Kesi ya Mnyika hukumu ni Leo

Status
Not open for further replies.
Mahakama ikifuata haki Mnyika ni mbunge wa ubungo. Jaji akitoa hukumu kwa maelekezo ya nje ya mahakama Mnyika siyo mbunge wa ubungo

Mungi.
Wewe kile kinachoifurahisha Chadema kwako ndio haki? Unatafsiri sheria za nchi kwa kutumia kichwa chako.

Tujaribu kuheshimu uhuru wa mahakama na tukubaliane na hukumu yoyote mahakama itakayotoa dhidi ya Mnyika.
 
Duu mim napenda kweli MNYIKA ashindwe ili wanvue huo ubunge ili uchaguzi uludiwe.
Halafu wapate jibu kuwa nani alitakiwa kuwa mbunge wa UBUNGO.
jimbo lenyewe limejaa vijana sio wazee mabwege wa kuhongwa t-shirt,kofia,kanga,vitenge,masharti,mitandio,vilemba,wali na pombe chafu(kienyeji).
 
Mungi.
Wewe kile kinachoifurahisha Chadema kwako ndio haki? Unatafsiri sheria za nchi kwa kutumia kichwa chako.

Tujaribu kuheshimu uhuru wa mahakama na tukubaliane na hukumu yoyote mahakama itakayotoa dhidi ya Mnyika.
ritz
nimekuwa nikifuatilia posts zako na comments zako una busara sana bro.
 
Ni maneno ya mfa maji, kama vurugu wanaitaka wataianzisha wao CDM ni amani tu
 
Mnyika akishindwa itakuwa ni dhulma tu -- na matokeo yake ni kuipandisha chati Chadema maradufu. Nimeshuhudia ya kule Arusha - baada ya kuondolewa Lema, CCM ime-cease ku-exist pale Arusha -- hakuna CCM sasa hivi, ni aibu tu waliojiletea CCM.

Nadhani mliopo Arusha mmeliona hili.
 
Wanabodi ile hukumu iliyokuwa inasubiriwa kwa hisia tofauti itaanza masaa machache hajayo tuone Kama chaguo la wapiga kura wa ubungo litapigwa chini au mahakama itawaunga mkono. Twende kazi
Tumuombee mpambanaji wetu na mahakama isimamie haki kutendeka!!!!! VIVA CHADEMA VIVA UKOMBOZI WA WANYONGE TANZANIA !!!!

 
mungu yupo upande we2 na kama wakichakachua watajua nguvu ya umma, segerea 2mekaa kimya pia arusha bt wakifanya ujinga huu na ubungo hapo 2tashndwa kuvumilia.
 
Mungi.
Wewe kile kinachoifurahisha Chadema kwako ndio haki? Unatafsiri sheria za nchi kwa kutumia kichwa chako.

Tujaribu kuheshimu uhuru wa mahakama na tukubaliane na hukumu yoyote mahakama itakayotoa dhidi ya Mnyika.

Ritz, ni vyema kuheshimu mahakama kama unavyosema. Lakini ukubali pia kuwa sheria zinapindishwa. Kweli 1+1=1 in normal mathematical principles!!! if not matrimonial mathematics where 1+1=1. Sasa kuna hukumu za hivyo
 
Kwenye Wall yake Facebook Mnyika kayaandika haya

Nimepokea taarifa kwamba hukumu ya kesi ya uchaguzi dhidi ya ushindi wetu Jimbo la Ubungo kesho tarehe 24 Mei 2012 itatolewa katika Jengo la MAHAKAMA KUU (KIVUKONI-COURT No. 1) badala ya jengo ilipo mahakama ya kazi (akiba) ambapo kesi iliendeshwa. Kama tulivyotafuta kura pamoja, tukapanga mstari kupiga kura pamoja na tukakesha kuzilinda pamoja tujumuike pamoja kujua hatma ya kura zetu. Hukumu ya kesi inatarajiwa kuanza kusomwa SAA NNE ASUBUHI hata hivyo ni muhimu kuwahi mapema zaidi asubuhi kwa ajili ya itifaki za kuingia mahakamani.

Maslahi ya Umma kwanza!

MUHIMU: Mpe taarifa mwenzako!
Rejao umeamua kuamplify face book ya Nyika una nia gani au gamba limekuwa moto unakaribia kulivua?????Karibu CDM kwa wapambanaji!!!!

 
Yote tunamwachia aliye juu, maana katika hali ya kawaida sheria nayo imebakwa, ni Mungu tu ambaye anaweza kuepusha balaa hilo. Katika hali ya kawaida bila ya ushabiki Mnyika ana mchango ambao bado ni muhimu katika mustakabali katika siasa za Tanzania na hasa Bunge letu, sote tumekuwa tukishuhudia michango yake katika bunge letu hasa kwa kuzingatia umakini wake katika kusoma nyaraka mbalimbali na kuibua mapungufu, ambayo yamekuwa muhimu kwa nchi.

Mungu watangulie Majaji ili waweze kutenda haki. Amina
 
Status
Not open for further replies.
4 Reactions
Reply
Back
Top Bottom