Kesi ya Semenya yaanza kusikilizwa

miss zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
2,900
2,000
Mwanariadha wa Afrika Kusini Caster Semenya anapinga sheria zinazopendekezwa na Shirikisho la Riadha Duniani – IAAF kuhusu viwango vya homoni za testosterone kwa wanariadha.

Kesi hiyo katika Mahakama ya usulishi wa migogoro michezoni inamhusu mwanariadha wa Afrika Kusini Caster Semenya ambaye anapinga sheria zinazopendekezwa na Shirikisho la Riadha Duniani – IAAF kuhusu viwango vya homoni za testosterone kwa wanariadha.

Akizungumza mapema leo kabla ya kuanza kikao hicho cha mahakama, Rais wa IAAF Sebastian Core aliwaambia wanahabari kuwa "Thamani ya msingi kwa IAAF ni kuwawezesha wasichana na wanawake kupitia riadha. Sheria tunazotunga ni kwa ajili ya kulinda uadilifu wa mashindano kwa njia ya haki na wazi na hicho hasa ndicho tunataka kukitetea. Kesi hiyo iliyowasilishwa na Semenya mwenye umri wa miaka 28, ni miongoni mwa kesi zilizowai kuchukua muda mrefu zaidi katika mahakama hiyo ya michezo mjini Lausanne, Uswisi.

IAAF inataka wanawake wenye vowango vikubwa vya homoni za testerone kupunguza viwango vyao kwa kupitia matibabu kabla ya kuruhusiwa kushiriki katika mbio za kuanzia mita 400 hadi maili moja.

Serikali ya Afrika Kusini inasema sheria hizo zinamlenga Semenya tu na kuziita kuwa ukiukaji mkubwa wa haki zake za binaadamu. THOKOZILE XASA, ni waziri wa michezo nchini Afrika Kusini.

"Kinachogombaniwa hapa ni zaidi ya haki ya kushiriki michezoni. Miili ya wanawake, maisha yao, uwezo wao kujipa kipato, utambulisho wao, usiri wao, hali yao ya kujihisi salama na kuwa sehemu ya ulimwengu vyote hivyo vinatilishwa mashaka.

Semenya sio mwanariadha pekee anayeweza kuathirika na sheria hizi – kuna washindi wa fedha na shaba wa mbio za mita 800 katika Olimpiki, Francine Niyonsaba wa Burundi na Mkenya Margaret Wambui, pia wanakabiliwa na maswali kuhusu viwango vyao vya testerone. Matthieu Reeb, Katibu Mkuu wa Mahakama ya CAS anasema kesi hiyo sio ya kawaida kwa sababu hawajawahi kuiona

"Kwa wiki nzima, tutawasikia mashahidi, watalaamu, na kisha Ijumaa hoja za mawakili wa pande zote. Tunatumai jopo la mahakama litakamilisha kesi hiyo ifikapo Ijumaa usiku, na kisha kutakuwa na wiki nne hivi za mashauriano kati ya wanachama wa jopo hilo, na uamuzi wa mwisho utatolewa kupitia maandishi na litatangazwa kwa umma.

Testosterone ni homoni ambayo inaongeza misuli, nguvu na damu, na hivyo kuchangia katika uwezo wa mwanariadha kuvumia uchovu. Kwa mujibu wa IAAF, wanariadha wenye kiwango kikubwa cha testerone kimsingi huwa wanapendelewa na hivyo watahitajika kupunguza kiwango chao ili kudumisha suala la haki katika mashindano.


Dw
 

Madame B

Verified Member
Apr 9, 2012
27,983
2,000

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom