Kesi ya Mbowe ilipikwa kipindi cha Hayati Rais Magufuli

Ukweli ni kwamba aliyeisimamia mpaka ikaiva, akaipakua na kulisha wananchi ndio wakuangushiwa gari bovu
 
Unafahamu kwamba kipindi Cha JPM Mh Mbowe kapoteza vingi Sana. Kabomolewa bilcanas, kuharibiwa shamba lake, kufungiwa gazeti lake la Tanzania daima, kufukuzwa kwenye Jengo la NHC ambalo kiasili ni Mali yao, kutajwa kwenye madawa ya kulevya na makonda, kuvamia na wasiojulikana na kusingiziwa alikuwa amelewa , kufungiwa akaunti yake na pesa zake kuchukuliwa

Leo mtu akikwambia hii ilikuwa ni kesi iliyopikwa na mwendazake unaona kwamba asingeweza kufunga mtu.

Kile kilichompata Lissu na hili la Mbowe lipi kubwa we jamaa?
kafukuzwa kwenye jengo la NHC ambalo kimsingi ni mali yao? mzee mbona unajikanyaga sana
 
Kwa hiyo wewe unajifanya kwamba hujui kusoma?

Tunasema kesi ilitengenezwa na Magufuli katika mpango wake kamambe wa kufuta upinzani Tanzania.
Hatujasema kipindi Mbowe anawekwa ndani Rais alikuwa Magufuli. Wewe ni Kasomi ka wapi?
kwanini SSH alishindwa kufuta kesi kama alivyofuta nyingine nyingi na kuamua kumuweka ndani
 
akawa ameaminishwa kuwa ule upupu wa kina Swila, Urio, Kingai kuwa ni ushahidi tosha wa ugaidi. Lakini alipoanza kuifuatilia Ile kesi akaja kugundua kuwa hakukuwa na ushahidi wowote wa maana.
Haya mshauri Mama awafanyeje wasukaji wa kesi hii akina Kingai, Swila, Urio na wengine wote undercovered najua kuna a lot of resources zimekuwa ulitilized kwenye hii kesi!!
 
Ukisoma haya maandishi ya mleta UZI unaweza kufanya HITIMISHO hivi; IQ au thinking capacity ya Watanzania tulio wengi ipo chini mno, kiasi kwamba sielewi hasa shule zinatusaidia nini; mleta UZI kama hana connection na mamlaka then ndio hivo uwezo wetu wa kufikiri ndio huo, kama yupo kwenye mamlaka ndio hayo hayo tu ya kutudharau kwamba sisi wasomaji, uwezo wetu wa kufikiri na ku analyse issues HATUNA na ndio maana tunaweza kutupiwa kila UJINGA cause wanajua TUTAAMINI tu. Hili la Mbowe hakuna namna ya kijisafisha, awamu hi ndio ya kulaumiwa. Kwani Mbowe aliondoka nchini lini? Mbowe hakutoroka, kaondoka kwa njia za kawaida kabisa, passport yake imegongwa mihuri vizuri tu, Lema na Lissu ni kweli walitoroka but sio Mbowe. Mbowe alitakiwa kufungwa na utawala hu, sio Magufuli
 
Ndio maana Katiba mpya ni muhimu sana
Kuna wakati huwa naona hizi kelele za katiba mpya zinatumika kama kisingizio cha kuficha madhaifu na maujinga yetu, kwamba hatuna tunaloweza kufanya lolote katiba kubadili lolote kisa ni hii katiba tuliyonayo hali inayofanya tuhisi kuwa hiyo katiba mpya ni kama suluhisho la ajabu kwa matatizo yote. Ni kama akili zimelala zinasubiri hakuna tunachoweza kufanya tunasubiri katiba mpya na kibaya hatuna tunachoweza kufanya ili ipatikane hiyo katiba mpya suluhisho la ajabu kwa matatizo yote.
 
Kuna kitu Lumumba mmejifunza kuhusu hii kesi...

Mbowe sio mdgo kama mlivofikiria wengi...

With time mtazidi kuelewa.
Mbowe ni mkubwa kweli ila kimbembe usiombe upewe wewe hiyo kesi kama ya Mbowe kama utaona hata watu kuzungumzia tu achilia mbali kukuombea kwa rais uachiliwe, utaozea jela tu kama ambavyo wengine wanaozea jela huko kwa kesi za mchongo tu ila Mbowe yeye katoka.

Wanasiasa ni watu muhimu si sawa na sisi.
 
Kesi ilikuwa ni ya Jiwe kujiandalia utawala wa milele, na kuua upinzani. Lakini Mungu si Athumani , akatenda jambo
Jambo lipi hilo la Samia kumuweka jela Mbowe hali ya kuwa hakuna ushahidi ili baadaye amtoe na kupiga nae picha ikulu na kuchukua point tatu?
 
Kesi ya Mbowe ilipikwa chini ya utawala wa Magufuli hivyo Mama Samia hatakiwi kulaumiwa Bali apongezwe Kwa kuwa tayari kurekebisha makosa ya mtangulizi wake.

1. File lilifunguliwa July 18, 2020 na Swila,Kingai DCI et al kipindi Cha JPM.

2. Walinzi wa Mbowe walikamatwa na kubambikiwa madawa ya kulevya, na silaha na sare za JWTZ mwezi August, 2020 kipindi Cha JPM.

3. Walinzi wa Mbowe waliandikishwa maelezo ya uongo kuwa wamekiri na kumtaja Mbowe kuhusika na ugaidi mwezi August 2020 kipindi Cha JPM.

4. Mashahidi karibia wote waliandikishwa maelezo mwaka 2020 kipindi cha JPM.

5. Lengo likawa kumkamata Mbowe na kumfungulia mashtaka soon baada ya uchaguzi, na haikuwa Mbowe tu ilikuwa Bali ilikuwa waunganishwe Tundu lissu na Godbless Lema.

6. Taarifa zikavuja, Tundu lissu alivyosikia Kuna kesi pending alikimbilia ubalozi wa Ujerumani then akakimbia nchi.

7. Lema aliposikia polisi wanamsaka akakimbia akavuka mpaka wa Kenya then akaenda Canada.

8. Na Mbowe akakimbia nchi akaenda zake Dubai, ndiyo kipindi alichokaa sana nje ya nchi akarudi ashadungwa chanjo ya Corona na ndiyo maana hata wasaidizi wa Samia walimwambia Samia kuwa Mbowe alikimbia nchi ni kweli alikimbia, amerudi JPM akiwa hoi.

Sasa katika mazingira haya huwezi kubisha kuwa aliyesuka hii kesi ni Magufuli. Samia ameingia Ikulu katika mazingira ambayo hakuwa hata amejianda hivyo alikuwa anahitaji muda ku cope na vitu vingi. Huku chini wasaidizi wake wakiwa tayari Wana ushahidi waliopika Kwa maelekezo ya Mwendazake. Amekuja kushtuka kesi ishafunguliwa na wakamdanganya kuwa Wana ushahidi wa kutosha kuthibitisha ugaidi wa Mbowe.

Mimi naamini Rais Samia ahusiki na hii kesi kule kuongea BBC ilikuwa ni kutokana na kudanganywa na wasaidizi wake na Kwa kuwa si mwanasheria na ni mtu anayeheshimu ushauri wa wataalamu akawa ameaminishwa kuwa ule upupu wa kina Swila, Urio, Kingai kuwa ni ushahidi tosha wa ugaidi. Lakini alipoanza kuifuatilia Ile kesi akaja kugundua kuwa hakukuwa na ushahidi wowote wa maana.
View attachment 2139966
Alu akakamatwa lini vile??
 
Awamu hii ukitaka kufanikiwa kimaisha tukana Magufuli tena sana tu.

Na Rais wa sasa wakati ikipikwa alikua msaidizi namba moja wa Magufuli , alikua anafahamu ila akamua kukaa kimya.
Ulitakaje kwa mfano
 
Kama kweli Hukumu ya HAKI ya milele ipo kutokana na matendo ya mwanadamu aliyoyafanya hapa duniani, huyu jamaa sijui ana hali gani huko
 
If She wants to get all the credit, she should at-least take part of the blame....

Naanza kuona harufu ya Unafiki wa hali ya Juu
 
Kesi ya Mbowe ilipikwa chini ya utawala wa Magufuli hivyo Mama Samia hatakiwi kulaumiwa Bali apongezwe Kwa kuwa tayari kurekebisha makosa ya mtangulizi wake.

1. File lilifunguliwa July 18, 2020 na Swila,Kingai DCI et al kipindi Cha JPM.

2. Walinzi wa Mbowe walikamatwa na kubambikiwa madawa ya kulevya, na silaha na sare za JWTZ mwezi August, 2020 kipindi Cha JPM.

3. Walinzi wa Mbowe waliandikishwa maelezo ya uongo kuwa wamekiri na kumtaja Mbowe kuhusika na ugaidi mwezi August 2020 kipindi Cha JPM.

4. Mashahidi karibia wote waliandikishwa maelezo mwaka 2020 kipindi cha JPM.

5. Lengo likawa kumkamata Mbowe na kumfungulia mashtaka soon baada ya uchaguzi, na haikuwa Mbowe tu ilikuwa Bali ilikuwa waunganishwe Tundu lissu na Godbless Lema.

6. Taarifa zikavuja, Tundu lissu alivyosikia Kuna kesi pending alikimbilia ubalozi wa Ujerumani then akakimbia nchi.

7. Lema aliposikia polisi wanamsaka akakimbia akavuka mpaka wa Kenya then akaenda Canada.

8. Na Mbowe akakimbia nchi akaenda zake Dubai, ndiyo kipindi alichokaa sana nje ya nchi akarudi ashadungwa chanjo ya Corona na ndiyo maana hata wasaidizi wa Samia walimwambia Samia kuwa Mbowe alikimbia nchi ni kweli alikimbia, amerudi JPM akiwa hoi.

Sasa katika mazingira haya huwezi kubisha kuwa aliyesuka hii kesi ni Magufuli. Samia ameingia Ikulu katika mazingira ambayo hakuwa hata amejianda hivyo alikuwa anahitaji muda ku cope na vitu vingi. Huku chini wasaidizi wake wakiwa tayari Wana ushahidi waliopika Kwa maelekezo ya Mwendazake. Amekuja kushtuka kesi ishafunguliwa na wakamdanganya kuwa Wana ushahidi wa kutosha kuthibitisha ugaidi wa Mbowe.

Mimi naamini Rais Samia ahusiki na hii kesi kule kuongea BBC ilikuwa ni kutokana na kudanganywa na wasaidizi wake na Kwa kuwa si mwanasheria na ni mtu anayeheshimu ushauri wa wataalamu akawa ameaminishwa kuwa ule upupu wa kina Swila, Urio, Kingai kuwa ni ushahidi tosha wa ugaidi. Lakini alipoanza kuifuatilia Ile kesi akaja kugundua kuwa hakukuwa na ushahidi wowote wa maana.
View attachment 2139966
Nakubaliana na wewe hii imepima kujua Mama ni mtu dhaifu sana
 
Back
Top Bottom