Kiapo cha ndoa kirekebishwe

GAGL

JF-Expert Member
Aug 5, 2010
390
395
Katika kuifikia Tanzania isiyokuwa na ukimwi kama kampeni iliyozinduliwa na Mhe. Rais miaka michache iliyopita "Tanzania bila ukimwi inawezekana" ninapendekeza kiapo cha ndoa kiwe namna hii:- "Mimi X nakubali kumuoa/kuolewa na Y awe mke/mume wangu katika maisha yangu yote, katika shida na raha na naahidi kumpenda, kumlinda katika hali yoyote ile na naahidi mbele ya Mungu, kanisa/msikiti/serikali, waamini waliopo hapa, ndugu, jamaa na marafiki kutomsaliti mwenzangu kimwili kwa kushiriki zinaa na mtu mwingine, ee Mwenyezi Mungu nisaidie"

Hii ni mbinu mpya ya kisaikolojia ambayo inaweza kusaidia sana katika kupambana na janga hili la ukimwi, kwani njia pekee inayoeneza ukimwi kiurahisi ni ngono ikisaidiwa sana na ukosefu wa uaminifu katika mahusiano. Kama kutakuwa na uaminifu utakuwa imara katika ndoa basi hata katika mahusiano ya kawaida kutakuwa na uaminifu.

Nawasilisha.
 
mkuu .... wewe umeshaoa ...! kwenye kiapo kuna sehemu inayotamka kwamba nitakuwa "muaminifu"
 
Vipi kuhusus wale ambao hajaoa au kuolewa unawafikiriaje? Maana umelenga wenye ndoa tu. Suala la mahusiano katika halihisishi ngono sio kwa walioona tu ambao itakuwa rahisi kuwaapisha hivyo.
 
Mkuu lazima ukubaliane na mimi kwamba ukimwi unachangiwa sana ukosefu wa uaminifu katika ndoa, hasa wababa mafataki wanautoa ukimwi ndani na kuupeleka nje, kama wababa na wamama wataacha kuwafuatilia vijana wadogo na wakaonesha uaminifu wa kweli bila hiyo itahamia hata kwa vijana walio katika mahusiano ya kawaida.
 
Kuna ile sehemu inayosema hivi...nakupokea uwe mume wangu wa ndoa au nakupokea uwe mke wangu wa ndoa......sasa ina maana hapa wanaacha mwanya kwa wasio wa ndoa kuwashughulikia!
 
Katika kuifikia Tanzania isiyokuwa na ukimwi kama kampeni iliyozinduliwa na Mhe. Rais miaka michache iliyopita "Tanzania bila ukimwi inawezekana" ninapendekeza kiapo cha ndoa kiwe namna hii:- "Mimi X nakubali kumuoa/kuolewa na Y awe mke/mume wangu katika maisha yangu yote, katika shida na raha na naahidi kumpenda, kumlinda katika hali yoyote ile na naahidi mbele ya Mungu, kanisa/msikiti/serikali, waamini waliopo hapa, ndugu, jamaa na marafiki kutomsaliti mwenzangu kimwili kwa kushiriki zinaa na mtu mwingine, ee Mwenyezi Mungu nisaidie"

Hii ni mbinu mpya ya kisaikolojia ambayo inaweza kusaidia sana katika kupambana na janga hili la ukimwi, kwani njia pekee inayoeneza ukimwi kiurahisi ni ngono ikisaidiwa sana na ukosefu wa uaminifu katika mahusiano. Kama kutakuwa na uaminifu utakuwa imara katika ndoa basi hata katika mahusiano ya kawaida kutakuwa na uaminifu.

Nawasilisha.
Pia sheria ipange mwanamke akionekana na mwanaume atiliwe shaka na waulizwe!.
Hata ukiwakuta watu wawili me/ke unawashitaki polisi au kuwepo vyombo husika.
Uaminifu ni jambo la kiroho....ukiwa muaminifu zipo njama au changa moto nyingi utazo fanyiwa lazima utatoka kwenye msitari(iman/uaminif) yako
 
ukimwi unaenezwa na wanawake zaidi.
Mtansamehe akina mama zangu!.
Wewe unajua unae mume wako...akija bw mwingine akutia vishawishi vile umevikosa au umepungukiwa ...unamkubali.
Hapo unategemea nini?
 
Sio sisi wanandoa ndio tubadilike? maana hata kiapo kikibadilishwa kama na sie hatujabadilika haitasaidia kitu
 
ukimwi unaenezwa na wanawake zaidi.
Mtansamehe akina mama zangu!.
Wewe unajua unae mume wako...akija bw mwingine akutia vishawishi vile umevikosa au umepungukiwa ...unamkubali.
Hapo unategemea nini?
We unachekesha kweli!Kwahiyo wanaume wametulia wamama ndo wanahangaika??Nna mifano hai...kati ya wanandoa watatu wanaotoka nje ya ndoa wawili ni wanaume!Na mmoja sio tu kamletea mkewe mtoto ila na ngoma juu!
 
Unajua kwanini nawataja akina dada?
Mwanaume hata awe fataki...akija kwenu hakuchukui bila idhin yako.
Mkatalie maombi kama utaweza...uone kama utapata upupu!.
 
Mkuu lazima ukubaliane na mimi kwamba ukimwi unachangiwa sana ukosefu wa uaminifu katika ndoa, hasa wababa mafataki wanautoa ukimwi ndani na kuupeleka nje, kama wababa na wamama wataacha kuwafuatilia vijana wadogo na wakaonesha uaminifu wa kweli bila hiyo itahamia hata kwa vijana walio katika mahusiano ya kawaida.

Nafikiri hapo kwenye red ilipaswa kuwa kinyume chake, ukimwi unatoka nje unaletwa ndani ya ndoa unless wahusika walioana wakiwa tayari waathirika.
 
Unajua kwanini nawataja akina dada?
Mwanaume hata awe fataki...akija kwenu hakuchukui bila idhin yako.
Mkatalie maombi kama utaweza...uone kama utapata upupu!.

Haya hongera kwa kugundua tatizo!Ni vizuri ukiwa unamwambia na yule DEMU wako hayo kabla yakumpeleka gheto!Maana wewe kuomba kwako kunakufanya wewe wa kwanza kuinitiate alafu unasema akatae!We unaomba ya kazi gani!Na huyo mwanaume kama sio msababishi akikubaliwa kwanini asipotezee!?
 
Teh teh teh!
Unaniumiza mbavu zangu !
Mimi sina tabia zakuomba ngono.
Ntaekua nae ntatosheka nae...kama atakua na mapungufu ntamuelimisha ...nae akinigundua nina mapungufu atanielimisha.
Tutaishi kwa raha na kwa amani.
 
Katika kuifikia Tanzania isiyokuwa na ukimwi kama kampeni iliyozinduliwa na Mhe. Rais miaka michache iliyopita "Tanzania bila ukimwi inawezekana" ninapendekeza kiapo cha ndoa kiwe namna hii:- "Mimi X nakubali kumuoa/kuolewa na Y awe mke/mume wangu katika maisha yangu yote, katika shida na raha na naahidi kumpenda, kumlinda katika hali yoyote ile na naahidi mbele ya Mungu, kanisa/msikiti/serikali, waamini waliopo hapa, ndugu, jamaa na marafiki kutomsaliti mwenzangu kimwili kwa kushiriki zinaa na mtu mwingine, ee Mwenyezi Mungu nisaidie"

Hii ni mbinu mpya ya kisaikolojia ambayo inaweza kusaidia sana katika kupambana na janga hili la ukimwi, kwani njia pekee inayoeneza ukimwi kiurahisi ni ngono ikisaidiwa sana na ukosefu wa uaminifu katika mahusiano. Kama kutakuwa na uaminifu utakuwa imara katika ndoa basi hata katika mahusiano ya kawaida kutakuwa na uaminifu.

Nawasilisha.

Yaani waafrika tumekuwa colonized mno mentally, inaonyesha wachangiaji karibu wote hapo juu hatujui wala UKIMWI ni nini, tunatamka tu.
 
Back
Top Bottom