Kiba na Harmonize kumpaisha Diamond juu zaidi

Justine Marack

JF-Expert Member
Jul 31, 2014
572
1,582
Kama mfuatiliaji wa muziki wa bongo kuna vitu tunakubaliana kuwa Kiba na Harnonize kwa nyakati tofauti wamenufaika sana na uwepo wa Dai.

Alikiba amekuwa mshindanishwa wa Diamond kwa muda mrefu, hii kitu ilimfanya kubweteka na kulala fofofo na hata akiwa hatoi ngoma watu walimzungumzia kwakua hakukuwa na msanii mwingine wa kumchalenji Chibu.

Sasa Mambo yamebadilika baada ya Harmonize kujiondoa WCB na inakua wazi anaitaka nafasi ya Kiba ili kupambana na Diamond. Watu wote wanao mchukia Mond wamehamia kwa Hamo. Sasa kiba na Hamo wanagawana mashabiki ambao wote ni wale wasio mpenda Mond, kuanzia media na watu binafsi.

Lakini kwa namna yoyote lazima washindane na Mondi ili wapate nafasi wanayo itaka. Kwa kuangalia kwa umakini. Alikiba ni kama huwa ameweka nyimbo kabatini akisubiri kiki kwa Mondi. Kipindi Kiba natoa Seduce kiki ilitoka kea Mondi baada ya kupost Picha ya Tangazo la Pepsi akiwa anacheka sanaa wakati huo huo WCB wakaachia wimbo wa Zilipendwa na hapo ndipo kila kona watu wamuonea huruma Kiba na kumpa Sapoti katika wimbo wake mpya.

Baada ya hapo hakutoa hit tena mpaka hii ya sasa baada ya Mondi kumualiaka kwenyw WCB festival na Kiba kinyume na kawaida yake akaibua habari za Penseli.

Ili kuthibitisha hilo Kiba akaita waandihi wa habari na wakaenda kwa wingi sana, Katika mahojioano baada ya Kiba kuulizwa habari za penseli Akajibu kuwa Najua wengi mmekuja kwa ajili ya kutaka kujua penseli. Kwahiyo kiba aliianzisha ishu ya penseli kama kiki na kutoa nyimbo.

Sasa Kiba ameshtuka, ila kubweteka hakuna tena, anaona Hamo anayemelea nafasi yake. Kiba sasa Ametangaza Festival yake kam Mondi na Wasafi festival. Kiba amekuwa wa kumchokonoa Mondi na sasa Kiba Namtaja Jina Diamond kwa sauti ya juu tofauti na alivyo zoweleka.

Katiak hali hii tunatarajia Naseeb Jumaa, Chibu Evara atazidi kuwa juu sana kwa miaka Mingine Mingi. Bila kusahau Media zake pia ziatapaa juu zaidi kwa kuwa zitakuwa zinatoa habari za wasanii wote, yaani mtazamaji wa Wasafi tv na Fm atakua napata habari zote hapo tofauti na kule wanako toa habari nusunusu.
 
Furahia kila hatua ya mafanikio ya kiburudani. Haiijalishi Ni kwa namna gani. Penda unachopenda kukisikiliza, shabikia unachopenda kushabikia support unachotaka kuki support

Mziki Ni mziki tu. Na mashabiki Ni wale wale tu
Wote Ni wanariadha wanaoshindana kwenye shindano moja so hawawezi kwenda sawa kwa sababu kila mtu ana kasi na mbinu zake za ukimbiaji
Kuwa na siku njema
 
siku zote ntasema kiba amshukuru sana simba ju bila yeye jina kiba lingekuwa historia kimziki hayupo kabisa
 
Wasiompenda Mondi (ikiwepo watu wasiopenda kuona mtu anafanikiwa, Media zilizotaka kuwatumia Wcb katika show za laki mbili wakagomewa, ma ex wake, wenye chuki binafsi nk) hawa wote waliungana kumsapoti Kiba kama kumkomoa Diamond na kumshusha.....sasa genge hili limegawanywa mara mbili na Harmonize kitendo kinachompa Dee nguvu maana namba zake zipo vile vile hazija gawanyika.

Hii inabidi anaejiita Mfalme afanye kazi ya ziada kweli kweli maana madhara yamesha onekana kule YouTube....zamani aliungwa mkono na promo za Mange na ghafla alishika namba ila leo hii Mange hafui dafu maana namba zimegawanywa.
 
Back
Top Bottom