Elections 2010 Kesi za Ubunge..................mahakama yatoa onyo..........

Rutashubanyuma

JF-Expert Member
Sep 24, 2010
219,470
911,174
Gazeti la Habari Leo linatufahamisha ya kuwa Mahakama zimewaonya wenye kesi za madai ya kupinga matokeo ya kura za Ubunge...........kwa kudai ya kuwa wazitafakari na kuona kama zina misingi ya kudai haki vinginevyo waziondoe kwa sababu uzoefu walionao wengi huzifungua kesi hizo kutokana na hasira ya kushindwa kwenye uchaguzi............................wajihakikishie kama wako kwenye mstari wa sheria kwa wale wote ambao wameyafungua mashauri hayo..................

Wahusika wote wanatakiwa kukamilisha uhakiki huo kabla ya Februari Mosi mwakani......


Mahakama Kuu yawaonya waliofungua kesi za ubunge

Imeandikwa na Namsembaeli Mduma; Tarehe: 27th December 2010 @ 08:27


KUTOKANA na uzoefu iliyoupata wakati wa kusikiliza kesi za kupinga matokeo ya uchaguzi wa wabunge wa 2005, Mahakama Kuu nchini imewasihi waliofungua kesi hizo mwaka huu kujiridhisha endapo zinastahili kuendelea kuwepo mahakamani, vinginevyo waziondoe kabla ya Februari mosi mwakani.

Mahakama imesema inatoa rai hiyo ili kuiepusha Serikali na matumizi makubwa ya fedha za umma yasiyostahili, pamoja na kujilinda wao wahusika na hasara inayoweza kuwakumba watakaposhindwa.

Aidha, Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG) nayo imesisitiza kutowafungulia kesi ya madai ya gharama za usumbufu, wote watakaotekeleza mwito huo kabla ya mashauri hayo kuanza kusikilizwa kwa sababu watakuwa wamesaidia kuondoa matumizi hayo ya fedha za umma yasiyo ya lazima na hivyo kusababisha fedha hizo kuelekezwa katika miradi mingine ya maendeleo ya nchi.

Hadi Desemba 10, mwaka huu, mahakama hiyo ilikuwa na mashauri 43 yatakayoigharimu serikali Sh bilioni 2.2, kutokana na kila moja kugharimu Sh milioni 53 zitakazotumika kuwasafirisha majaji husika kutoka kituo kimoja cha kazi kwenda kingine, kwa ajili ya kuyasikiliza, kwa kipindi cha miaka miwili mfululizo.

Jaji Kiongozi wa Mahakama hiyo, Fakih Jundu aliliambia gazeti hili ofisini kwake Dar es Salaam mwishoni mwa wiki iliyopita kuwa uwezekano wa kuokoa fedha hizo upo na kwamba, hilo litawezekana endapo wagombea walioshindwa na kufungua mashauri hayo au wanachama wao waliofanya hivyo kwa sababu za hasira, maumivu ya kushindwa na nyinginezo, huku wakijua kuwa hawana ushahidi wa kutosha, wataamua kuyaondoa mahakamani kwa hiyari yao wenyewe, kabla ya kuanza kusikilizwa mapema Februari mwakani.

"Ninafahamu wapo waliofungua mashauri haya kwa hasira, bila kuangalia kama yana msingi au la, na wengine hawajui madhara yake wakishindwa ilimradi wamejua ni haki yao basi wameyafungua, nawashauri wajiridhishe kuona kama yanastahili kuendelea kuwepo kwa
sababu yana gharama zake pindi watakaposhindwa na vile vile yanasababisha serikali itumie fedha nyingi pasipo ulazima," alisema Jaji Kiongozi.

Kwa maelezo ya Jaji huyo, wananchi hawana budi kufanya kampeni juu ya suala hilo na kuwashauri wahusika wayaangalie upya mashauri yao kabla ya vikao vya kuyasikiliza kuanza, vinginevyo serikali haina budi kuingia gharama hiyo ya kidemokrasia.

Akizungumzia hasara wanayoweza kuipata walioshindwa kesi hizo, Jundu alisema itategemea na gharama alizozitumia aliyelalamikiwa ambapo wengine huwa na mawakili zaidi ya wawili kwa gharama kubwa.

Alisema, kimsingi pamoja na kulipa tozo la kufungua shauri Sh 200,000, mwenye shauri hulazimika kulipa fedha taslimu Sh milioni tano mahakamani kama dhamana ambayo
hujumlishwa na fedha nyingine atakazotakiwa kumlipa aliyemshinda kama gharama za kesi.

"Mahakama haipati kitu hapo zaidi ya tozo la laki mbili na serikali inatumia shilingi milioni 53 kwa kila shauri itakalolisikiliza, sasa ni vema yakawepo yale ya msingi," alisema Jaji Kiongozi.

Kutokana na sheria iliyorekebishwa hivi karibuni kuhusu gharama za kufungua shauri la kupinga matokeo ya uchaguzi wa ubunge kutoka Sh 5,000 iliyokuwa ikitozwa awali hadi Sh 200,000, Jaji Jundu alisema ni rahisi kwa kila anayeona ana uwezo huo kufungua shauri bila kujiridhisha juu ya msingi wa shauri husika na hivyo kujikuta akilikatisha kabla halijamaliza
kusikilizwa huku serikali ikiwa imekwisha tumbukiza fedha nyingi.

Naye Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali, George Masaju alisema pamoja na kuwasamehe watakaoondoa mashauri hayo, wako tayari kuwapa ushauri wa kisheria utakaowasaidia kuona kama mashauri yao yanafaa kuendelea kuwepo mahakamani au la.

Masaju alisema mfano hai ulionekana mwaka 2005 ambapo mashauri ya aina hiyo yalikuwa
38, lakini ni manne tu ndio yaliyosikilizwa hadi mwisho na moja tu kutenguliwa baada ya walioyafungua yale 34 kuona baadaye kuwa hayakuwa na msingi wakati tayari serikali ilikwisha gharamia usikilizwaji wake.

"Tunajua wapo wanaofungua kwa hasira na wengine kwa kutokujua kama hawana ushahidi, ninachoshauri ni wahusika kujiridhisha kwanza na kuomba ushauri ndani ya muda huu wa hadi mwisho ni mwa Januari mwakani.

Hata ofisi yetu inawakaribisha kwa ushauri huo…sio busara kuangalia fedha za umma zikitumika nyingi kwenye kesi ambazo hata hivyo ni vigumu kuzithibitisha," alisema Naibu Mwanasheria Mkuu.

Naye Waziri wa Fedha, Mustafa Mkulo, alisema kutolewa kwa fedha hizo na serikali kwa haraka kiasi hicho kutategemea mapendekezo ya AG juu ya udharura na umuhimu wa mashauri hayo.

Mkulo alisema endapo AG atathibitisha dharura hiyo, Hazina italazimika kufuata taratibu zote za kiserikali za kutoa fedha hizo kutoka kwenye akaunti yake ya dharura, na hivyo kufanikisha uendeshwaji wake.

Hata hivyo, imeelezwa kuwa, Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali hutenga fedha za kusimamia kesi hizo kwenye bajeti zake za kila kipindi cha mwaka wa uchaguzi.

Mkulo alisema ikumbukwe kuwa Hazina ndio chanzo pekee cha fedha zote zinazotumiwa na mahakama nchini kwa ajili ya uendeshaji wa shughuli zake na kwamba makusanyo yote inayoyapata kutokana na mashauri yanayofunguliwa hupelekwa hazina.

 
Wanaofahamu sheria na taratibu za uendeshaji wa kesi hii kauli ya kuwataka waliofungua kesi waondoe mashauri yao siyo kuingilia uhuru wa mahakama na kuonyesha dhahiri kuwa hakuna haki itakayofanyika? Kwani wanaofungua kesi wanasheria wao hawafahamu madhara ya hizo kesi endapo wateja wao watashindwa?

Kwa maoni yangu kauli hizi ni msimamo na maelekezo ya dola jinsi hukumu za hizo kesi zitakavyokuwa hivyo kuna haja labda ya kudai kuundwa mahakama maalumu za kushighulikia kesi hizo nje ya mfumo wa kawaida wa mahakama
 
Wanaofahamu sheria na taratibu za uendeshaji wa kesi hii kauli ya kuwataka waliofungua kesi waondoe mashauri yao siyo kuingilia uhuru wa mahakama na kuonyesha dhahiri kuwa hakuna haki itakayofanyika? Kwani wanaofungua kesi wanasheria wao hawafahamu madhara ya hizo kesi endapo wateja wao watashindwa?

Kwa maoni yangu kauli hizi ni msimamo na maelekezo ya dola jinsi hukumu za hizo kesi zitakavyokuwa hivyo kuna haja labda ya kudai kuundwa mahakama maalumu za kushighulikia kesi hizo nje ya mfumo wa kawaida wa mahakama

Hiyo ndiyo hoja ya kimsingi...mahakama inatoka wapi kubeza walalamikaji hata mafaili hawajakabidhiwa na kuchukulia ya kale ni lazima yajirudie mwaka hadi mwaka?
 
Hapo kuna mkono wa mtu amini usiamini. Ni mkono uleule uliokwamisha hoja ya Mgombea Binafsi.
 
Duuh! Toka lini mahakama inaamua kuchukua upande badala ya kusikiliza na kisha kutoa maamuzi ili kila mtu aridhike? Haya mambo ya aina hii ndiyo yanayoua na kudhalilisha professionals Tanzania. Hii nchi haitakaa sawasawa kama tunataka kuindesha kwa mipangilio ya kutishana na kuonyeshana umwamba. Tuiendeshe kama watu ambao tunajua tunalofanya. Kwa statement ya aina hii mahakama imeshaamua kujiingiza kwenye debate isiyo na tija. I wish I could learn to keep my mouth shut if I dont have something to say!!
 
hii ndio Tz.
Umetukanwa na mtu unaenda kwa mjumbe kushtaki, mjumbe anakuambia tafakari kama kuna ulazima wa kushitaki.
Kama hakuna ulazima inamaana umekubali kutukanwa na vilevile mjumbe ana kubali kwa namna moja au nyingine kutukanwa ni halali!!!
I wish wange wapa mbinu za kushinda kesi na sio vitisho.
Hivi wabunge wa CCM ambao wamefungua mashtaka hayo ni wangapi?
 
Back
Top Bottom