Kibanda ajitoa kamati ya Nchimbi...

Mimi naungana na Kibanda it is nonsense sasa kuanza kujadili mwananchi avaeje wakati hajui mlo wake wakesho achilia mbali hiyo hela ya kununua hilo vazi la sherehe, labda waniambie hilo nalo limo kwenye mchakato wa katiba. Mimi ni mmasai bwana haya mambo yakulazimisha suti siyawezi huwa natinga ulaya na lubega na wazungu wana admire vile vile.


Hivi siku za nyuma sana si ilikuwepo "National Dress"? Wanaume ilikuwa inafanana na Kaunda Suit na wanawake ilikuwa vazi la vitenge na kilemba cha kitenge. Ni lini vazi hili lili expire?
 
Hivi huo unyanyaswaji wa waandishi wa habari na serikali umeanza yeye Kibanda alipokamatwa au upo muda mrefu?

Manake kama upo muda mrefu na yeye alipoteuliwa kuwa mmoja wa wanakamati kwa nini hakukataa kwa kutumia sababu hiyo hiyo aliyoitoa sasa?
. Si ni bora unyamaze!
 
Maswali mengine hayana msingi mambo huenda kwa wakati ukiwauliza wananchi kwa nini mwaka 2005 walimchagua Kikwete wengi watasema wangejua....sasa wamejua na Kibanda leo kajua simple.

Na ukiwauliza watz hao hao kwanini walirudia tena kumchagua jakaya 2010 watasemaje?maana urais alionao sasa hakuchaguliwa 2005! twende mbele turudi nyuma kibanda kwenye hili ana mambo yake binafsi na anajua mwenyewe kwanini anafanya hivi na kwa maslahi ya nani.....mbona hatukumuona akichukua maamuzi magumu kama haya wakati wa sakata la mpiganaji mpoki bukuku na askari magereza kwa kushirikiana na mh.mapuri au sakata la mwanahalisi kufungiwa na kubenea kumwagiwa tindikali au kwenye sakata la gazeti la kulikoni kufungiwa?hii ya yeye kuhojiwa na polisi juzi ndio unyanyasaji mbaya zaidi wa wanahabari kupata kutokea nchini?sipendi watu wanafiki.
 
Heshima mbele sana mkuu,

Kwenye hiyo kamati wanahabari wamejazana.

Mwenyekiti wa kamati ni Joseph, mmiliki wa vituo vya radio, tv na magazeti.....mkuu ana maana yake hapa.

Rushwa ya Tanzania haitaisha kamwe kama social capital itakuwa low kiasi hiki cha mtu kutumia ofisi ya umma ku-fulfil personal/group goals, well reciprocity siyo synonimous to corruption ....my own observation and reasoning!

Safari hii watajibeba wengine hatuambiliki wala kutishika we have all the powers kuvuruga mipango yao kiasi cha kuwafanya baadaye wageukiane wao kwa wao bila kujua mpanzi wa mbegu mbaya ni nani.
 
Na ukiwauliza watz hao hao kwanini walirudia tena kumchagua jakaya 2010 watasemaje?maana urais alionao sasa hakuchaguliwa 2005! twende mbele turudi nyuma kibanda kwenye hili ana mambo yake binafsi na anajua mwenyewe kwanini anafanya hivi na kwa maslahi ya nani.....mbona hatukumuona akichukua maamuzi magumu kama haya wakati wa sakata la mpiganaji mpoki bukuku na askari magereza kwa kushirikiana na mh.mapuri au sakata la mwanahalisi kufungiwa na kubenea kumwagiwa tindikali au kwenye sakata la gazeti la kulikoni kufungiwa?hii ya yeye kuhojiwa na polisi juzi ndio unyanyasaji mbaya zaidi wa wanahabari kupata kutokea nchini?sipendi watu wanafiki.
Watanzania wanazidi kuelimika wale wa 2005 walimchangua kwa 80%, walipogundua wamekosea wale welevu? hawakurudia kosa ndio maana 2010 akapata 60%, you know less by 20% kwa serikali hizi zenye kila kitu hadi tume za uchaguzi is not a joke, sielewi kama angegombea mara ya tatu angepata ngapi labda 20%. Kuhusu Kibanda wengi wana hoji kwa nini sasa? lets leave the decision to his discretion, labda ameona huu ndio wakati mwafaka kwake afterall hii si mara yake ya kwanza kusema serikali inanyanyasa vyombo vya habari.
 
Hivi siku za nyuma sana si ilikuwepo "National Dress"? Wanaume ilikuwa inafanana na Kaunda Suit na wanawake ilikuwa vazi la vitenge na kilemba cha kitenge. Ni lini vazi hili lili expire?
I don't think kama tulikuwa na official national dress.
 
...Muhariri wa gazeti la Tazania Daima amejitoa kwenye kamati ya kutafuta vazi la taifa iliyokuwa imechaguliwa na waziri Imanuel Nchimbi...sababu alizotoa ni kuonyesha kutokubaliana na serikali dhidi ya unyanyasaji wa waandishi wa habari akiwamo yeye.

Source:Channel Ten

======
Update
======



Kibanda utakuwa huru pale tu utakapotubu dhambi ya kuisaliti tasnia ya habari kwa kuwa mramba viatu vya mafisadi, kutafuta huruma kupitia mlango wa nyuma, eti unapambana na unyanyaswaji wa waandishi wa habari haitakusaidia, kwani umeshiriki kuwakandamiza waansihi wa habari nchini kutokana na unafiki wako.

Jee, na kwenye payroll ya EL nako umejitoa!!!
 


TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI



UTANGULIZI


Itakumbukwa kwamba Desemba 15 mwaka huu, Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Dk. Emmanuel Nchimbi aliniteua kuwa mjumbe katika Kamati ya Kitaifa ya Kukamilisha Mchakato wa Kupata Vazi la Taifa.

Siku chache baada ya uteuzi huo, nilipokea wito wa kuitwa na kuhojiwa na Jeshi la Polisi kutokana na makala ambayo ilichapishwa katika gazeti la Tanzania Daima la Jumatano, Novemba 30 mwaka 2011.

Kufuatia mahojiano hayo, Desemba 21 nilifikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, ambako polisi na wanasheria wa serikali walinifungulia mashtaka ya kuwachochea askari kutoitii Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Nilipata dhamana katika kesi hiyo ambayo imeahirishwa hadi Januari 19, 2012 itakapotajwa tena.

MSIMAMO NA UAMUZI WANGU

Baada ya kutafakari kwa kina kuhusu uteuzi wa Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo sambamba na uamuzi wa serikali kunihoji na kunifungulia mashitaka, busara yangu binafsi na kwa kuzingatia ushauri nilioupata kutoka kwa wahariri wenzangu, nimefikia uamuzi wa kujitoa katika Kamati ya Kutafuta Vazi la Taifa.


Nimelazimika kufikia uamuzi huo kwa sababu zifuatazo:

1.
Mosi, uamuzi wa serikali kupitia Jeshi la Polisi na Waendesha Mashitaka kunifungulia kesi ya kuchochea uasi inanifanya niamini kwa dhati kwamba, haina imani nami binafsi na ina nia ya dhati ya kuhakikisha ninaadhibiwa na hivyo kukinzana na imani ambayo Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo ameionyesha kwangu kupitia uteuzi wake.

2.
Pili, nimelazimika kufikia uamuzi huo wa kujitoa katika kamati hiyo baada ya kujiridhisha pasipo shaka kwamba mchakato mzima uliohusisha sakata langu kama Mhariri Mtendaji kuhojiwa na kufunguliwa mashitaka na polisi na hatimaye kufikishwa kwangu mahakamani usingeweza kufikiwa pasipo kuishirikisha Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo ambayo inaongozwa na Waziri Nchimbi.

3. Tatu, kwa kuyatambua hayo nimeona itakuwa ni uamuzi wenye hekima kujitoa katika kamati hiyo kwa kuzingatia uhalisia kwamba nitashindwa kutimiza wajibu wangu ipasavyo nikiwa mjumbe katika kamati hiyo, sababu kubwa ikiwa ni kuwapo kwa hali ya kutoaminiana na kutiliana shaka kati ya wizara na waziri Nchimbi kwa upande mmoja na mimi mteule katika kamati huyo kwa upande mwingine.

4. Mwisho, wakati nikichukua uamuzi huo mgumu, napenda kuchukua fursa hii kumshukuru sana Waziri Nchimbi kwa kuonyesha imani nami hata kuniteua kuwa miongoni mwa wajumbe wanane wanaounda Kamati ya Kitaifa ya Vazi la Taifa.

Imetolewa na

Absalom Kibanda
Mhariri Mtendaji
Free Media Ltd

Source; Katibu wa Jukwaa la Wahariri, Neville Meena



 
nchi hii bana inaongozwa na viongozi mambumbumbu sana..sasa kachochea kitu gani huyo kibanda?? huyu mwema bana na jeshi lake nd maana liko kama zezeta hivi
 
kajitoa ngoja tumuweke mtu mwengine ambaye atakuwa ni wakaribu yake ili imuume kwa kukosa dili la posho za mkuu wa kaya..

ngoja tuone dr nchimbi atasemaje kuhusiana na hili.

RIP TZ
 
nchi hii bana inaongozwa na viongozi mambumbumbu sana..sasa kachochea kitu gani huyo kibanda?? huyu mwema bana na jeshi lake nd maana liko kama zezeta hivi

unafahamu madhara ambayo yanaweza kutokea baada ya huo waraka tena kuchapwa gazetini? . Acheni serikari ifanye kazi yake, Hata angekuwa nani ni lazima ahojiwe kama amehusika ktk waraka huo, mbona nyie waandishi mnajiona kama maraika ktk nchi hii yaani hamtaki kuguswa kbs hata kama mnaenda nje ya utaratibu?. msijeweke juu ya sheria mtatupeleka kubaya kwanza mpo kama upepo vile na mnanunuliwa sana kuandika mambo mengine yasiyo na tija kbs kwa nchi yenu.
 
Back
Top Bottom