Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 4,393
- 14,500
Wakuu!
Mwenyekiti CHADEMA Taifa Tundu Lissu kufikishwa katika Mahakamani ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam leo kwa ajili kesi ya Uhaini inayomhusu.
Kumbuka kwamba kwenye kesi hii Tundu Lissu anajitetea mwenyewe.
Je, leo mwamba anaachiwa au atarudishwa tena 'kukamilisha na kumalizia kabisa kabisa kabisaaaa upelelezi?'
Wacha tuone kitakachojiri!
Kesi ya uhaini inayomkabili Lissu kutajwa tena leo Julai 15, uamuzi wa DPP kungojewa
Kesi ya uhaini inayomkabili Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Tundu Antiphas Lissu inaendelea leo Julai 15, 2025 ikiwa ni siku 14 tokea iliposikilizwa mara ya mwisho, ambapo unangojewa uamuzi ya Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) kutokana na jalada ambalo ilielezwa kuwa lipo mezani kwake.
Ikumbukwe kuahirishwa kwa kesi hiyo inayotajwa kwenye Mahakama ya Hakimu Mkazi KIsutu, kulifikiwa baada ya Mahakama hiyo kukubali maombi ya upande wa Jamhuri ulioeleza kuwa mpaka tarehe hiyo Julai 1, 2025, bado DPP alikuwa ajafanya uamuzi wa jalada la kesi ambalo lipo mezani kwake.
Awali, kabla ya kutolewa uamuzi huo na mahakama, Tundu Lissu wakati akijitetea aliiomba Mahakama kuagiza upande wa Jamhuri kulipeleka shauri lake Mahakama Kuu ya Tanzania haraka kama wamekamilisha ushahidi au Mwendesha Mashtaka aonyeshe nia ya kutoendelea na shauri lake, hivyo amuachie huru (nolle prosequi). Ikumbukwe Mahakama Hakimu Mkazi Kisutu inafungwa mikono kisheria kusikiliza kesi hiyo.
===
Ulinzi umeimarishwa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Dar es Salaam
Kaimu Katibu Mkuu wa CHADEMA, John Mnyika Mwenyekiti wa chama hicho Kanda ya Nyasa, Joseph Mbilinyi (SUGU),Mwenyekiti wa Bawacha Taifa, Sharifa Suleiman tayari wamefika hapa Kisutu kufuatilia kesi ya uhaini inayomhusu Mwenyekiti wa chama chao Tundu Lissu.
Tayari Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA Bara, John Heche awasili katika ukumbi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kufuatilia mwenendo wa kesi ya Uhaini inayomkabili Mwenyekiti wa Chama Taifa, Tundu Lissu.
Mabalozi na wawakilishi wa balozi mbalimbali nchini wakiwa katika ukumbi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kufuatilia mwenendo wa kesi ya Uhaini inayomkabili Mwenyekiti wa Chama, Tundu Lissu.
Wakili wa Serikali Mkuu, wakati wa Usikilizaji wa kesi ya uhaini Na. 8607/2025 dhidi ya Tundu Lissu.
"Tarehe iliyopita tuliiambia Mahakama yako kwamba shauri hili lipo hatua ya kusomwa na kutolewa maamuzi. Upelelezi wake umekamilika kwa utimilifu wake na baada ya Ofisi ya Taifa ya Mashtaka yaani Ofisi ya DPP kusoma jalada hili, umejiridhidha ushahidi uliopo unajitosheleza kwenda kupeleka kesi Mahakama Kuu".
Tundu Lissu apinga Kesi kuahirishwa tena
''Leo ni siku ya 97 niko Mahabusu na wafungwa waliohukumiwa Kifo nimechoka na hizi habari''
"Mkurugenzi wa Mashtaka tayari alishasoma jalada, kwa mujibu wa sheria lilipaswa kuwa mahakamani na ielezwe kuwa taarifa imeshapelekwa Mahakama Kuu – si vinginevyo,"
"Hii hali si ya kufurahisha. Nimekaa mahabusu kwa muda mrefu, niko karibu na wafungwa wa kunyongwa hadi kufa, halafu bado DPP hana uamuzi kama aendelee na kesi au la?"
"Mahakama zisiruhusu kufanya kazi zake kwa kuendeshwa na waendesha mashtaka, hatujatekeleza kukamilisha ushahidi ahirisha, unaahirisha! Eeeh! unaahirisha. Mheshimiwa unaahirisha tangu tarehe 10"
"Watu wa taifa hili wanajua, na ulimwengu unajua, hakuna kesi hapa bali ni Siasa. Ni mwaka wa uchaguzi, na mwaka wa uchaguzi kiongozi mkuu wa chama cha upinzani amekamatwa, amepewa kesi ya uhaini — si kwa sababu ni mhaini, bali kwa sababu ya Siasa, ili watu waende kwenye uchaguzi wasisumbuliwe na 'No Reforms, No Election'."
"Nchi yetu imechafuka kwasbababu ya Kesi hii"
"Mheshimiwa umeambiwa kwamba naomba huruma ya Mahakama. Mimi siombi huruma ya Mahakama. Siombi, sijaomba na sitaomba. Ninachotaka, utaratibu wa Mahakama usichezewe. Mawakili wa Serikali na DPP wanachezea utaratibu wa Mahakama. Mimi siyo aina ya watu ambao wataomba huruma ya Mahakama, kwa sababu nasimamia ninachoamini kuwa ni kweli. Wanaomba huruma ya Mahakama ni wenye hatia."
"Kama nilivyosema, hii kesi Mheshimiwa iliyofunguliwa Mahakama ya Afrika Mashariki kuhusu mambo yanayohusiana na kesi hii (kesi ya Lissu ya uhaini). Jaji Mkuu Mstaafu wa Kenya, Mutunga na hao wenzake walizuiliwa uwanja wa ndege, wakawekwa kizuizini, halafu wafukuzwa wakati mkataba wa Afrika Mashariki unasema ni raia wa Afrika Mashariki, wana haki ya kuingia na kutoka, na kuja mahakamani na kuangalia kinachoendelea, kwahiyo tumepelekwa mahakamani"
Kesi ya Uhaini ya Lissu yaahirishwa tena Mahakama ya Kisutu, hadi Julai 30, 2025
Kesi ya uhaini ya Tundu Lissu imeahirishwa hadi Julai 30, 2025, baada ya Jamhuri kuomba muda kusubiri uamuzi wa Mahakama Kuu kuhusu ombi la kuwakinga mashahidi.
Ahirisho hilo limetolewa na Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Franko Kiswaga baada ya kusikiliza hoja za upande wa Jamhuri na upande wa utetezi.
Katika hoja zake, Lissu aliitaka Mahakama isiahirishe kesi hiyo kwa kuwa upande wa Jamhuri umekuwa ukiahirisha kwa muda mrefu lakini upande wa Jamhuri nao, ulitoa hoja kuwa umeomba ahirisho kwa kuwa tayari wameshawasilisha maombi Mahakama Kuu ya kuficha mashahidi katika kesi hiyo kabla ya kupeleka kesi hiyo Mahakama Kuu.
Hakimu alikubaliana na upande wa Jamhuri na kisha kuutaka Upande wa Jamhuri ushughulikie maombi hayo haraka iwezekanavyo ili haki iweze kuendelea kufuata mkondo wake.