Kiatu cha Messi chawakera raia wa Misri

real G

JF-Expert Member
Feb 7, 2013
5,227
5,292
Hatua ya mchezaji maarufu wa soka duniani Lionel Messi kutoa viatu vyake viuzwe kusaidia watu wasiojiweza imeibua mjadala mkali nchini Misri.

Messi alifanya hivyo akidhani labda kwamba alikuwa anafanya hisani bila kufahamu kwamba viatu huwa na maana nyingine nchini Misri na pia katika mataifa ya mengine ya Uarabuni.

Wakati wa mahojiano ya runingani ''katika kipindi cha Yes am Famous'' kinachopeperushwa hewani na runinga ya MBC Misri, mchezaji huyo wa Argentina aliwaambia watangazaji hao kwamba angependa kutoa viatu vyake vipigwe mnada.

Kitendo chake kilipokelewa tofauti kabisa na wiki chache zilizopita alipopongezwa na kusifiwa sana kwa kutimiza ndoto ya kijana mmoja wa Afghanistan alipomtumia mpira na fulana yake.
Alipokuwa akivitoa viatu vyake Misri, hakujua kwamba viatu huchukuliwa kama matusi au kukosea watu heshima katika maeneo mengi ya Mashariki ya Kati.

Muda mfupi baadaye wakazi wa maeneo hayo walimkashutumu sana kupitia mitandao ya kijamii
Na ili kujibu matusi hayo mbunge mmoja wa Misri said Hassin anayetangaza kipindi kwa jina 'Infirad' alitoa kiatu chake na kusema kwamba atampatia Messi.

Chazo:BBC
 
Dunia ya sasa tunapaswa pia kujifunza tamaduni za watu wengine
Niliwahi kuona Colin Powell akifurahia kuoneshwa mbwa aliepewa jina lake

Sasa sisi waswahili mtu akikwambia nimempa mbwa wangu jina lako utaona nimekuheshimu au nimekudharau?
 
Hahaha,

Bill Clinton alimpa mbwa wake jina la "Buddy", jina hilo lilikuwa la mjomba wake aliyempenda ambaye alikuwa amefariki muda si mrefu wakati huo.

Unaweza ku imagine mswahili umpe mbwa wako jina la mjomba wako aliyefariki muda si mrefu uliopita?
 
kwa waswahili mbwa ni kiumbe cha hadhi ya chini sana , ila hao wanamuona kama rafiki
 
watu wengine vichwani kumejaa kamasi tupu,unalazimishaje misri apende tamaduni za messi?huyo messi akifanyiwa vitendo ambavyo si utamaduni wake atachekacheka?wabongo sijui tuna nini sisi,au chuki tu kwa wamisri?
 
Waliokasirika ndio wamechemka.

Messi ni football star. Kiatu ni football gear. Kutoa gear yake ni ishara ya heshima.

Utamaduni wa kuangaliwa hapo ni wa soka.
Mkuu hakuna kitu adhimu kama utamaduni na ustaarabu wa jamii. Kila jamii ina tunu zake ambazo ukizigusa unakosana nao, sisi tumekuwa tofauti kidogo ila wenzetu wako nazo hizo tamaduni zao. Usiwalaumu waarabu kwa kuwa sisi tamaduni zetu tunaziasi sana, Messi ana menejimenti na washauri anaowalipa ambao lilikuwa jukumu lao kutazama tukio hilo.
Hao wataalamu walitakiwa wamwambie Messi hiki hakifai kwa hawa watu, atafute njia zingine manake anazo sports gear nyingi sana. Kma unakumbuka suala la Mascerano alivyokumbwa na suala la kodi, yeye alisema kuna watu amewaajiri na lilikuwa jukumu lao kulipa kodi na yeye binafsi hahusi na adhabu itakayotolewa.
 
Dunia ya sasa tunapaswa pia kujifunza tamaduni za watu wengine
Niliwahi kuona Colin Powell akifurahia kuoneshwa mbwa aliepewa jina lake

Sasa sisi waswahili mtu akikwambia nimempa mbwa wangu jina lako utaona nimekuheshimu au nimekudharau?

:)

Interesting...
 
Mkuu hakuna kitu adhimu kama utamaduni na ustaarabu wa jamii. Kila jamii ina tunu zake ambazo ukizigusa unakosana nao, sisi tumekuwa tofauti kidogo ila wenzetu wako nazo hizo tamaduni zao. Usiwalaumu waarabu kwa kuwa sisi tamaduni zetu tunaziasi sana, Messi ana menejimenti na washauri anaowalipa ambao lilikuwa jukumu lao kutazama tukio hilo.
Hao wataalamu walitakiwa wamwambie Messi hiki hakifai kwa hawa watu, atafute njia zingine manake anazo sports gear nyingi sana. Kma unakumbuka suala la Mascerano alivyokumbwa na suala la kodi, yeye alisema kuna watu amewaajiri na lilikuwa jukumu lao kulipa kodi na yeye binafsi hahusi na adhabu itakayotolewa.
watu wengine vichwani kumejaa kamasi tupu,unalazimishaje misri apende tamaduni za messi?huyo messi akifanyiwa vitendo ambavyo si utamaduni wake atachekacheka?wabongo sijui tuna nini sisi,au chuki tu kwa wamisri?
mimi sitamlaumu Messi, kwa kuwa alikua na lengo zuri tu,
halafu pia mbona wachezaji wa Raja Casablanca ya Morocco (ambao ni waarabu) walishang'ang'ania viatu vya ronaldinho ili wakaviweke kama ufahari? kwa hiyo tamaduni za hawa watu hazipo clear

VIDEO: Raja Casablanca players take Ronaldinho's boots - Goal.com
 
mimi sitamlaumu Messi, kwa kuwa alikua na lengo zuri tu,
halafu pia mbona wachezaji wa Raja Casablanca ya Morocco (ambao ni waarabu) walishang'ang'ania viatu vya ronaldinho ili wakaviweke kama ufahari? kwa hiyo tamaduni za hawa watu hazipo clear

Ronaldinho booted out of the Club World Cup by Raja Casablanca players
Samahani mkuu, katika nchi za kwanza duniani kuuonja ustaarabu ni Misri. Hawa watu wana ustaraabu mkongwe sana na wanauheshimu sana, unaweza kuona ni waarabu waliopo Afrika lakini kwenye duru za kiarabu Misri ni moja kati ya nchi zenye heshma kubwa sana.
Kama utakumbuka mwanzoni ilikuwa ni adimu sana kuona mchezaji wa Misri akicheza ligi nje ya Misri. Yote ile ilikuwa ni kuonyesha wenyewe ni bora sana. Sasa kwa hili la Messi linafungua hisia zingine kwa Waarabu wa Misri, wanaona Messi hajawatendea haki, kwa kuwa kama ni sportsgear mbona zipo nyingi ukiachilia mbali kiatu! Pole sana mkuu.
 
sasa kama waarabu wanaona kiatu cha mtu ni kama tusi kwao kwa nini waling'ang'ania hicho kiatu cha dinho? au hawa walivunja tamaduni?
 
Mie nazungumzia waarabu wa Misri weye unawasema waarabu wa Morocco, sasa tutaelewana? Nimeshakueleza hapo juu jinsi waarabu wa Misri walivyo tofauti na Bedouins!
 
kwa hiyo waarabu wanao mind ishu ya viatu ni wa misri tu?
 
Back
Top Bottom