Sky Eclat
JF-Expert Member
- Oct 17, 2012
- 57,720
- 215,786
Familia ya watu sita, baba, mama, na watoto watatu wa kiume wa kike mmoja, mama na baba walikuwa wote career people. Mtoto wa kwanza wa kiume alikuwa chuo, wengine high school na secondary.
Ile familia ilihitaji dada wa kazi, alijitokeza binti mzuri na maridadi, dada wakujipenda flani hivi. Mama alikuwa mtu wa kusafiri sana, na hata siku alizokuwa nyumbani jikoni aliingia mara chache sana inapobidi, kwakweli mama akiwa na extra time ni wa sofa na movie. Bahati nzuri binti yake alipenda kupika, kwahiyo binti alimpa house girl company mara nyingi.
Mama alikuwa ni wa kulalamika sana, kufoka, kugomba, hata glass ya maji ya kunywa ataita nanii.. hembu niletee maji, chakula, mara nguo zangu hazikunyooshwa vizuri. Baba alijisikia vibaya sana, kama binti yake yuko tuition baba atakaa na dada jikoni atamsaidia kukata vitunguu. Mama anaanza kumuuliza we baba nanii unafanya nini huko? Atajibiwa mke wangu huyu sio kuli, nae pia ni binadamu hatuwezi kukaa tunaangalia T.V. wakati mtoto wa watu anatupikia.
Baada ya muda yule dada akawa mgonjwa, kupima ngoma ilikuwa imeitika. Tatizo lilikuwa, baba mwenyenyumba na mtoto wa kwanza wa chuo wote walikuwa wanamparamia dada kila mtu kwa muda wake. Baba na mtoto wote walikuwa +ve. Yule mama alisema kheri angekutana na mchawi kuliko yule dada alivyomtenda.