Hata huyo Messi wako anatakiwa kujuwa tamaduni zake sio kwa dunia yote.
Kwanza huyo Messi siyo wangu, ni wa Barca, na umesema vema "anatakiwa kujuwa tamaduni zake siyo za dunia yote". Bila shaka unaweza kujibu haya maswali:
1. Kama alitakiwa kujua tamaduni zake na siyo za dunia yote ulitegemeaje ajue tamaduni za watu wa Misri?
2. Kwa kuwa utamaduni uliopo ktk jambo hili ni wa SOKA, je, unajua maana ya KIATU CHA SOKA (siyo kila kiatu) ktk utamaduni wa soka?
3. Unajua ni kwa nini mchezaji bora kwenye soka hutunikiwa sanamu ya KIATU cha dhahabu? Na je, kwa mantiki ya wamisri na wewe, FIFA huwa inamdhalilisha huyo mchezaji bora?
4. Kama unaelewa kuwa lengo la Messi lilikuwa ni kufanikisha "fund raising" kwa lengo jema, je, unaelewa jambo la kunadi "Kiatu cha soka cha Messi" lingeleta thamani gani?
Jamani, mimi naamini sote tuliumbwa na akili njema na ufahamu mzuri na Mwenyezi. Ebu jitahidini kuondoa hizo kuta bandia katika akili zeni ili muuone uzuri wa kazi ya Mwenyezi nje ya kuta zenu!