Kesi ya Mbowe ichochee mageuzi makubwa katika jeshi la Polisi na uwanja wa haki nchini

Yoda

JF-Expert Member
Jul 22, 2018
37,617
46,257
Kesi ya mbowe imeuonyesha umma mkubwa utendaji wa jeshi la polisi ambao haukuwa unafahamika na wengi. Bila kujali hukumu ya mwisho ya kesi hii kwa washtakiwa wote wanne jeshi la polisi na tasnia ya haki inahitaji mageuzi makubwa angalau Sita.

1.Sheria inayoweka ulazima wa kuweka camera za CCTV kwenye vituo vyote vya polisi na

2.Kamisheni huru ya kiraia juu ya jeshi la polisi kuratibu utendaji wake, kushughulikia malalamiko dhidi ya jesho la polisi na kupendekeza hatua za nidhamu kwa serikali pale ambapo inabidi. Ni muhimu kamisheni hiyo iwe chini ya bunge na iwajabike kwa bunge tu.

3.Ajira ndani ya jeshi la polisi iwe kuanzia ngazi ya diploma. Elimu ni muhimu sana katika namna binadamu anavyofanya kazi zake kwa ufanisi na kufuata utaratibu.

4.Makosa yote yawe na dhamana. Makosa yasiyo na dhamana yanaacha ombwe kubwa sana katika utendaji wa polisi kwa sababu yanawapa nguvu kubwa sana zisizodhibitiwa.

5.Iwepo sheria ya kuwafikisha watuhumiwa katika mahakama zenye uwezo kamili wa kusikiliza kesi zao na pale tu ambapo ushahidi umekamilika. Haina maana yoyote kuwapeleka washtakuwa katika mahakama isiyo na uwezo wa kusikiliza kesi yao au ushahidi ukiwa haujakamilika.

6.Iwepo sheria inayotoa fursa ya kudai fidia kwa watu ambao wameshikiliwa mahabusi kwa zaidi ya nusu mwaka au kufungwa kimakosa na baadaye wakaachiwa au kufutiwa hukumu zao na mahakama. Uwajibikaji wa aina hii utaleta nidhamu na taadhari kubwa katika kushughulika na haki za watu.
 
Madhila yatokanayo na utendaji mbovu wa polisi yanawakuta hata makada kindakindaki wa CCM wakati mwingine, busara iwatume kufanya mageuzi haya hata kabla hawajaondoka madarakani kwa sababu hakuna uhakika hata wapya watakaoingia baada yao watayatekeleza haya angalau ndani ya muda mfupi. Haya ni kwa manufaa ya wote.
Ni lazima kwanza CCM iondoke madarakani ndio haya yatekelezeke.
 
Kesi ya mbowe imeuonyesha umma mkubwa utendaji wa jeshi la polisi ambao haukuwa unafahamika na wengi. Bila kujali hukumu ya mwisho ya kesi hii kwa washtakiwa wote wanne jeshi la polisi na tasnia ya haki inahitaji mageuzi makubwa angalau Sita.

1.Sheria inayoweka ulazima wa kuweka camera za CCTV kwenye vituo vyote vya polisi na

2.Kamisheni huru ya kiraia juu ya jeshi la polisi kuratibu utendaji wake, kushughulikia malalamiko dhidi ya jesho la polisi na kupendekeza hatua za nidhamu kwa serikali pale ambapo inabidi. Ni muhimu kamisheni hiyo iwe chini ya bunge na iwajabike kwa bunge tu.

3.Ajira ndani ya jeshi la polisi iwe kuanzia ngazi ya diploma. Elimu ni muhimu sana katika namna binadamu anavyofanya kazi zake kwa ufanisi na kufuata utaratibu.

4.Makosa yote yawe na dhamana. Makosa yasiyo na dhamana yanaacha ombwe kubwa sana katika utendaji wa polisi kwa sababu yanawapa nguvu kubwa sana zisizodhibitiwa.

5.Iwepo sheria ya kuwafikisha watuhumiwa katika mahakama zenye uwezo kamili wa kusikiliza kesi zao na pale tu ambapo ushahidi umekamilika. Haina maana yoyote kuwapeleka washtakuwa katika mahakama isiyo na uwezo wa kusikiliza kesi yao au ushahidi ukiwa haujakamilika.

6.Iwepo sheria inayotoa fursa ya kudai fidia kwa watu ambao wameshikiliwa mahabusi kwa zaidi ya nusu mwaka au kufungwa kimakosa na baadaye wakaachiwa au kufutiwa hukumu zao na mahakama. Uwajibikaji wa aina hii utaleta nidhamu na taadhari kubwa katika kushughulika na haki za watu.
Yametimia
 
Hakika, lazima kuwa na chombo huru cha weledi juu ya polisi kuangalia na kudhibiti utendaji wao.
Hilo la pili ni la dharura haswa. Independent body or commission (whatever you call it) to oversee TPF ni muhimu mno!
 
6.Iwepo sheria inayotoa fursa ya kudai fidia kwa watu ambao wameshikiliwa mahabusi kwa zaidi ya nusu mwaka au kufungwa kimakosa na baadaye wakaachiwa au kufutiwa hukumu zao na mahakama. Uwajibikaji wa aina hii utaleta nidhamu na taadhari kubwa katika kushughulika na haki za watu
Hiyo sheria ikiwepo itafilisi hazina.
 
Back
Top Bottom