Kesi ya ndoa ya Dk Slaa yasogezwa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kesi ya ndoa ya Dk Slaa yasogezwa

Discussion in 'Jukwaa la Sheria (The Law Forum)' started by jakamoyo, Aug 15, 2012.

 1. j

  jakamoyo JF-Expert Member

  #1
  Aug 15, 2012
  Joined: May 12, 2011
  Messages: 260
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 35
  Wednesday, 15 August 2012 08:49

  Na James Magai,

  NDOA ya Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Dk Willibrod Slaa na mchumba wake, Josephine Mushumbusi imezidi kuwekwa rehani baada ya Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam kusogeza mbele usikilizwaji wa mapingamizi yaliyowekwa dhidi ya ndoa hiyo.

  Dk Slaa na Josephine walitarajia kufunga ndoa kwenye Kanisa Katoliki Julai 21 mwaka huu, lakini Rose Kamili anayedai kuwa ni mke wa Dk Slaa, alifungua kesi kupinga ndoa hiyo na kudai fidia ya Sh550 milioni. Kesi hiyo namba 4 ya mwaka 2012 alisema ilitarajiwa kuanza kusikilizwa jana lakini Dk Slaa ameweka pingamizi dhidi ya Rose akidai kuwa hana haki ya kufungua kesi kupinga yeye kufunga ndoa na Josephine kwa kuwa hawakuwa na ndoa halali kisheria.

  Kwa mujibu wa pingamizi hilo la Dk Slaa, ndoa kati yake na Rose ni ndoa ya dhana tu ambayo haiwezi kumfanya awe na nguvu ya kupinga kufunga ndoa baina yake na Josephine kwa tatatibu za kisheria. Akitoa ufafanuzi wa pingamizi hilo, Wakili wa Dk Slaa, Phillemon Mutakyamirwa alisema kuwa kutokana na sababu hiyo Rose hakupaswa kufungua kesi mahakamani kupinga Dk Slaa kufunga ndoa na Josephine kisheria na kwamba kesi hiyo iko mahakamani isivyo sahihi.

  "Hakupaswa kufungua kesi kupinga kufungwa kwa ndoa inayotarajiwa kufungwa kisheria, bali alipaswa kuleta maombi na ati ya kiapo, kuomba mahakama iangalie labda kama kuna mali walizochuma pamoja au matunzo ya watoto," alisema Mutakyamirwa.

  Hata hivyo wakati Dk Slaa kupitia kwa wakili wake akiweka pingamizi dhidi ya Rose kumfungulia kesi, Rose naye kupitia kwa wakili wake Joseph Tadayo ameweka pingamizi dhidi ya pingamizi la Dk Slaa. Katika pingamizi lake, pamoja na mambo mengine, Rose kupitia kwa wakili wake pia anadai kuwa pingamizi hilo la Dk Slaa lina kasoro na kwamba limewasilishwa mahakakamani isivyo halali. Kwa mujibu wa pingamizi hilo la Rose lililowasilishwa mahakamani hapo jana na Wakili wake Tadayo, pingamizi la Dk Slaa limewasilishwa mahakamani isivyo halali kwa kuwa halijathibitishwa kutokana na kutokuwepo kwa saini ya Josephine.

  Kutokana na mapingamizi hayo, Mahakama imeamua kuanza kusikiliza pinamizi la Dk Slaa dhidi ya Rose na imeamuru usikilizwajiwa huo ufanyike kwa njia ya maandishi, baada ya mawakili wa pande zote kukubaliana hivyo. Hivyo Jaji Lawrance Kaduli aliamuru Dk Slaa kuwasilisha mahakamani maelezo yake ya maandishi katika kipindi cha juma moja kuanzia jana, yaani kabla ya, au Agosti 21 na kumtaka Rose kuwasilisha majibu Septemba 4, 2012.

  Pia Jaji Kaduli alipanga kesi hiyo itajwe Septemba 18, 2012 kwa ajili ya kupanga tarehe ya kutoa uamuzi wa pingamizi hilo la Dk Slaa.
  Ikiwa mahakama itatupilia mbali pingamizi la Dk Slaa basi itaanza kusikiliza rasmi madai ya Rose na uamuzi huo ndio utakaoamua ama Dk Slaa kufunga au kutokufunga ndoa na Josephine. Kutokana na mazingira hayo ndoa hiyo imeendelea kubaki njia panda na hatima yake haijajulikana kuwa itakuwa ni lini na kutegemeana na maamuzi ya Mahakama.

  Madai ya Kamili

  Katika kesi hiyo, Kamili ambaye ni Mbunge wa Viti Maalum (Chadema), anaiomba Mahakama kusimamisha ndoa yao hiyo inayotarajiwa kufungwa Julai 21, mwaka huu. Kamili, pia anaiomba mahakama iamuru Dk Slaa amlipe Sh50 milioni kama fidia aliyotumia kujihudumia pasipo matunzo ya mumewe huyo. Mbunge huyo kupitia wakili wake Tadayo, aniomba pia mahakama iamuru Mushumbusi amlipe kiasi cha Sh500 milioni kama fidia ya maumivu aliyoyapata kutokana na kitendo chake cha kuingilia ndoa yao.

  Katika hati hiyo ya madai, mbunge huyo anadai kuwa ndoa inayotarajiwa kufungwa kati ya Slaa na Mushumbusi ni batili kwa sababu kuna ndoa nyingine halali na inayoendelea kuishi kati yake na mumewe huyo iliyofungwa mwaka 1985. Alidai baada ya kufungwa kwa ndoa hiyo, Juni 18, 1987 walifanikiwa kupata mtoto wa kike anayeitwa Emiliana Muchu na baadaye Septemba 23, 1988 walipata mtoto mwingine wa kiume, Linus Amsi.

  Katika uhusiano wao, Slaa akiwa ni Padri wa Kanisa Katoliki, alifanya taratibu zilizomwondosha katika nafasi hiyo ya upadre na kuanza maisha ya familia. Baada ya taratibu hizo, jamii ya Watanzania iliwatambua kama mume na mke ambapo hata kumbukumbu za hati za kimataifa kama za kusafiria ziliwatambua kuwa wanandoa. Kamili aliendelea kudai katika maelezo hayo kuwa yeye na Slaa waliishi maisha ya ndoa yenye amani, yaliyowawezesha kupata mali kadhaa walizomiliki kwa pamoja ikiwemo nyumba iliyopo kwenye kiwanja namba 609 kitalu E, nyumba ya makazi iliyopo kijiji cha Gongali huko Karatu na vifaa mbalimbali vya nyumbani.

  Hati ya mashtaka imeendelea kueleza kuwa, uhusiano kati ya Slaa na mkewe Kamili, ulianza kuharibika mwaka 2009, baada ya Slaa kuwa na uhusiano na mwanamke mwingine kinyume cha sheria.

  "Tangu mwaka huo 2009, Slaa akaitelekeza familia yake kwa kutoipatia huduma," imeeleza hati hiyo.

  Kamili anaiomba mahakama iamuru kuwa yeye na Slaa bado ni mke na mume na kwamba, Mushumbusi aliingilia ndoa yao hivyo mahakama izuie ndoa inayotajiwa kufungwa Julai 21, mwaka huu. Kamili pia amewasilisha hati hiyo ya mashtaka kwa Kiongozi Mkuu wa Kanisa Katoliki nchini, Mwadhama Polycarp Kadinali Pengo.

  Kamili amemweleza Kadinali Pengo ambaye pia anaongoza Jimbo Kuu la Katoliki la Dar es Salaam, kuwa moja ya Parokia za Dar es Salaam zina taarifa ya ndoa hiyo. Nakala ya madai hayo pia imewasilishwa kwa Msajili wa Mahakama Kuu, Msajili wa Ndoa na kwa Askofu Mkuu wa Jimbo la Mbulu.

  Chanzo: Mwananchi
   
 2. Ritz

  Ritz JF-Expert Member

  #2
  Aug 15, 2012
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 42,252
  Likes Received: 4,672
  Trophy Points: 280
  Wanabodi.

  Ndoa ya Kitibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendelo Chadema, Dr Slaa na mchumba wake, Josephine Mushumbusi imezidi kuwekwa rehani baada ya Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam kusogeza mbele usikilizwaji wa mapingamizi yaliyowekwa dhidi ya ndoa hiyo.

  DK Slaa na Josephine walitarajia kufunga ndoa kwenye Kanisa Katoliki Julai 21 mwaka huu, lakini Rose Kamili anayedai kuwa ni mke wa Dk Slaa, alifungua kesi kupinga ndoa hiyo na kudai fidia ya Sh550 milioni.

  Kesi hiyo namba 4 ya mwaka 2012 ilitarajiwa kuanza kusikilizwa jana lakini Dk Slaa ameweka pingamizi dhidi ya Rose, akidai kuwa hana haki ya kufungua kesi kupinga yeye kufunga ndoa na Josephine kwa kuwa hawakuwa na ndoa halali kisheria.

  Dk Slaa anasema kati yake na Rose ni ndoa ya dhana tu ambayo haiwezi kumfanya awe na nguvu ya kupinga, Rose naye kupitia kwa wakili wake Joseph Tadayo ameweka pingamizi dhidi ya pingamizi la Dk Slaa, anadai pingamizi la Dr Slaa, lina kasoro na kwamba limewasilishwa mahakamani isivyo halali.

  SOURCE: MWANANCHI AGOSTI 15 2012...ukurasa wa 2.
   
 3. k

  kabombe JF-Expert Member

  #3
  Aug 15, 2012
  Joined: Feb 11, 2011
  Messages: 15,580
  Likes Received: 8,520
  Trophy Points: 280
  Napata wasiwasi kidogo na uadilifu wa Dr.Slaa.Ina maana hatambui pia wale watoto aliozaa na Mh.Kamili?
  Vipi mtoto aliezaa na Josephine kabla ya ndoa?Kuna tatizo katika suala la ucha mungu hapa
   
 4. peri

  peri JF-Expert Member

  #4
  Aug 15, 2012
  Joined: Mar 22, 2011
  Messages: 2,588
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 145
  yangu macho, tusubiri hukumu ya mahakama.
   
 5. N

  Nikupateje JF-Expert Member

  #5
  Aug 15, 2012
  Joined: Dec 22, 2009
  Messages: 1,314
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 160
  Moderator wa JF,

  Kama mlizuia thread yangu ya jana nikiwakumbusha wana-JF kuhusu Kesi hii na ikibidi tupate LIVE UPDATE kama kwenye kesi zingine, basi kwa nini leo unaruhusu Kesi hii ijadiliwe hapa JF kama si upendeleo?

  Wadau,

  Oneni ninachokisema kwa kufungua hii link kama mtaweza (Click Here). Ilikuwa locked jana.
   
 6. Shine

  Shine JF-Expert Member

  #6
  Aug 15, 2012
  Joined: Feb 5, 2011
  Messages: 11,514
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  Mahakama gani? Hii hii ccm ama gani?
   
 7. Shinto

  Shinto JF-Expert Member

  #7
  Aug 15, 2012
  Joined: Dec 6, 2010
  Messages: 1,781
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Hii ni habari mbaya kwa wale viwavi waliokuwa wanadhani ndoa ilishafungwa!
   
Loading...