Kibamba: Demokrasia ndani ya CCM imesambaratika

sammosses

JF-Expert Member
Jan 24, 2011
1,682
1,110
Mwenyekiti wa jukwa la katiba Deo Kibamba amesikitishwa na hali ya demokrasia kuvurugika ndani ya CCM kutokana na malumbano ambayo yameshika kasi kwenye majukwa ya kisiasa kuliko ndani ya vikao halali vya Chama.Ameendelea kufafanua wakati wa mwalimu watu walikuwa wanapishana na kulumbana ndani ya vikao vya chama lakini mwisho wa siku mmoja alitoka nje nakupewa dhamana ya kuzungumzia msimamao wa pamoja wa chama,tofauti na hivi sasa kila mmoja natoka kivyake kusemea msimamo wake bila kujali vikao vya chama.

Hali ya kuvurugika demokrasia ndani ya CCM kimtazamo inatishia uhai wa chama ikiwa ni pamoja na kujenga makundi yasiyo na tija kwa mustakabli wa chama.Malumbano hayo yawezekana yakashika kasi ifkapo 2015 na kusababisha kusamabaratika kwa CCM.
 
ccm haijawahi kuwa na dmokrasia sema kulikuwa na wababe.<BR>sasa hivi kila mtu ni mbabe hakuna wa kumnyooshea mwenzake kidole.<BR>
 
Yes, ccm haijajijua yenyewe ni nani na cku zote wanaficha kujulikana wao ni nani, wasione ajabu kuitwa majina mengi tu kama ifuatavyo: Janga la Kitaifa, kichwa cha Nazi, Mafisadi, Majambazi, n.k
 
Mwenyekiti wa jukwa la katiba Deo Kibamba amesikitishwa na hali ya demokrasia kuvurugika ndani ya CCM kutokana na malumbano ambayo yameshika kasi kwenye majukwa ya kisiasa kuliko ndani ya vikao halali vya Chama.Ameendelea kufafanua wakati wa mwalimu watu walikuwa wanapishana na kulumbana ndani ya vikao vya chama lakini mwisho wa siku mmoja alitoka nje nakupewa dhamana ya kuzungumzia msimamao wa pamoja wa chama,tofauti na hivi sasa kila mmoja natoka kivyake kusemea msimamo wake bila kujali vikao vya chama.

Hali ya kuvurugika demokrasia ndani ya CCM kimtazamo inatishia uhai wa chama ikiwa ni pamoja na kujenga makundi yasiyo na tija kwa mustakabli wa chama.Malumbano hayo yawezekana yakashika kasi ifkapo 2015 na kusababisha kusamabaratika kwa CCM.

tena wengine tunaomba malumbano hayo yaendelee. wanyonyane macho ili hawa Gambaz wakafie huko
 
Malumbano nimsingi wamaendeleo namabadiliko!Ukiona mwenye uelewa na ufahamu hafuati utaratibu ujue lipo lazaidi kwenye huo utaratibu!Nakosa nikosa tu liwe limetajwa kwautaratibu au bila utaratibu!Cha msingi nikujiangalia nakujisahihisha sio ooo hajafuata utaratibu!Wakati unaona kweli umekosea!Ifike wakati tuache blaablaa tukubali mapungufu tubadilike twende mbele!
 
Tatizo ambalo hawataki kulisikia japokluwa vijana nao wamepewa uongozi wa chama ni changamoto iliyoachwa na marehemu Horace KOLIMBA kuwa chama kimepoteza dira na mwelekeo.Nilidhani Nape akitumia falsafa iliyoachwa na aliyekuwa katibu mkuu huyo kukinusuru chama kumbe naye ameiingia kwenye mfumo ule ule wa majungu na malumbano yasiyo na tija badala ya kufanyia kazi tahimini iliyo achwa na Kolimba.

Ama kweli kiumbe hukifuata kifo chake pale kinapomfika.
 
Mwenyekiti wa jukwa la katiba Deo Kibamba amesikitishwa na hali ya demokrasia kuvurugika ndani ya CCM kutokana na malumbano ambayo yameshika kasi kwenye majukwa ya kisiasa kuliko ndani ya vikao halali vya Chama.Ameendelea kufafanua wakati wa mwalimu watu walikuwa wanapishana na kulumbana ndani ya vikao vya chama lakini mwisho wa siku mmoja alitoka nje nakupewa dhamana ya kuzungumzia msimamao wa pamoja wa chama,tofauti na hivi sasa kila mmoja natoka kivyake kusemea msimamo wake bila kujali vikao vya chama.

Hali ya kuvurugika demokrasia ndani ya CCM kimtazamo inatishia uhai wa chama ikiwa ni pamoja na kujenga makundi yasiyo na tija kwa mustakabli wa chama.Malumbano hayo yawezekana yakashika kasi ifkapo 2015 na kusababisha kusamabaratika kwa CCM.

Enzi za Mwalimu maamuzi ya vikao yalikuwa yanafanyiwa kazi objectively and decisively tofauti na sasa hivi ambao maamuzi ya vikao ni subjective ili kulinda kambi moja au individual interests against the other na kwa hiyo kusababisha sintofahamu unazozishuhudia kwa sasa, wengi wamekosa imani na utendaji wa chama kwa hiyo wanaamua kuongea nje ya vikao ku-send message kwamba hawaridhiki na hali ilivyo ndani ya chama, hawana imani na vikao tena, kwa mfano wakati wa uchaguzi mdogo wa Arumeru mashariki tuhuma za rushwa zilianikwa dhidi ya Sioi Sumar aliyekuwa mgombea wa CCM; lakini bado Mwenyekiti akaamua kuzifumbia macho kama vile kutotaka kukwazana na Edward lowassa ambaye ni Baba mkwe wa Sumari na king maker, hata majuzi walipojaribu kutathmini kushindwa kwao Arumeru Mashariki; kuna tetesi JK aliizima agenda hiyo nafikiri kwa sababu zile zile nilizozitaja awali! kwa utaratibu huo people are frustrated ndio maana wanaropoka hovyo hovyo; tutashuhudia mengi katika siku zijazo.
 
Kila chama kina utaratibu wake wa kusemea mambo yake,na msingi wa katiba ya CCM ulitamka wazi kiongozi yeyote yule akubali kukosolewa na kukosoa pale panapo kwenda tofauti na mtazamo wa kichama.Tatizo lililopo kuna watu wamepandikizwa kuhakikisha wanapinga kila kitu hata kama ni kizuri ili kufanikisha malengo ya mtu fulani kwa maslahi binafsi.

Ukweli siku zote utajidhirisha mara baada ya CCM kuacha mi9singi yake kama katiba ya mwaka 1977 ya CCM ilivyotamka na kuwa chama cha matajiri wakubwa tena wenye pesa chafu.Hali hiyo ndiyo tatizo linaloikumba kwa sasa,na kwa kuwa ndiyo walioshika serikali basi na serikali yake imekuwa ya ubabaishaji bila kujali matakwa ya wananchi wake.

Malumbano nimsingi wamaendeleo namabadiliko!Ukiona mwenye uelewa na ufahamu hafuati utaratibu ujue lipo lazaidi kwenye huo utaratibu!Nakosa nikosa tu liwe limetajwa kwautaratibu au bila utaratibu!Cha msingi nikujiangalia nakujisahihisha sio ooo hajafuata utaratibu!Wakati unaona kweli umekosea!Ifike wakati tuache blaablaa tukubali mapungufu tubadilike twende mbele!
 
Mwalimu Nyerere alishasema upinzani wa kweli utatoka ndani ya chama cha mapinduzi,na kweli upinzani huo wa kweli ndiyo unao dhoofisha chama,chama kimeingia kwenye utwala wa kambale kila mna ukoo ana sharubu matokeo yake haijulikani nani baba,mama na mtoto.Ukosefu huu unaosababisha unyaufu ndani ya chama ni kuzaa serikali legelege inayoshindwa kusimamia ustawi wa wananchi wake kwa kujishughulisha election canddate rally ilihali muda wa uchaguzi haujafika.

Enzi za Mwalimu maamuzi ya vikao yalikuwa yanafanyiwa kazi objectively and decisively tofauti na sasa hivi ambao maamuzi ya vikao ni subjective ili kulinda kambi moja au individual interests against the other na kwa hiyo kusababisha sintofahamu unazozishuhudia kwa sasa, wengi wamekosa imani na utendaji wa chama kwa hiyo wanaamua kuongea nje ya vikao ku-send message kwamba hawaridhiki na hali ilivyo ndani ya chama, hawana imani na vikao tena, kwa mfano wakati wa uchaguzi mdogo wa Arumeru mashariki tuhuma za rushwa zilianikwa dhidi ya Sioi Sumar aliyekuwa mgombea wa CCM; lakini bado Mwenyekiti akaamua kuzifumbia macho kama vile kutotaka kukwazana na Edward lowassa ambaye ni Baba mkwe wa Sumari na king maker, hata majuzi walipojaribu kutathmini kushindwa kwao Arumeru Mashariki; kuna tetesi JK aliizima agenda hiyo nafikiri kwa sababu zile zile nilizozitaja awali! kwa utaratibu huo people are frustrated ndio maana wanaropoka hovyo hovyo; tutashuhudia mengi katika siku zijazo.
 
Watanzania wa leo wanamwomba sana mwenyezi Mungu CCM isambaratike ili usiku ulioendelea kwa miaka zaidi ya 50 sasa papambazuke. Mungu wetu kama unavyotupenda sisi waja wako tunaomba chama hiki chenye kuwatesa watanzania kwa miaka hiyo yote kife. CCM lazima efe watanzania wapone na umasikini. CCM ife kwa manufaa ya watanzania wanyonge lakini kama itaendelea kusitawi ni dalili mbaya kwa watanzania. CCM lazima ife AMINA
 
Siku zote dua njema Mungu huibariki,kwa muda tangu wakae madarakani hakuna kubwa walililofanya zaidi ya kuwagawa Watanzania kwa udini,ukanda na kipato.Mwalimu alishatusahaulisha utumwa lakini hivi sasa tabaka la watwana na mabwana limeshika kasi.Ndio maana leo pesa zinaitwa vijisenti,ndo maana leo kuna wafanyabiashara wenye mifuko mikubwa iliyoweza kuiweka serikali yetu mikononi mwao.
 
Huu ni ugonjwa Unaoambukiza kama AIDS Ni vizuri zikawekwa kanuni kali kuzuia watu kuzungumza nje ya vikao mambo yanayoweza kukiangamiza chama. CDM hatuko mbali na hili tusichekelee kabisa watanzania wanapenda kuiga zaidi kuliko kubuni kitu kipya. Tutarajie akina SHIBUDA wengi pia
 
Hapo umesema CDM wasibweteke kwa kuona nao wanapendwa sana na wanyonge,kwani mlolongo wa wakimbizi wa kisiasa toka CCM waangaliwe vizuri ikibidi wachujwe yasije yakawakuta yanayowakuta CCM
 
Kuanzia viongozi walio Serikalini kwa tiketi ya ccm,pamoja na wananchama wake wote wapo kwa ajili ya maslahi yao binafsi,sasa anapotokea mtu ndani ya ccm ama nje ya ccm kumshututu kiongozi hasa kwa wizi wa Mali ya uma ndipo hapo hupoteza subira na kujibu mapigo bila kusubiri vikao halali vya chama na sbb kuu ni kuwa Yule anaeshutumiwa huwa anaona kitumbua chake kinatiwa mchanga.Tujiulize unapokuwa ktk chama kwa minajili ya kusubiria ulaji na sio kuwatumikia wananchi unafikiri hicho kitakuwa ni chama au taasisi ya kuzalisha wezi?(EPA/RICHMOND to DOWANS/KAGODA/B.O.T).
 
Tukatae tusikatae mfumo ndani ya chama umepitwa na wakati kiasi tusipokuwa makini mdororo huu unao kikumba chama hiki utazidisha shughuli za maendeleo kudidimia.Nasema hivyo ni kimaanisha viongozi hawa wa serikali ndiyo viongozi wakuu wa CCM wamejikita zaidi kwenye migogoro maslahi kwa nbio za urais zaidi kuliko kujikita kwenye matatizo ya wananchi.Hali inayopelekea uchumi wetu kudidimia.
 
Back
Top Bottom