Kesi ya vigogo BoT kughushi vyeti yakwama | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kesi ya vigogo BoT kughushi vyeti yakwama

Discussion in 'Jukwaa la Sheria (The Law Forum)' started by Rutashubanyuma, Aug 14, 2011.

 1. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #1
  Aug 14, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,345
  Likes Received: 418,840
  Trophy Points: 280
  [TABLE="class: contentpaneopen"]
  [TR]
  [TD="class: contentheading, width: 100%"]Kesi ya vigogo BoT kughushi vyeti yakwama
  [/TD]
  [TD="class: buttonheading, width: 100%, align: right"] Send to a friend [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
  [TABLE="class: contentpaneopen"]
  [TR]
  [TD="class: createdate"] Friday, 12 August 2011 21:32 [/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD]

  Nora Damian
  MAWAKILI wa upande wa utetezi katika kesi ya kughushi vyeti inayowakabili wafanyakazi wanane wa kitengo cha kuhesabu fedha chakavu katika Benki Kuu ya Tanzania (BoT) jana walikwamisha usikilizwaji wa kesi hiyo kwa kushindwa kufika mahakamani.

  Kesi hiyo ilikuwa imepangwa kuendelea kusikilizwa kwa mashahidi wa upande wa mashtaka, lakini ilikwama kutokana na mawakili wa upande wa utetezi kutofika mahakamani.

  Hakimu Mkazi Rita Tarimo aliahirisha kesi hiyo hadi Septemba 12 itakapoendelea kusikilizwa.
  Washtakiwa wanaokabiliwa na kesi hiyo ni Justine Mungai, Christine Ntemi, Siamini Kombakono, Janeth Magehenge, Beather Masawe, Jacquline Juma, Philimina Mutagurwa na Amina Mwinchumu.

  Wote wanatetewa na mawakili wa kujitegemea Majura Magafu, Jerome Msemwa na Mpale Mpoki.
  Washtakiwa hao wanadaiwa kughushi vyeti vya kidato cha nne vinavyoonyesha vilitolewa na Baraza la Taifa la Mitihani (Necta).

  Washtakiwa wote kwa pamoja walifikishwa kwa mara ya kwanza mahakamani hapo Septemba 19, 2008 wakikabiliwa na shtaka la kughushi vyeti vya kidato cha nne na kumdanganya mwajiri wao kwa kuwasilisha vyeti hivyo na kupatiwa ajira.[/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
   
 2. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #2
  Aug 14, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,345
  Likes Received: 418,840
  Trophy Points: 280
  yaani hata form four nayo mtu hana........................it is so sad............
   
Loading...