Kibali cha kufufua maiti chamtokea puani

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
42,318
33,125
MKUU wa wilaya ya Mbinga, Edmund Mjengwa, amemsimamisha kazi Ofisa Mtendaji wa Kata ya Ruanda, Maurus Lulemi na kuamuru awekwe rumande. Hatua ya Mjengwa inatokana na Lulemi kudaiwa kutoa kibali kwa mganga wa jadi, ili amfufue mtoto anayedaiwa kufa kwa imani za kishirikina. Akizungumza na Uhuru jana, Mjengwa alisema amefikia uamuzi wa
kumsimamisha kazi ofisa huyo kutokana na kukiuka maadili ya kazi. Alisema serikali haiamini ushirikina. “Ndiyo nimemsimamisha kazi na tutamfikisha mahakamani kwa sababu alichofanya kinaweza kuhatarisha amani na kusababisha mauaji,” alisema. Awali, ilidaiwa kuwa, usiku wa Mei 18, mwaka huu, Lulemi alitoa kibali kwa mganga huyo ili apige ramli na kumfufua mtoto huyo kutoka kaburini. Lulemi, ambaye ni mlinzi wa amani katika kata hiyo, aliruhusu kitendo hicho kufanyika kwenye eneo lake, ambapo zilizuka vurugu miongoni mwa wakazi wa eneo hilo. Imeelezwa kuwa, Lulemi alishindwa kuzuia vurugu hizo, hivyo kulazimika kutoa taarifa kituo cha polisi wilayani Mbinga, kuomba msaada wa askari ili kutuliza ghasia hizo. Polisi walifika eneo la tukio na kuzima vurugu hizo, ambapo baadae uchunguzi ulibaini chanzo ni hatua ya Lulemi kuruhusu upigwaji ramli. Kamanda wa Polisi mkoa wa Ruvuma, Michael Kamuhanda, alisema walimtia mbaroni Lulemi na atafikishwa mahakamani muda wowote. Alisema katika vurugu hizo, baadhi ya wananchi wa eneo hilo wamedai kupotelewa na mali mbalimbali.


Kibali cha kufufua maiti chamtokea puani
 
Back
Top Bottom