Kibaka Alipojaribu Kumuibia Mike Tyson

Kibaka Alipojaribu Kumuibia Mike Tyson

Herbalist Dr MziziMkavu

Platinum Member
Joined
Feb 3, 2009
Posts
43,093
Reaction score
34,910
[TABLE="width: 491"]
<tbody>[TR]
[TD="colspan: 3"]Kibaka Alipojaribu Kumuibia Mike Tyson[/TD]
[/TR]
[TR="bgcolor: #E1E1E1"]
[TD]
6174422.jpg

Mike Tyson[/TD]
[TD]Sunday, January 08, 2012 9:22 PM
Kibaka wa nchini Marekani ambaye alizamia kwenye chumba cha hoteli kwaajili ya kuiba alinusuru maisha yake kwa kuahirisha mpango wake na kukimbia baada ya kugundua mtu aliyetaka kumuibia ni bingwa wa zamani wa ndondi za uzito wa juu duniani, Mike Tyson.[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="colspan: 3"]Kibaka huyo alizamia kwenye chumba cha hoteli ambayo Mike Tyson na familia yake walikuwa wamefikia baada ya sherehe za kuukaribisha mwaka mpya wa 2012 ambazo ziliambatana na shoo ya nguvu ya muziki toka kwa mkongwe Stevie Wonder.

Bingwa huyo wa zamani wa ndondi za uzito wa juu ambaye alijipatia umaarufu duniani kwa kuwadondosha watu ulingoni kwa makonde yake alikuwa amelala kwenye chumba cha hoteli ya The Cosmopolitan iliyopo mjini Las Vegas wakati aliposikia sauti ya mtu akinyata ndani ya chumba chake.

Kibaka huyo baada ya kugundua kuwa mtu aliyetaka kumuibia alikuwa ni Mike Tyson, aliahirisha mpango wake na kukimbia mikono mitupu.

Walinzi wa hoteli waliitwa na msako mkali wa kumtafuta mwizi huyo ulianza.

Msemaji wa hoteli ya The Cosmopolitan alisema kuwa wamepokea taarifa za tukio hilo na polisi wameanzisha uchunguzi wao.[/TD]
[/TR]
</tbody>[/TABLE]

chanzo. Kibaka Alipojaribu Kumuibia Mike Tyson
 
bora alikimbia maana sipati picha angekamatwa cjui ingekuwaje.
 
Uwoga wake tu jamaa nowadays kawa kama babu wa ordonyo tu hahahahaaaa......lol.
 
Jamaa ngumi yake ina kilo 50 yaani ni kama mfuko wa cement uliojaa sawa sawa.
 
Back
Top Bottom