Kiatu cha ''Shoga" - A

black abdu

Senior Member
Dec 2, 2022
152
208
Kuna yale mahojiano kati ya Zamaradi na marehemu Kaoge, aliyekuwa shoga maarufu Dar, ambayo yalisababisha kipindi cha Zama kufungiwa. Swali moja lilinifikirisha, alimuuliza Kaoge kama angependa mwanae aje kuwa shoga pia... kwa mshangao wangu Kaoge alijibu HAPANA!!

Nikajiuliza, kama ni kitu wanachokipenda, kwa nini wasipende watoto wao pia wawe kama wao?

Kutoka uchunguzi kidogo nilioufanya ni kuwa wao hawajivunii kuwa walivyo, ni kama mtu amezaliwa na kujikuta na ulemavu fulani, ndivyo hata wao wanatamani wanegkuwa kama wanaume wengine wa kawaida ila hisia zao zinakinzana nao (utalielewa vema baadae kidogo) ......utaniuliza mbona kuna hao maarufu tunawaona mitandaoni?

1. Hao wamefikia hapo baada ya kupata ushawishi kutoka kwa mashirika au watu wanaofanya kazi na watu wa aina hiyo, kuwa wajiamini na kujikubali, lakini mwanzo hawakuwa hivyo, walichukulia hali hii kwa kificho na aibu.

2. Jamii yetu ina mchango mkubwa kuwapaisha hawa watu, hasa kupenda habari za Kiki na udaku wa ajabu, mtu akiwa na umaarufu kiajabu, anaula. Ukiangalia wanaovuma hawana cha maana wanachofanya, ila Jamii ndio inawapa umaarufu.

MASHIRIKA YANAYOHAMASISHA USHOGA:
Najua kuna mashirika yanayotetea haki za hawa watu lakini sikujua kuna mashirika yanahamasisha ushoga, kuwa watu wawe mashoga....kwa manufaa gani na ya nani? Wao wananufaikaje? Hata tukisema Marekani inahamasisha ushoga; wao wananufaika na nini? Mbona kwao hawafanyi hizo jitihada za kuhamasisha zaidi ya kutetea tu haki zao, wasibaguliwe au kunyanyasika?

Bado natafakari juu ya hii dhana mpya kuwa kuna mashirika yanahamasisha, hadi watoto wanafundishwa......halafu iweje?

Kama kweli yapo, tunahitaji kupambana nayo kwa hali yoyote kwa sababu watatuzalishia kizazi kitakachoteseka na nafsi zao.

Nasema watateseka na nafsi zao kwa sababu hata huko Ulaya tunaona mashoga walio maarufu wengi wakipitia nyakati za msongo wa mawazo na hata wengine kuishia kujiua.

Nawaweka Mashoga kwenye makundi haya:

Tuendelee Post B
 
Back
Top Bottom