Kesi ya namba 458 ya JamiiForums vs Jamhuri yakwama kuendelea, shahidi ashindwa kutokea

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,812
11,986
Kesi namba 458 ya mwaka 2016 (Jamhuri v Maxence Melo na mwenzake Micke William) inayohusu kuendesha mtandao bila kutumia Kikoa cha do.TZ na Kuzuia Upelelezi wa Polisi imetajwa leo Oktoba 18, 2019 katika Mahakama ya Hakimu Mkazi, Kisutu.

Kesi hiyo imeshindwa kuendelea baada ya shahidi wa upande wa Jamhuri kutofika Mahakamani na hakuna sababu zozote zilizotolewa juu ya kutokufika kwake.

Upande wa Utetezi leo umewakilishwa na Mawakili, Peter Kibatala, Jebra Kambole, Jeremiah Mtobesya na Emmanuel Christopher. Upande wa Jamhuri umewakilishwa na Wakili Adolf Mkini akiwa amemuwakilisha Wakili anayehusika na shauri hili, Daisy Makakala.

Wakili wa Jamhuri amesema shauri hilo lilikuwa kwa ajili ya kusikilizwa lakini anaomba ahirisho kwa kuwa Jamhuri haina Shahidi lakini pia Wakili anayehusika na kesi hayupo. Sababu ya Wakili kutokuwepo haikuwekwa wazi.

Kutokana na maelezo ya Jamhuri, Mwakili wa upande wa Utetezi wamekubali kuahirishwa kwa kesi hili wakisema “Tunaona hadi Maaskari wameandaliwa kabisa kuwakamata wateja wetu. Mheshimiwa Hakimu tunaomba ahirisho fupi.” Walionekana askari 3 wakiwa wamejiandaa kwa ukakamavu.

Baada ya maelezo hayo, Hakimu Huruma Shaidi ameeleza kuwa mara ya mwisho alisema lilikuwa ni ahirisho la mwisho ila anajua akiifuta kesi hii washtakiwa watakamatwa na kesi kuanza upya, sasa anaona bora tu iahirishwe tena.

Hakimu baada ya kusema hayo ameahirisha shauri hilo hadi Novemba 07, 2019.

Itakumbukwa mara ya mwisho kutajwa kwa shauri hili, Wakili Daisy Makakala aliomba ahirisho la mwisho huku shahidi anayesubiriwa akiwa ametimiza takriban miezi saba hajafika na kesi imekuwa ikiahirishwa kila inapotajwa kutokana na sababu hiyo.

Aidha, JamiiForums inakabiliwa na kesi nyingine ya Kuzuia Upelelezi katika Mahakama hiyo ya Kisutu chini ya Hakimu Thomas Simba, itakayoendelea kusikilizwa Oktoba 22, 2019.
*****

UPDATES:
Kesi hii imeendela leo Novemba 07, 2019 mbele ya Hakimu Huruma Shaidi huku Upande wa Jamhuri umewakilishwa na Wakili Daisy Makakala huku upande wa utetezi ukiwakilishwa na Benedict Alex

Wakili wa Jamhuri amesema Shahidi ameshindwa kufika hivyo wameomba kupewa muda zaidi huku wakiendelea na mchakato wa kufunga Ushahidi. Amesema kama shahidi hatapatikaka, watafunga ushahidi.

Hakimu kaahirisha kesi. Itatajwa tena tarehe 26 Nov 2019.
******


Kujua zaidi kuhusu shauri hili lilivyokuwa mara ya mwisho Mahakamani, soma >>


Aidha, kujua kinachoendelea kwenye kesi zote zinazomuhusisha Mkurugenzi Mtendaji wa Jamii Media na Mwanahisa mwenzake, soma >>>

 
Mungu akiwa upande wetu hakuna aliye juu yetu. Aya yote yana mwisho. Nchi hii ni yetu lazima tuwe huru.

NB:GIZA HALIWEZI KUSHINDA NURU.
 
Naamini hizi kesi zote mwisho wake ni ushindi kwetu na fedhea kwa utawala huu..

Jf itadumu milele
 
Back
Top Bottom