Kesi za uchaguzi wa Wabunge................... | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kesi za uchaguzi wa Wabunge...................

Discussion in 'Jukwaa la Sheria (The Law Forum)' started by Rutashubanyuma, Feb 16, 2011.

 1. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #1
  Feb 16, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,305
  Likes Received: 417,643
  Trophy Points: 280
  Nimeona kurahisisha ufuatiliaji wa kesi za uchaguzi wa wabunge kuna uhaja wa kuanzisha special thread ya kuziripoti na kuzifuatilia....................
   
 2. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #2
  Feb 16, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,305
  Likes Received: 417,643
  Trophy Points: 280

  Mpendazoe aamriwe alipe milioni 5/- za kesi

  Imeandikwa na Regina Kumba; Tarehe: 15th February 2011 @ 23:50

  MAHAKAMA Kuu imetupilia mbali maombi ya aliyekuwa mgombea ubunge wa Jimbo la Segerea kwa tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Fred Mpendazoe aliyeomba asilipe ada ya kesi ya uchaguzi kupinga matokeo katika jimbo hilo.

  Katika uamuzi wake, Jaji Profesa Juma Othman amesema sheria inamtaka anayefungua kesi ya uchaguzi kulipa ada ya Sh milioni tano.

  Jaji huyo alitupilia mbali ombi hilo la Mpendazoe na kupanga kesi hiyo kutajwa Februari 23, mwaka huu na kuangalia kama Mpendazoe amelipa ada hiyo.

  Wadaiwa katika kesi hiyo ni Mbunge wa jimbo hilo, Makongoro Mahanga (CCM), Mwanasheria Mkuu, (AG) na Msimamizi wa Uchaguzi.

  Mpendazoe amefungua kesi hiyo Namba 98 ya mwaka huu, akilalamikia ukiukwaji wa taratibu na sheria za uchaguzi katika jimbo hilo, analalamikia mwenendo mzima wa uchaguzi, mchakato wa uchaguzi katika jimbo hilo kwamba vilikiuka taratibu na sheria za uchaguzi.

  Pia, anadai mwenendo wa ukusanyaji kura kwamba ulikuwa mbovu na ujumuishaji wa kura, kuhesabu na utangazaji wa matokeo ulikiuka taratibu na sheria za uchaguzi.

  Mpendazoe anaiomba Mahakama hiyo itengue ubunge katika jimbo hilo na kuamuru ufanyike uchaguzi mdogo na kwamba kama haitaamuru uchaguzi kufanyika, atangazwe kuwa mbunge.

   
 3. T

  TULIBAHA Member

  #3
  Feb 26, 2011
  Joined: Jan 23, 2011
  Messages: 49
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 15
  alaf mi natka kujua hv wabunge wliopita bila kupingwa hiv ni wabunge kisheria? wamepata wapi legitimacy km hawajashiriki general election oct. 2010?
   
 4. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #4
  Mar 1, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,305
  Likes Received: 417,643
  Trophy Points: 280
  Kesi ya Mpendazoe, Mahanga hakieleweki


  na Happiness Katabazi


  [​IMG] MAHAKAMA Kuu Kanda ya Dar es Salaam, Machi 8 mwaka huu itatoa uamuzi wa kulikubali au kulikataa ombi la aliyekuwa mgombea ubunge wa Segerea Fred Mpendazoe (CHADEMA) la kutaka aruhusiwe kuweka sh milioni 15 mahakamani kama dhamana.
  Dhamana hiyo ni sh milioni tano kwa kila mdaiwa ambapo wadaiwa katika kesi hiyo ni Mbunge wa Segerea na Naibu Waziri wa Kazi na Ajira Dk. Makongoro Mahanga (CCM), Mwanasheria Mkuu wa Serikali na aliyekuwa msimamizi wa uchaguzi anazotakiwa kuzitoa kwa mujibu wa Sheria ya Uchaguzi ya mwaka 2002.
  Katika kesi ya msingi Mpendazoe anapinga matokeo ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2010 jimbo la Segerea yaliyomtangaza Dk. Mahanga kuwa mbunge.
  Baada ya Jaji Ibrahim Juma kusikiliza ombi la mlalamikaji na pingamizi la mawakili wa wadaiwa lililotaka ombi hilo litupwe, amesema atatoa uamuzi wa ama kukubali au kukataa ombi la Mpendazoe Machi 8.
  Awali wakili wa mlalamikaji Peter Kibatala aliiambia mahakama kuwa wamekuja na ombi jipya la kuomba mteja wake aruhusiwe kuweka kiasi hicho cha fedha kwani tayari mteja amekwishakipata.
  Hata hivyo wakili wa wadaiwa hao Jerome Msemwa alilipinga ombi hilo na kuiomba mahakama isimruhusu hadi pale mlalamikaji atakapopeleka ombi rasmi mahakamani la kuiomba impangie kiwango cha kuweka mahakamani hapo.
  Wakili Msemwa aliongeza kuwa kifungu cha 111(3) cha Sheria ya Uchaguzi kinamtaka mwombaji anayeiomba mahakama imsamehe kulipa dhamana hiyo au kumpunguzia kiwango cha kulipa, anatakiwa awasilishe ombi hilo ndani ya siku 14 tangu alipofungua kesi ya msingi ya kupinga matokeo ya ubunge.
  Akipangua hoja hiyo wakili wa Mpendazoe, Kibatala aliiambia mahakama kuwa kifungu hicho kilichotumiwa na Msemwa hakiendani na ombi lao waliloliwasilisha kwa kuwa ombi lao ni mahakama imruhusu aweke kiasi hicho cha fedha na si vinginevyo.
  Februali 15, mwaka huu, Jaji Juma alitupilia mbali ombi la Mpendazoe la kuitaka mahakama hiyo imsamehe kulipa fedha hizo kwa sababu hana uwezo wa kupata fedha hizo na kwamba alibaini hati ya kiapo cha maombi hayo kilikuwa na dosari za kisheria.
   
 5. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #5
  Mar 1, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,305
  Likes Received: 417,643
  Trophy Points: 280
  Hatma kesi ya Mpendazoe Alhamisi


  Na Kulwa Mzee

  MAHAKAMA Kuu ya Tanzania inatarajia Machi 3, mwaka huu kutoa uamuzi wa ama kumruhusu aliyekuwa mgombea ubunge Jimbo la Segerea kwa tiketi ya
  CHADEMA, Bw. Fred Mpendazoe kulipa sh. milioni 15 au kutupilia mbali kesi yake kwa kuwa yuko nje ya muda.

  Kesi hiyo ilikuwa inaendelea jana mbele ya Jaji Ibrahim Juma ambapo Wakili wa Mpendazoe, Bw. Peter Kibatala alikuwa tayari na mteja wake kulipa kiasi hicho cha fedha kwa mujibu wa sheria.

  Baada ya kuwasilisha hoja ya kulipa sh. milioni 15, Wakili wa Mbunge wa Segerea, Dkt. Makongoro Mahanga, Bw. Jerome Msemwa aliwasilisha hoja ya kupinga kulipwa kwa fedha hizo hadi mahakama iangalie ni kiasi gani kinapaswa kulipwa na kwamba walalamikaji wako nje ya muda.

  Hoja hiyo ilipingwa na Bw. Kibatala ambaye alisema Wakili Msemwa hana hoja ya msingi na kwamba malipo hayo yako kisheria, hivyo yalipwe na mwisho wa kesi wakishindwa watakaofaidika nazo ni walalamikiwa.

  Alisema fedha zinatakiwa kulipwa zote, hivyo aliiomba mahakama kuruhusu malipo hayo yafanyike ili kesi ya msingi iendelee kusikilizwa.

  Jaji Juma baada ya kusikiliza malumbano hayo ya kisheria aliahirisha kesi hadi Machi 3, mwaka huu kwa ajili ya kutoa uamuzi.

  Wadaiwa katika kesi hiyo ni Mbunge wa Segerea, Dkt. Mahanga (CCM), Mwanasheria Mkuu wa serikali na Msimamizi wa Uchaguzi.

  Bw. Mpendazoe alifungua kesi hiyo Namba 98 ya mwaka jana, akilalamikia ukiukwaji wa taratibu na sheria za uchaguzi katika jimbo hilo, analalamikia mwenendo mzima wa uchaguzi, mchakato wa uchaguzi katika jimbo hilo kwamba vilikiuka taratibu na sheria za uchaguzi.

  Pia, anadai mwenendo wa ukusanyaji kura ulikuwa mbovu na ujumlishaji wa kura, kuhesabu na utangazaji wa matokeo ulikiuka taratibu na sheria za uchaguzi.

  Anaiomba mahakama hiyo itengue ubunge katika jimbo hilo na kuamuru ufanyike uchaguzi mdogo au atangazwe yeye kuwa mbunge.

  Awali, Bw. Mpendazoe aliomba mahakama hiyo imsamehe malipo ya sh milioni 15 (sh milioni 5 kwa kila mlalamikiwa) kwa kuwa hana uwezo huo, lakini ombi hilo lilitupiliwa mbali na mahakama, ikidaiwa ni hitaji la kisheria.

  [​IMG]
   
 6. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #6
  Mar 1, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,305
  Likes Received: 417,643
  Trophy Points: 280
  PHP:
  alaf mi natka kujua hv wabunge wliopita bila kupingwa hiv ni wabunge kisheriawamepata wapi legitimacy km hawajashiriki general election oct2010?
  Ni mpaka ipingwe mahakamani na tafsiri sahihi ya kisheria kupatikana huko..........................
   
 7. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #7
  Mar 5, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,305
  Likes Received: 417,643
  Trophy Points: 280
  Mbatia kumuongeza Mdee mshitakiwa mwingine


  na Happiness Katabazi


  [​IMG] MAHAKAMA Kuu Kanda ya Dar es Salaam, imekubali ombi la aliyekuwa mgombea ubunge wa Jimbo la Kawe kwa tiketi ya NCCR-Mageuzi, James Mbatia, la kutaka mahakama hiyo imruhusu kuondoa mahakamani hati yake ya madai ili aende kuifanyia marekebisho na kisha kuirejesha upya mahakamani hapo.
  Katika kesi hiyo ya kupinga matokeo ya uchaguzi ya Jimbo la Kawe, yenye namba 111/2010, Mbatia anamlalamikia Mwanasheria Mkuu wa Serikali na Mbunge wa jimbo hilo, Halima Mdee (CHADEMA) ambaye hata hivyo hakuwepo mahakamani jana.
  Amri hiyo ya kukubali ombi la Mbatia ilitolewa jana na Msajili wa Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam, Amir Msumi, ambapo aliwataka mawakili wa Mbatia, Mohamed Tibanyendera na Aloyce Komba wawasilishe hati mpya Machi 8 na kesi hiyo itakuja kutajwa Machi 10, mwaka huu.
  Awali mapema jana asubuhi wakili Tibanyendera na Komba waliiambia mahakama kuwa kesi hiyo ilikuja kwa ajili ya kutajwa ila mlalamikaji (Mbatia) anawasilisha ombi la kuomba kuiondoa hati ya madai ili aende kuifanyia marekebisho kwani kwa mujibu wa mabadiliko ya kanuni, kesi za uchaguzi uliofanyika mwaka 2010, yanalazimisha msimamizi wa uchaguzi wa jimbo husika naye afunguliwe kesi, jambo ambalo katika hati yao ya madai hawakuwa wamemshitaki.
  Tibanyendera alieleza kuwa kwa mujibu wa kanuni za zamani za sheria ya uchaguzi ya mwaka 2002 kabla hazijafanyiwa mabadiliko mwaka jana, mlalamikaji alikuwa akiruhusiwa kumshitaki mbunge aliyeshinda katika jimbo husika na Mwanasheria Mkuu wa Serikali aliyekuwa akishitakiwa kwa niaba ya msimamizi wa uchaguzi wa jimbo.
  "Kwa maelezo hayo ya kisheria, mteja wetu (Mbatia) anaomba abadilishe hati yake ya madai ya awali ili aweze kumuongeza msimamizi wa uchaguzi wa Jimbo la Kawe, kwa hiyo katika hati hiyo mpya tutakayoiwasilisha Jumatatu ijayo wadaiwa watakuwa ni watatu na si wawili tena.
  "Na sababu ya pili ya mteja wetu kuiondoa hati hiyo akaifanyie marekebisho ni kwamba wapiga kura wawili wa jimbo hilo wamejitokeza na kuungana na Mbatia katika kesi hiyo dhidi ya Mdee," alidai wakili Tibanyendera.
  Novemba 25, mwaka 2010 Mbatia alifungua kesi ya kupinga matokeo ya ubunge wa jimbo hilo ambayo yalimtangaza Halima Mdee (CHADEMA) kuwa ndiye aliyeshinda na ataliongoza jimbo hilo kwa kipindi cha miaka mitano.
   
 8. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #8
  Mar 5, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,305
  Likes Received: 417,643
  Trophy Points: 280
  PHP:
  "Kwa maelezo hayo ya kisheria, mteja wetu (Mbatia)  anaomba abadilishe  hati yake ya madai ya awali ili aweze kumuongeza  msimamizi wa uchaguzi  wa Jimbo la Kawe, kwa hiyo katika hati hiyo mpya  tutakayoiwasilisha  Jumatatu ijayo wadaiwa watakuwa ni watatu na si  wawili tena.
  Shame on you Mbatia............................
   
 9. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #9
  Mar 5, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,305
  Likes Received: 417,643
  Trophy Points: 280
  Msimamizi wa Uchaguzi Kawe kuunganishwa kesi ya Mbatia Send to a friend Saturday, 05 March 2011 09:26

  Tausi Ally
  MAHAKAMA Kuu Kanda ya Dar es Salaam, imeagiza Mkurugenzi wa Manispaa ya Kinondoni, ajumuishwe kesi ya kupinga matokeo ya ubunge wa Jimbo la Kawe iliyofunguliwa na aliyekuwa mgombea kupitia Chama cha NCCR Mageuzi, Joseph Mbatia.
  Mbatia alifungua kesi hiyo akipinga matokeo yaliyompa ushindi aliyekuwa mgombea kupitia Chadema, Halima Mdee.Walalamikiwa wengine katika kesi hiyo, ni Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG).
  Lakini, jana Msajili wa Wilaya wa Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam, Amir Msumi, aliagiza Mkurugenzi wa Manispaa ya Kinondoni ambaye ndiye msimamizi wa Uchaguzi wa jimbo hilo aunganishwe katika kesi hiyo.
  Msumi alitoa agizo hilo kufuatia maombi yaliyotolewa mahakamani hapo na wakili Mbatia, Mohamed Tibanyendela, wakati ilipotajwa kwa mara ya kwanza.Tibanyendela aliomba mahakama hiyo imruhusu kufanya marekebisho katika hati yao ya madai ili kumuongeza msimamizi wa uchaguzi wa jimbo hilo, ikiwamo kuwaongeza walalamikaji wengine wawili ambao wanapinga matokeo hayo.
  Alidai kuwa walalamikaji hao ambao ni wakazi wa jimbo la Kawe, ni Hemed Kanoni na Solomon Lufunda, ambao pia wameomba kuungana na Mbatia kupinga matokeo ya uchaguzi huo.Tibanyendera alidai kuwa wanafanya mabadiliko hayo kwa sababu walikuwa hawajui kama kuna sheria ndogo ndogo zinazosimamia uchaguzi ambazo zinawalazimisha kumuongeza Msimamizi wa Uchaguzi kwenye hati ya madai yao.
  Mbatia kupitia mawakili wake, Tibanyendera na Aloyce Komba, Novemba 25, mwaka jana walifungua kesi ya madai namba 111 kupinga matokeo ya uchaguzi uliofanyika Oktoba 31, mwaka jana yaliyompa ushindi Mdee.
  Kutokanana na mabadiliko hayo, waliomba kuondoa hati ya madai ya awali na kuwasilisha mpya iliyofanyiwa mabadiliko.
  Msumi aliwataka kuwasilisha hati hiyo Machi 8, mwaka huu na kwamba Machi 10, mwaka huu kesi itatajwa.
  Hata hivyo mawakili hao, waliiomba mahakama iwape maelekezo ya jinsi ya kulipa ada ya kuendesha kesi hiyo ya uchaguzi. Kwa mujibu wa sheria ya uchaguzi iliyopo sasa inamtaka mtu kutoa Sh5 milioni kwa kila anayelalamikiwa. Kwa hali hiyo Mbatia atatakiwa kutoa cha Sh15 milioni.
   
 10. BongoLogik

  BongoLogik JF-Expert Member

  #10
  Mar 5, 2011
  Joined: Aug 10, 2009
  Messages: 261
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Hivi huyu Mbatia sababu zake za kupinga ni nini hasa?
   
 11. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #11
  Mar 9, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,305
  Likes Received: 417,643
  Trophy Points: 280
  Tundu Lissu ‘kidedea' mahakamani Send to a friend Tuesday, 08 March 2011 20:16

  Habel Chidawali, Dodoma

  MAHAKAMA Kuu Kanda ya Dodoma, jana ilifutilia mbali kesi iliyokuwa ikimkabili Mbunge wa Singida Mashariki Tundu Lissu (Chadema) na kusema kuwa kesi hiyo ilifunguliwa kimakosa hivyo haiwezi kuendelea kusikilizwa.

  Jaji Sivangilwa Mwangesi,alisema kuwa kesi hiyo ilikuwa na kasoro nyingi kutokana na vifungu vya kisheria na akasema haiwezi kuendelea kusikilizwa mahakamani hapo.
  Kesi hiyo ilifunguliwa na wanachama wawili wa CCM, Shaban Itambu na Pascal Hallu ambao wamewafungulia kesi ya kupinga matokeo Mbunge wa Singida Mashariki, Tindu Lissu, msimamizi wa uchaguzi na mwanasheria wa serikali.

  Hata hivyo wakati kesi hiyo ikifutwa jana, Lissu mwenyewe hakuwepo mahakamani baada ya kuelezwa kuwa aliharibikiwa na gari akiwa njiani kuja Dodoma ambapo aliwakilishwa na ndugu yake Samson Mkotya ambaye alisema kuwa mbunge huyo alikuwa Morogoro baada ya juzi kuharibikiwa na gari lake.

  Kufutwa kwa kesi hiyo ni ushindi kwa Tundu Lissu ambaye tangu mwanzo wa kesi hiyo alionekana kujiamini zaidi na kusema kuwa kesi hiyo ingeishia katika hatua za mwanzo bila ya kufika mbali.

  "Mimi nasema kuwa,kesi hii naisimamia mwenyewe na ninatambua kuwa haiwezi kufika mahali popote kwa kuwa imejaa makosa mengi ya kisheria ambayo kimsingi kama Jaji ataamua kufuata haki hakuna kesi hapa," alisema Lissu siku alipowasilisha ombi la kufutwa kwa kesi hiyo.

  Mbunge huyo ambaye kitaaluma ni mwanasheria aliwasilisha kumbukumbu za hukumu za kesi nyingi ambazo zilifunguliwa kwa mtindo huo ambazo alisema kuwa yeye (Lissu) alizisimamia lakini alishindwa.

  Baadhi ya kesi alizonukuu Lissu ni pamoja na kesi ya John Mnyika na Charles Keenja, Joyce Chitende na Zainabu Gama, John Jomba na Christopher Ole-Sendeka ambazo alisema kuwa zote zilifunguliwa kwa mtindo huo lakini zilishindwa kuendelea.

  Jana Jaji Silivangira alisema licha ya Kifungu cha 111 (b) ambacho Lissu alisema kuwa kimekosewa kutokuwa na mapungufu ya moja kwa moja, lakini kwa kutumia sheria hiyo katika kifungu 112 (a),(b) bado ufunguaji wa kesi hiyo ulionekana kuwa na makosa.

  Moja ya vitu ambayo Lissu alitaka viwekwe ni pamoja na wadai hao kulipa gharama za kesi ya uchaguzi ambazo walishindwa kuzilipa,kingine ni pamoja na kufutilia mbali ombi la wadai walilotaka kusamehewa kulipa gharama hizo akidai kuwa kama hawana fedha wasingeweza kuweka mawakili.

  Kwa upande wao Mawakili waliokuwa wakisimamia kesi hiyo kwa upande wa wadai kampuni ya Uwakili la Wasonga walishindwa kuzungumza chochote kwani mara baada ya kumalizika kwa kesi hiyo waliondoka mahakamani hapo.  Comments
  +1 #3 kangaroo 2011-03-09 15:41 wawaw fagilia braza
  Quote

  +2 #2 mekaki 2011-03-09 13:39 hahah hahha a ccm mlidhanai mahamaani pia kuna ufisadi? si mahakama zote.haki imetendeka lol1
  Quote

  +2 #1 Debora 2011-03-09 13:07 Haki imetendeka kaka Lissu. Hongera.
  Quote
   
 12. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #12
  Mar 9, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,305
  Likes Received: 417,643
  Trophy Points: 280
  Tundu Lissu ‘kidedea’ mahakamani Send to a friend Tuesday, 08 March 2011 20:16

  Habel Chidawali, Dodoma

  MAHAKAMA Kuu Kanda ya Dodoma, jana ilifutilia mbali kesi iliyokuwa ikimkabili Mbunge wa Singida Mashariki Tundu Lissu (Chadema) na kusema kuwa kesi hiyo ilifunguliwa kimakosa hivyo haiwezi kuendelea kusikilizwa.

  Jaji Sivangilwa Mwangesi,alisema kuwa kesi hiyo ilikuwa na kasoro nyingi kutokana na vifungu vya kisheria na akasema haiwezi kuendelea kusikilizwa mahakamani hapo.
  Kesi hiyo ilifunguliwa na wanachama wawili wa CCM, Shaban Itambu na Pascal Hallu ambao wamewafungulia kesi ya kupinga matokeo Mbunge wa Singida Mashariki, Tindu Lissu, msimamizi wa uchaguzi na mwanasheria wa serikali.

  Hata hivyo wakati kesi hiyo ikifutwa jana, Lissu mwenyewe hakuwepo mahakamani baada ya kuelezwa kuwa aliharibikiwa na gari akiwa njiani kuja Dodoma ambapo aliwakilishwa na ndugu yake Samson Mkotya ambaye alisema kuwa mbunge huyo alikuwa Morogoro baada ya juzi kuharibikiwa na gari lake.

  Kufutwa kwa kesi hiyo ni ushindi kwa Tundu Lissu ambaye tangu mwanzo wa kesi hiyo alionekana kujiamini zaidi na kusema kuwa kesi hiyo ingeishia katika hatua za mwanzo bila ya kufika mbali.

  "Mimi nasema kuwa,kesi hii naisimamia mwenyewe na ninatambua kuwa haiwezi kufika mahali popote kwa kuwa imejaa makosa mengi ya kisheria ambayo kimsingi kama Jaji ataamua kufuata haki hakuna kesi hapa," alisema Lissu siku alipowasilisha ombi la kufutwa kwa kesi hiyo.

  Mbunge huyo ambaye kitaaluma ni mwanasheria aliwasilisha kumbukumbu za hukumu za kesi nyingi ambazo zilifunguliwa kwa mtindo huo ambazo alisema kuwa yeye (Lissu) alizisimamia lakini alishindwa.

  Baadhi ya kesi alizonukuu Lissu ni pamoja na kesi ya John Mnyika na Charles Keenja, Joyce Chitende na Zainabu Gama, John Jomba na Christopher Ole-Sendeka ambazo alisema kuwa zote zilifunguliwa kwa mtindo huo lakini zilishindwa kuendelea.

  Jana Jaji Silivangira alisema licha ya Kifungu cha 111 (b) ambacho Lissu alisema kuwa kimekosewa kutokuwa na mapungufu ya moja kwa moja, lakini kwa kutumia sheria hiyo katika kifungu 112 (a),(b) bado ufunguaji wa kesi hiyo ulionekana kuwa na makosa.

  Moja ya vitu ambayo Lissu alitaka viwekwe ni pamoja na wadai hao kulipa gharama za kesi ya uchaguzi ambazo walishindwa kuzilipa,kingine ni pamoja na kufutilia mbali ombi la wadai walilotaka kusamehewa kulipa gharama hizo akidai kuwa kama hawana fedha wasingeweza kuweka mawakili.

  Kwa upande wao Mawakili waliokuwa wakisimamia kesi hiyo kwa upande wa wadai kampuni ya Uwakili la Wasonga walishindwa kuzungumza chochote kwani mara baada ya kumalizika kwa kesi hiyo waliondoka mahakamani hapo.  Comments
  +1 #3 kangaroo 2011-03-09 15:41 wawaw fagilia braza
  Quote

  +2 #2 mekaki 2011-03-09 13:39 hahah hahha a ccm mlidhanai mahamaani pia kuna ufisadi? si mahakama zote.haki imetendeka lol1
  Quote

  +2 #1 Debora 2011-03-09 13:07 Haki imetendeka kaka Lissu. Hongera.
  Quote
   
 13. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #13
  Mar 9, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,305
  Likes Received: 417,643
  Trophy Points: 280
  Korti yakubali ombi la Mpendazoe, Lissu kidedea


  na Danson Kaijage


  [​IMG] HATIMAYE Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam, imekubali ombi la aliyekuwa mgombea ubunge jimbo la Segerea, Fred Mpendazoe (CHADEMA), la kutaka mahakama imruhusu aweke sh milioni 15 mahakamani kama dhamana.
  Dhamana hiyo ni kwa kila mdaiwa ambapo wadaiwa katika kesi hiyo ni mbunge wa Segerea na Naibu Waziri wa Kazi na Ajira, Dk. Makongoro Mahanga (CCM), Mwanasheria Mkuu wa Serikali na aliyekuwa Msimamizi wa Uchaguzi anazotakiwa kuzitoa kwa mujibu wa Sheria ya Uchaguzi ya mwaka 2010.
  Uamuzi huo ulitolewa jana na Jaji Profesa Ibrahimu Juma ambapo alisema anakubaliana na ombi lilowasilishwa na wakili wa Mpendazoe, Peter Kibatala, lililoiomba mahakama hiyo iwaruhusu kuweka kiasi hicho cha fedha kwa sababu ombi hilo limekidhi matakwa ya kisheria.
  "Mahakama inakubaliana na ombi la mlalamikaji (Mpendazoe) na linalitupilia mbali pingamizi la mdaiwa (Dk. Mahanga) na wenzake kwa sababu kifungu cha sheria walichokitumia kuwasilisha pingamizi hilo si sahihi na hakiendani na ombi la mlalamikaji.
  "… kwa maana hiyo mahakama imemruhusu mlalamikaji kuwasilisha kiasi hicho cha fedha na ndipo kesi ipangwe tarehe ya kuanza kusikilizwa," alisema Jaji Juma.
  Februari 28 mwaka huu, wakili wa Mpendazoe, Peter Kibatala aliwasilisha ombi jipya la kuomba mteja wake aruhusiwe kuweka kiasi hicho cha fedha kwani tayari mteja amepata kiasi hicho cha fedha.
  Katika kesi ya msingi Mpendazoe anapinga matokeo ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2010 katika jimbo la Segerea yaliyomtangaza Dk. Mahanga kuwa mbunge wa jimbo hilo.
  Katika katua nyingine, Mahakama Kuu Kanda ya Dodoma imetupilia mbali maombi ya kuondoa ama kusamehewa dhamana za gharama za uendeshaji kesi za uchaguzi, yaliyofunguliwa na wanachama wawili wa CCM dhidi ya mbunge wa Singida Mashariki, Tindu Lissu (CHADEMA).
  Hukumu hiyo ilitolewa jana na Jaji Silivangira Mwangesi na kuongeza kuwa Lissu ameshinda kesi hiyo kutokana na kutofuatwa kwa utaratibu wakati wa kufungua kesi hiyo.
  Hata hivyo, hukumu hiyo ilitolewa wakati Lissu hakuwepo mahakamani. Mlalamikiwa huyo aliwakilishwa na ndugu yake aliyejitambulisha kwa jina la Samson Mkotya ambaye alidai alifanya hivyo kwa kuwa Lissu aliharibikiwa na gari mkoani Morogoro.
  Maombi hayo yaliwasilishwa na wanachama wawili wa CCM, Shaban Itambu na Pascal Hallu ambao wamewafungulia kesi ya kupinga matokeo ya ubunge jimbo la Singida Mashariki, Tindu Lissu, Msimamizi wa Uchaguzi na Mwanasheria wa Serikali.
  Hata hivyo, Lissu alipinga maombi hayo kwa sababu waombaji hawakuwasilisha maombi ya kutaka kupangiwa dhamana ya gharama za uendeshaji kesi za uchaguzi.
  Lissu aliwasilisha hukumu za kesi tatu ambazo mahakama kuu iliwahi kuzitupa baada ya walalamikaji kutowasilisha kwanza maombi ya kupangiwa dhamana hiyo.
  Hukumu zilizowasiliswa na Lissu ni ya John Mnyika na Charles Keenja, Joyce Chitende na Zainabu Gama, John Jomba Koyo na Christopher Ole Sendeka.
  Akipinga pingamizi hilo, wakili wa walalamikiwa hao ni Abdallah Possi, alisema si lazima Jaji akubaliane na hukumu hizo ambazo zimetolewa na majaji wenzake wa mahakama hiyo.  [​IMG]
   
 14. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #14
  Apr 6, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,305
  Likes Received: 417,643
  Trophy Points: 280
  Kesi ya Ng'umbi, Mnyika kusikilizwa Aprili 8


  na Happiness Katabazi


  [​IMG] MAHAKAMA Kuu Kanda ya Dar es Salaam, Ijumaa ya wiki hii itasikiliza ombi dogo la aliyekuwa mgombea Ubunge wa Jimbo la Ubungo (CCM) Hawa Ng'umbi la kuomba mahakama hiyo impatie msamaha wa kutolipa sh milioni 15 kama dhamana ya kesi yake ya kupinga ubunge wa mbunge wa Jimbo hilo (CHADEMA), John Myika.
  Ng'umbi katika kesi ya kupinga matokeo ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2010 yaliyomtangaza Mnyika kuwa mshindi, ana mshitaki Mwanasheria Mkuu wa Serikali, John Mnyika na aliyekuwa msimamizi wa uchaguzi wa jimbo hilo, ambapo Mnyika anatetewa na wakili wa kujitegemea, Edson Mbogoro.
  Ng'umbi alifungua kesi Na. 107/2010 Machi 22, mwaka huu, akitaka mahakama itengue ushindi wa Mnyika kwasababu sheria ya uchaguzi ilikiukwa.
  Msajili wa Wilaya wa Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam, Amir Msumi, aliyasema hayo jana wakati kesi hiyo ilipotajwa na kusema kwamba tayari uongozi wa kesi hiyo umeishampanga jaji wa kuisikiliza, ambapo kesi hiyo itasikilizwa na Jaji Upendo Msuya.
  Juzi Mnyika aliwasilisha pingamizi mahakamani hapo dhidi ya ombi hilo dogo la mlalamikaji (Ng'umbi) la kutaka asamehewe kiasi hicho cha fedha.
  Mnyika aliiomba mahakama itupilie mbali ombi la mlalamikaji kwa sababu mlalamikaji ana uwezo wa kulipa kiasi hicho cha fedha kama sheria ya uchaguzi ya mwaka 2002 inavyomtaka mlalamikaji katika kesi ya uchaguzi kuweka mahakamani sh milioni tano kwa kila mdaiwa anayemshitaki.
   
 15. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #15
  Apr 9, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,305
  Likes Received: 417,643
  Trophy Points: 280
  Saturday April 09, 2011 Local News
  High Court adjourns petition case against Mnyika

  By JULIUS BWAHAMA, 8th April 2011 @ 12:00, Total Comments: 0, Hits: 73

  DEFEATED Ubungo Chama Cha Mapinduzi (CCM) parliamentary candidate, Hawa Ng'umbi has requested the High Court to waive a 5m/- bond required to file the case.

  Ms Ng'umbi who lost to Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) candidate, John Mnyika, said she is in no position to raise the bond money.

  High Court Registrar, Amir Msumi, however, yesterday adjourned the case till next Friday when a ruling will be made on the request.

  The court received the application in writing before the Registrar, Mr Msumi set next Friday as the date the court shall hear Ng'umbi's submission orally.

  Ng'umbi filed the case last year disputing the parliamentary election results in Ubungo constituency, in which the Chadema candidate emerged the eventual winner.

  Apart from Mnyika, Ms Ng'umbi also filed a case against the Attorney General and the Ubungo National Electoral Commission (NEC) returning officer.

  According to court reports, Ng'umbi wanted the cost lifted because she could not afford it.
  Previously, Mnyika had opposed Ng'umbi's application.

  According to him, the petitioner was able to pay the 15m/- because she is the Bukombe District Commissioner in Shinyanga and that she also holds other government posts, a fact that she was in possession to clear the bill.

  Last week, the case was adjourned because Mnyika had complained before the court that his counsel had not received the case file from the petitioner, therefore they needed sometime to go through the file.

  According to the new election petition law, a complainant in any case is to pay the court a security bond worth 5m/- for each respondent in a case, therefore Ng'umbi was required to pay 15m/- in total.
   
 16. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #16
  Apr 9, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,305
  Likes Received: 417,643
  Trophy Points: 280
  PHP:
  Last weekthe case was adjourned because Mnyika had complained  before  the court that his counsel had not received the case file from  the  petitionertherefore they needed sometime to go through the file
  Does this contention makes sense..............................kama hawajalipata faili watawezaje kulipitia?????????????????
   
 17. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #17
  Apr 16, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,305
  Likes Received: 417,643
  Trophy Points: 280
  Kesi ya Mpendazoe Vs Dk. Mahanga yafika patamu


  na Happiness Katabazi


  [​IMG] MAHAKAMA Kuu Kanda ya Dar es Salaam, Mei 25, 26 na 27 itaanza rasmi kusikiliza kesi ya kupinga matokeo ya uchaguzi wa ubunge jimbo la Segerea uliofanyika mwaka jana yaliyomtangaza Naibu Waziri wa Kazi na Ajira, Dk. Makongoro Mahanga, kuwa mbunge, iliyofunguliwa na aliyekuwa mgombea ubunge wa jimbo hilo kwa tiketi ya (CHADEMA), Fred Mpendazoe.
  Mbali na Dk. Mahanga washtakiwa wengine ni Mwanasheria Mkuu wa Serikali na aliyekuwa msimamizi wa uchaguzi wa jimbo hilo.
  Katika madai yake mlalamikaji ambaye ni Mpendazoe anataka Mahakama Kuu itengue ushindi wa Dk. Mahanga kwa kuwa taratibu za sheria ya uchaguzi ya mwaka 2010 hazikufuatwa.
  Kwa mujibu wa hati ya wito wa kuitwa mahakamani iliyotolewa na mahakama hiyo ambayo gazeti hili limefanikiwa kuona nakala yake, wahusika wa pande zote katika kesi hiyo wameshapewa nakala ya wito huo, wakitakiwa kufika mahakamani hapo siku hiyo mbele ya Jaji Ibrahim Juma.
  Kwa upande wake wakili wa Mpendazoe, Peter Kibatala, alilithibitishia gazeti hili jana kwamba tayari ameshapokea wito huo kwa niaba ya mteja wake na kwamba watafika bila kukosa siku hiyo ambapo kesi yao itaanza kuunguruma rasmi.
  Kesi ya Mpendazoe ni kesi ya kwanza kati ya kesi tisa za kupinga matokeo ya uchaguzi wa ubunge wa mwaka 2010 kufikia hatua hiyo ya juu ya kuanza kusikilizwa. Kesi nyingine za aina hiyo bado ziko katika hatua za awali mbele ya Msajili wa Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam.
   
 18. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #18
  Apr 21, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,305
  Likes Received: 417,643
  Trophy Points: 280
  Mnyika aomba korti ifute kesi ya Ng'umbi


  na Happiness Katabazi


  [​IMG] MBUNGE wa Jimbo la Ubungo (CHADEMA), John Mnyika, ameiomba Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam itupilie mbali kesi ya kupinga ubunge wake iliyofunguliwa na aliyekuwa mgombea ubunge (CCM), Hawa Ng'umbi, kwa madai kuwa hati ya madai haina mantiki kisheria na tuhuma zilizotolewa dhidi yake zinafedhehesha na haziwezi kufanyiwa utetezi.
  Mbali na Mnyika, Ng'umbi ambaye pia ni Mkuu wa Wilaya ya Bukombe, katika kesi hiyo anamshitaki Mwanasheria Mkuu wa Serikali na aliyekuwa msimamizi wa uchaguzi wa jimbo hilo.
  Ng'umbi ambaye anatetewa na wakili Issa Maige, alifungua kesi hiyo namba 107/2010 Machi 22 mwaka huu, akitaka mahakama hiyo itengue ushindi wa Mnyika kwa sababu sheria ya uchaguzi ilikiukwa. Katika kesi hiyo Mnyika kuanzia sasa anatetewa na wakili wa kujitegemea, Tundu Lissu na Edson Mbogoro.
  Mnyika kupitia mawakili wake hao aliwasilisha kwa maandishi majibu yake kuhusu madai ya Ng'umbi juzi mahakamani hapo.
  Katika majibu yake hayo, Mnyika pamoja na mambo mengine ameiomba mahakama ifute kesi hiyo kwani madai mbalimbali yaliyotolewa yakiwamo ya matokeo ya uchaguzi hayajatolewa vielelezo vyovyote kama fomu za matokeo katika vituo vya kupigia kura kuthibitisha ukiukwaji wa taratibu.
  "Hati ya madai haizionyeshi hizo fomu za matokeo katika vituo vya kupigia kura na jinsi taratibu za uchaguzi zilivyokiukwa. Hoja hiyo inakinzana na kifungu cha 79A(3) cha Sheria ya Taifa ya Uchaguzi Sura ya 343 kama ilivyofanyiwa marekebisho mwaka 2010.
  "Naomba mahakama hii ifute kesi ya msingi iliyofunguliwa na mlalamikaji dhidi yangu na wenzangu kwa sababu madai yote anayotuhumu hajaambatanisha na vielelezo kwamba karatasi za matokeo katika vituo vya uchaguzi zilikosewa na kusababisha kumtangaza Mnyika ndiye mshindi… hati ya madai ya kesi hiyo haina mantiki kisheria," alidai Mnyika kwenye nakala ya majibu yake ambayo gazeti hili linayo," alisema Mnyika katika majibu yake hayo.
  Aprili 18 mwaka huu, Jaji Upendo Msuya, alitoa uamuzi wa ombi lililowasilishwa na Ng'umbi la kutaka mahakama hiyo impunguzie dhamana ya kesi ambayo kwa mujibu wa sheria alipaswa alipe jumla ya shilingi milioni 15 kwa sababu kila mdaiwa mmoja mlalamikaji analazimika kumuwekea dhamana ya shilingi milioni tano.
  Akitoa uamuzi huo, Jaji Msuya alimpunguzia dhamana hiyo na kumwamuru alipe shilingi milioni tatu kwa kila mdaiwa miongoni mwa hao watatu, hivyo kufanya jumla ya dhamana inayopaswa kulipwa kuwa shilingi milioni tisa. Dhamana hiyo inapaswa kulipwa ndani ya siku 14 kuanzia siku mahakama hiyo ilipotoa uamuzi huo.  [​IMG]
   
 19. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #19
  Apr 28, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,305
  Likes Received: 417,643
  Trophy Points: 280
  Mahakama yampunguzia Mbatia ada ya kesi yake Send to a friend Wednesday, 27 April 2011 21:32

  James Magai
  MAHAKAMA Kuu Kanda ya Dar es Salaam, imempunguzia Mwenyekiti wa Chama Cha NCCR-Mageuzi, James Mbatia na wanachama wawili wa chama hicho, ada ya kuendesha kesi yake dhidi ya Mbunge wa Jimbo la Kawe, Halima Mdee.

  Katika kesi hiyo, Mbatia ambaye alikuwa mgombea wa kiti hicho, uchaguzi mkuu mwaka jana, alifungua kesi kupinga ushindi wa Mdee.Sheri ya Uchaguzi inamtaka mlalamikaji kuweka mahakamani dhamana ya Sh5 milioni kwa kila mlalamikiwa.

  Kwa msingi huo, Mbatia kupitia kwa wakili wake, Mohamed Tibanyendela, aliwasilisha maombi mahakamani hapo akiomba mahakama kumpangia kiwango cha chini itakachoona kinafaa.

  Hata hivyo, sheria hiyo pia inatoa nafasi kwa mlalamikaji kuomba kusamehewa au kupangiwa kiwango cha chini zaidi ya hicho kilichotajwa kwa kadri mahakama itakavyoona kulingana na mazingira ya kesi husika.

  Lakini, Mbatia aliwasilisha maombi mahakamani hapo kupitia kwa wakili wake, Tibanyendela akiiomba mahakama kumpunguzia kiasi hicho, badala yake alipe Sh1 milioni kwa kila mlalamikiwa.

  Katika maombi hayo, licha ya mambo mengine, Mbatia alidai hivi sasa hana uwezo wa kulipa kiasi hicho kwa sababu ametoka kwenye kampeni za uchaguzi huo.

  Wanachama wengine wa chama hicho ambao waliomba kuunganishwa na Mbatia kwenye kesi hiyo, Hemed Kanoni na Solomon Lufunda, waliomba mahakama kuwasamehe kulipa kiasi chochote cha dhamana kwa madai kuwa, hawana uwezo huo kwa sababu ni wakulima.

  Akitoa uamuzi huo jana, Jaji John Utamwa, alitupilia mbali maombi ya Mbatia kutaka alipe Sh1 milioni kwa kila mlalamikiwa, na walalamikaji wenzao kutokulipa kabisa kwa sababu zao hazina msingi.Jaji Utamwa aliwapunguzia kiwango hicho na kuwataka kulipa Sh3 milioni kwa kila mlalamikiwa wote kwa pamoja.

  Kwa uamuzi huo, Mbatia na wenzake wanapaswa kulipa Sh9 milioni kama dhamana ya kesi yao, badala ya Sh15 milioni, ndani ya siku kumi 14 tangu kutolewa kwa uamuzi huo ili kesi iweze kupangiwa siku ya kusikiliza.
  
Katika kesi hiyo, Mbatia anapinga ushindi wa Mdee, anachodai kuwa Mdee wakati wa kampeni alitoa tuhuma za uongo kwamba Mbatia alikuwa akipewa Sh80 milioni na CCM, mambo ambayo anadai yalimwathiri katika upigaji kura.
   
 20. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #20
  Apr 28, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,305
  Likes Received: 417,643
  Trophy Points: 280
  Mbatia kulipa mil. 9/- kumpinga Mdee


  Na Rehema Mohamed

  MAHAKAMA Kuu Kanda ya Dar es Salaam imewataka walalamikaji katika kesi ya kupinga uchaguzi iliyofunguliwa na Mwenyekiti wa chama cha NCCR-Mageuzi, Bw. James
  Mbatia na wenzake dhidi ya Mbunge wa Jimbo la Kawe Bi. Halima Mdee kulipa jumla ya sh. milioni 9 kama gharama ya dhamana ya kesi hiyo.

  Uamuzi huo umetolewa jana na Jaji wa Mahakama hiyo, Bw. John Utamwa wakati kesi hiyo ilipofikishwa mahakamani hapo kwa ajili ya kuanza kusikilizwa.

  Bw. Utamwa alisema kuwa kila mlalamikaji atatakiwa kulipa sh. milioni 3 kwa kila mshtakiwa badala ya milioni 5/- kama sheria inavyosema. Wanaoshtakiwa katika kesi hiyo, ni Bi. Mdee, Msimamizi wa Uchaguzi na Mwanasheria Mkuu wa Serikali.

  Awali Bw. Mbatia aliiomba mahakama hiyo impunguzie kutoka sh. milioni 5 na badala yake alipe milioni moja kwa kila mshtakiwa kama dhamana ya kesi hiyo na wenzake kuomba kusamehewa kulipa fedha hizo, ambapo Bw. Utamwa alisema maombi hayo hayakuonesha sababu ya msingi ya kuwa hawana uwezo wa kulipa dhamana iliyopangwa kisheria.

  Alisema kuwa mawakili wa pande zote mbili walionesha nia ya kupunguzwa kwa kiasi hicho cha fedha za dhamana ambapo walipanga walalamikaji walipe kati ya sh. milioni 1 hadi 2.5.

  Alisema kutokana na maombi yaliyowasilishwa kwake aliamua kupanga kiasi cha sh. milioni 3 kwa kila mlalamikaji kama malipo ya dhamana ya kesi hiyo.

  Kesi hiyo imeahirishwa hadi Mei 17, mwaka huu itakapotajwa tena ambapo kiasi hicho cha fedha kinahitajika kulipwa kabla ya tarehe hiyo, ili iendelee kusikilizwa.

  Bw. Mbatia kupitia mawakili wake, Bw. Mohamed Tibanyendera na Bw. Aloyce Komba, Novemba 25, mwaka jana walifungua kesi ya madai namba 111 kupinga matokeo ya uchaguzi uliofanyika Oktoba 31, mwaka jana yaliyompa ushindi Bi. Mdee.
  [​IMG]
   
Loading...