamati hiyo baada ya kujiridhisha pasipo shaka kwamba mchakato mzima uliohusisha sakata langu kama Mhariri Mtendaji kuhojiwa na kufunguliwa mashitaka na polisi na hatimaye kufikishwa kwangu mahakamani usingeweza kufikiwa pasipo kuishirikisha Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo ambayo inaongozwa na Waziri Nchimbi.

3. Tatu, kwa kuyatambua hayo nimeona itakuwa ni uamuzi wenye hekima kujitoa katika kamati hiyo kwa kuzingatia uhalisia kwamba nitashindwa kutimiza wajibu wangu ipasavyo nikiwa mjumbe katika kamati hiyo, sababu kubwa ikiwa ni kuwapo kwa hali ya kutoaminiana na kutiliana shaka kati ya wizara na waziri Nchimbi kwa upande mmoja na mimi mteule katika kamati huyo kwa upande mwingine.

4. Mwisho, wakati nikichukua uamuzi huo mgumu, napenda kuchukua fursa hii kumshukuru sana Waziri Nchimbi kwa kuonyesha imani nami hata kuniteua kuwa miongoni mwa wajumbe wanane wanaounda Kamati ya Kitaifa ya Vazi la Taifa.

Imetolewa na

Absalom Kibanda
Mhariri Mtendaji
Free Media Ltd
Mwenyekiti Jukwaa la Wahariri
 
Nampongeza kwa dhati ndugu Kibanda kwa uamuzi wake wa kuachana na hili zoezi la kipuuzi. Tanzania tuna matatizo lukuki lakini Nchimbi anaona jambo la muhimu ni mavazi?
 
Waandishi wa habari kuwa cozy cozy na watawala kutaondoa objectivity.

Leo muandishi akubali kuteuliwa na waziri katika vikamati mbuzi vyenye ulaji tele, kesho waziri kachemsha, muandishi anaweza kumuwajibisha ipasavyo kweli?

Zaidi ya hapo, kwa mtu yeyote anayejiheshimu na kuheshimu na kuelewa utamaduni ni nini, idea nzima ya utamaduni kuamuliwa kwa kamati ni kituko.
 
...Muhariri wa gazeti la Tazania Daima amejitoa kwenye kamati ya kutafuta vazi la taifa iliyokuwa imechaguliwa na waziri Imanuel Nchimbi...sababu alizotoa ni kuonyesha kutokubaliana na serikali dhidi ya unyanyasaji wa waandishi wa habari akiwamo yeye.

Source:Channel Ten

Mimi nilidhani sababu itakuwa ni kutokukubaliana na dhana nzima ya kuwa na kamati ya kutafuta vazi la taifa na kufuja hela za walipa kodi kumbe yeye anazungumzia unyanyaswaji.

Pathetic.
 
Yametimia! What is Vazi la taifa? Upuuzi! Kibanda tulisubiri ufanye hili!
 
Safi kabisa bwana Kibanda,haiwezekani haohao wawanyanyase nyie waandishi tena wakati huo wajirudi kijanja umefanya vema sana mkuu kufanya hvyo
 
Mimi nilidhani sababu itakuwa ni kutokukubaliana na dhana nzima ya kuwa na kamati ya kutafuta vazi la taifa na kufuja hela za walipa kodi kumbe yeye anazungumzia unyanyaswaji.

Pathetic.
You got a point! Labda tupate statement nzima!
 
Waandishi wa habari kuwa cozy cozy na watawala kutaondoa objectivity.

Zaidi ya hapo, kwa mtu yeyote anayejiheshimu na kuheshimu na kuelewa utamaduni ni nini, idea nzima ya utamaduni kuamuliwa kwa kamati ni kituko.
Hapo kweli ni kituko ndugu yangu kiranga..!By the way kibanda amefanya uamuzi sahihi.
 
Waandishi wa habari kuwa cozy cozy na watawala kutaondoa objectivity

Heshima mbele sana mkuu,

Kwenye hiyo kamati wanahabari wamejazana.

Mwenyekiti wa kamati ni Joseph, mmiliki wa vituo vya radio, tv na magazeti.....mkuu ana maana yake hapa.
 
  • Thanks
Reactions: Ame
Hapo kweli ni kituko ndugu yangu kiranga..!By the way kibanda amefanya uamuzi sahihi.

Hapana uamuzi wake ulitakiwa uje mapema, sasa hapa asingenyanyaswa na kuhojiwa na vyombo vya dola basi angeendelea kula posho na kutafuna lunch na mkuu.
 
Mimi nilidhani sababu itakuwa ni kutokukubaliana na dhana nzima ya kuwa na kamati ya kutafuta vazi la taifa na kufuja hela za walipa kodi kumbe yeye anazungumzia unyanyaswaji.

Pathetic.

Wabongo kuondokana na ukoloni huu itabidi miaka mingi tu ipite, hususan kwa sababu mkoloni wa leo mweusi mwenzetu.
 
Naheshimu maamuzi ya Kibanda japo hayana utashi binafsi zaidi ya hisia potofu za kinyang'anyolo cha ukubwa ndani ya CCM.......siku moja ataujua ukweli.
 
Teh..teh...teh, kbanda bwana! Lakin nayeye si naskia yupo kwenye payroll ya mafisad?
 
Hivi huo unyanyaswaji wa waandishi wa habari na serikali umeanza yeye Kibanda alipokamatwa au upo muda mrefu?

Manake kama upo muda mrefu na yeye alipoteuliwa kuwa mmoja wa wanakamati kwa nini hakukataa kwa kutumia sababu hiyo hiyo aliyoitoa sasa?
 
Alipochaguliwa alikubali na kufurahi sana na kesho yake kulikuwa na column kubwa kwenye gazeti analoliongoza lenye heading ya " Kibanda aula kamati ya Vazi la Taifa" na mbaya zaidi aliye mteua ni waziri wa habari...hizi habari za leo kujitoa kwa ajili ya unyanyasaji ni ubinafsi wa hali ya juu, na ikumbukwe kuwa huyu jamaa ni mwenyekiti wa wahariri bongo.
 
Mimi nilidhani sababu itakuwa ni kutokukubaliana na dhana nzima ya kuwa na kamati ya kutafuta vazi la taifa na kufuja hela za walipa kodi kumbe yeye anazungumzia unyanyaswaji.

Pathetic.
Yote kwa pamoja.
 
Hivi huo unyanyaswaji wa waandishi wa habari na serikali umeanza yeye Kibanda alipokamatwa au upo muda mrefu?

Manake kama upo muda mrefu na yeye alipoteuliwa kuwa mmoja wa wanakamati kwa nini hakukataa kwa kutumia sababu hiyo hiyo aliyoitoa sasa?
Maswali mengine hayana msingi mambo huenda kwa wakati ukiwauliza wananchi kwa nini mwaka 2005 walimchagua Kikwete wengi watasema wangejua....sasa wamejua na Kibanda leo kajua simple.
 
Back
Top Bottom