nyakahanga
JF-Expert Member
- Mar 7, 2013
- 240
- 65
Salam aleykum wanajamvi.
Natumaini mu wazima wa afya na mnaendelea na majukumu yenu ya kujiingizia kipato. Juzi nikiwa ofisini nilifuatwa na shemeji yangu ambaye ameolewa na mdogo wangu wiki mbili tu zilizopita.
Alikuja kwa ajili ya ushauri juu ya kitu kinachomsumbua. Kitu chenyewe ni kuwa, kipindi anasoma sekondari alikuwa na mpenzi wake (si mdogo wangu) ambaye walipendana sana (si unajua mapenzi ya utotoni). Ilifika kipindi wakala kiapo cha damu, yaani kila mtu akajichanja na kulamba damu ya mwenzake.
Kadri siku zilivyoenda (kwa maelezo ya shemeji yangu) jamaa yake akaanza kubadilika na kuonesha tabia zilizomtia aibu binti wa watu kila kukicha (ulevi na uvutaji bangi). Hivyo binti alishindwa kuvumilia baada ya mfululizo wa matukio hivyo akaamua kukata shauri ya kuachana na jamaa yule.
Jamaa hakuonesha kujali kitendo cha kuachwa hivyo alichukulia poa tu na kila mtu akachukua hamsini zake. Lakini hivi karibuni baada ya jamaa kusikia ex wake anafunga ndoa ndiyo kaanza visa na maneno ya kumtishia shemeji yangu kuwa damu yake itamlilia milele!!
Hivyo shemeji alikuwa ananiomba nimpe ushauri afanyeje maana hii kauli inamuathiri psychologically (anavyodai yeye). Kusema kweli nilimwambia ashikilie imani tu hakuna kitu kibaya kitakachompata.
Japo majibu haya mimi binafsi sikuwa na uhakika nayo kabisa ikabidi nitafute muda niwaulizie wadau juu ya hii kitu. Mwenye maelezo ya kina juu ya aina hii ya kiapo anipe ufafanuzi ili niweze kuwa na nyongeza ya ushauri kwa shemeji yangu maana namwona kila siku hana raha huku mdogo wangu akihangaika kumfanyia kila kitu ili awe na furaha.
Nawasilisha.
~nyakahanga~