GE2025 Kesi ya Zuio CHADEMA kufanya shughuli za kisiasa yaahirishwa Hadi Agosti , 18, 2025

GE2025 Kesi ya Zuio CHADEMA kufanya shughuli za kisiasa yaahirishwa Hadi Agosti , 18, 2025

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

DuaZaMama

JF-Expert Member
Joined
Jun 2, 2025
Posts
1,882
Reaction score
4,129
Kesi ya madai iliyofunguliwa dhidi ya Bodi ya Wadhamini ya CHADEMA na Katibu Mkuu wa chama hicho, inayohusu zuio la kufanya shughuli za kisiasa, imeahirishwa hadi Agosti 18, 2025, kwa ajili ya kusikilizwa kwa uamuzi wa maombi ya kutengua zuio hilo.

Shauri hilo, Na. 8323/2025, liliwasilishwa na aliyewahi kuwa Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA upande wa Zanzibar, Said Issa Mohammed, na linahusu zuio lililotolewa na Mahakama tarehe 10 Juni 2025, ambalo liliwazuia viongozi wa CHADEMA kufanya shughuli za utendaji pamoja na kutumia rasilimali za chama. Katika hatua ya hivi karibuni, upande wa walalamikiwa kupitia kwa mawakili wao wamewasilisha maombi ya kutaka zuio hilo litenguliwe, wakidai kuwa lilienda kinyume cha haki ya kikatiba ya kushiriki siasa.

Pia wameeleza kuwa wakati zuio hilo linatolewa, hawakuwa na mwakilishi mahakamani baada ya Wakili Jebra Kambole kujitoa, hivyo walinyimwa haki ya kusikilizwa. Hata hivyo, upande wa wajibu maombi umepinga hoja hizo kwa msingi kuwa walalamikiwa hawakukosa haki ya kusikilizwa, bali walishindwa kufuatilia mwenendo wa shauri hilo kwa uzembe wao wenyewe. Mahakama imesema itatoa uamuzi kuhusu hoja hizo tarehe 18 Agosti, hatua ambayo itaamua kama zuio hilo litaendelea kuwepo au la.
28a5eac0-ff16-407e-be20-81b93e80cc24_976x645.jpg
 
Hii kesi hata ikiisha mwakani mwishoni ni sawa
 
Hapo hakimu anafuata maelekezo tu kama Ndugai.
Pambana na Hali yenu wenyewe , Mh Ndugai (RIP), YEYE ameisha hitimisha ya kwake hapa Duniani, kumuandama hakutuwasaidia kitu at this moment when your house is in disarray .
 
Siku mto maelekezo kutoka juu akifa au kuondoka madarakani ghafla hawa majaji huwa wanajifanya wana integrity na wana uchungu mkubwa na uhuru wa mahakama.
 
Tuna utawala wa shetani ambao umeua mihimili yote. Sasa mahakama imekuwa kama klabu ncha pombe za kienyeji ambamo mwenye uwezo wa kununua debw la kimpuni, sute, komoni au ulanzi, anaweza akawaimbisha wote wanaokunywa bure.
 
🤣🤣🤣🤣 kwahiyo manyumbu ya chadema bado yanasubiri mahakama itende haki wajinga hawajawahi kuisha🤣🤣🤣🤣
 
Huku hakimu atakufa kama ndugai siku akifa nitaacha kunywa bia kummer mae hakimu ulie goma kujitoa kwenye kesi
 
Back
Top Bottom